Kuba (jengo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muundo wa kuba

Kuba (Kar. قبة kubba) ni sehemu ya jengo inayoonekana kama nusu tufe iliyoko juu ya jengo fulani.

Ni sifa inayolenga kuonyesha umuhimu maalum wa jengo hili. Hivyo ni hasa makanisa, misikiti na majengo makubwa ya serikali zinazopambwa kwa kuba juu yake. Pamoja na hayo kuba inaweza kupazia sauti ya mseamji chini yake hivyo imesaidia kwa kusudi la kuwahotubia watu wengi.

Kati ya Waswahili wa Afrika ya Mashariki kuna desturi ya kupamba makaburi ya watu muhimu kama mashehe kwa kujenga kuba juu yake.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kuba zilijulikana tangu zama za kale katika Uhindi na katika mazigira ya Mediteranea. Hekalu ya Pantheon katika Roma ya Kale ilikuwa kuba kubwa duniani kwa miaka mingi. Katika karne ya 6 kanisa kuu la Hagia Sofia lilijengwa mjini Konstantinopoli. Kanisa hili ilikuwa kielelezo cha makanisa mengi yaliyojengwa baadaye. Baada ya kuingia kwa Waturuki katika eneo la Konstantinopoli walitumia kuba lake pia kama mfano kwa ajili ya misikiti mikubwa na hivyo kuba imekuwa sifa ya misikiti mingi.


Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kuba (jengo) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.