Biofueli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Basi itumiayo biofueli kutokana na soya
Katika nchi mbalimbali biofueli huuzwa kwa bei nafuu; hapa juu tangazo la biodiseli nchini Ujerumani

Biofueli ni fueli inayopatikana kutokana na masi ya mimea au viumbehai vingine. Tofauti na fueli kisukuku ambayo ni mabaki ya viumbehai ya miaka mingi iliyopita biofueli hutokana na masi iliyopatikana hai au iliyokaa muda kidogo tu.

Biofueli hupatikana kama dutu mango, kiowevu au gesi.

Matumizi ya biofueli ni kama nishati ya kuendesha injini za magari, kuwasha moto nyumbani au upishi. Hutumiwa pia kwa utengenezaji wa umeme.

Kuna mbinu mbili hasa kutengeneza biofueli.

  • kulima mimea yenye kiwango kikubw cha sukari au wanga kama muwa. Kwa msaada wa bakteria wanga au sukari hubadilishwa kuwa alikoholi (ethanoli).
  • kulima mimea yenye kiwango kikubwa cha mafuta katika mbegu au miili yao kama algae, michikichi (mawese) au soya.

Ethanoli hizi hutumiwa badala ya petroli na mafuta badala ya diseli katika injini ya mwako.

Njia nyingine ni kutumia ubao au manyasi mbalimbali zinazokaushwa, mara nyingi kukatwa na kupewa umbo la donge halafu kuchomwa kwa kutengeneza umeme.