Rafadha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rafadha ya meli ilyoko nje ya maji gudani
Rfadha ya eropleni huangliwa kabla ya kuruka

Rafadha (pia: rafardha; kutoka Kar. ارفض arfadha = kusambaza‎‎) ni chombo chenye umbo la panka kinachozunguka na kusogeza ndege hewani au boti na meli kwenye maji.

Mara nyingi rafadha hutengenezwa kwa metali isipokuwa kuna pia rafadha za ubao kwa ndege au rafadha za plastiki.

Fizikia ya rafdha[hariri | hariri chanzo]

Rafadha iko mwishoni wa msukano au mtaimbo unaozungushwa na injini. Rafadha huzunguka sambamba na mwendo wa mtaimbo ukiwa na mikono yake inayosababisha mkondo katika maji au hewa. Mkondo huu unasababisha mwinuko kanieneo yaani tofauti katika kani ya maji (hewa) kwa jumla na kanieneo ndani ya mkondo. Umbo la mikono ya rafadha na mweleko wa mzunguko huleta ama kanieneo kubwa au dogo na hivyo rafadha inaweza kuvuta au kusukuma chombo chake. Rafadha ya meli kwa kawaida imetengenezwa kwa njia ili kusukuma na rafadha ya eropleni kwa kawaida imetengenzwa kwa kuvuta.

Historia ya rafadha[hariri | hariri chanzo]

Msingi wa uwezo wa rafdha ilitambuliwa na Archimedes wakati wa Ugiriki ya Kale aliyegundua mtmbo wa skrubu ya Archimedes iliyopandisha maji kutoka mtoni kwenda mashamba.

Leonardo da Vinci ni mtu wa kwanz anayejulikana kutambua nafasi ya rafadha kwa kusukuma chombo alipochora ramani ya helikopta ya kwanza lakini wakati wke teknolojia haikupatikana ilikuwa mchoro tu. Wengine kama James Watt walitambua pia uwezo wa rafadha lakini hawakuitumia katika mitambo.

Mwaka 1827 Mwaustria Josef Ressel alifaulu mara ya kwanza kutengeneza rafadha ya kusogeza meli. Wengine waliendeleza mtambo wake na kuanzia katikati ya karne ya 19 rafadha ilionekana kama teknolojia ya juu kwa meli zilizokuwa na injini ya mvuke.

Siku hizi rafadha ni teknolojia ya kawaida kwa meli hata kama mitambo mengine kama usukumaji wa jeti imeenea pia.

Ndege ndogo husogezwa kwa rafadha lakini ailimia kubwa ya ndege kubwa hutumia nguvu ya jeti isipokuwa hata jeti hutumia fizikia ya rafadha ndani yake.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: