Panka
Panka (pia: pangaboi, feni) ni kifaa kinachosababisha mwendo wa hewa, kwa kawaida kwa kusudi la kuipoza. Huwa na mikono kadhaa inayozunguka. Mwendo husababishwa na mota ya umeme.
Panka hutumiwa kupunguza hisia ya joto. Hali halisi panka haipozi hewa, kinyume chake mota ya umeme unatoa joto kidogo wakati wa kufanya kazi. Lakini mwendo wa hewa kutokana na mzunguko wa panka unasababisha uvukizaji wa jasho kwenye ngozi ya watu na hivyo hisia za baridi au angalau hisia ya kupungukiwa joto.