Dari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dari ya Kikanisa cha Sisto IV inaonyesha hadithi ya uumbaji.
Dari ya ubao katika hekalu la Japani.

Dari (kwa Kiing. ceiling) ni sehemu inayofunika kikomo cha juu cha chumba .

Inaficha tu paa juu yake au sehemu ya chini ya sakafu ya ghorofa ya juu.

Kuna aina nyingi tofauti za dari katika usanifu majengo.

Kuna dari tambarare na kuna dari yenye umbo la kuba. Katika majengo ya kisasa, mara nyingi dari ni uso wa chini wa sakafu ya ghorofa ya juu.

Katika majengo ya kidini, dari mara nyingi hupambwa kwa michoro au mozaiki. Mfano maarufu ni dari ya Kikanisa cha Sisto IV iliyochorwa na Michelangelo.

Dari kwenye chombo cha majini[hariri | hariri chanzo]

Kwenye meli au chombo kingine cha majini dari ni sehemu ambako watu hukaa na chini yake mizigo huwekwa. Inaweza kuitwa pia sitaha.

Tafsiri[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: