Kriketi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mechi ya kriketi: mstatili nyeupe ni "pitch", watu wenye suruali nyeusi ni marefa. Mtupa mpira anatupa, wenzake wanasubiri nyuma ya wiketi na mpiganaji wa timu nyingine ili washike mpira
"Pitch" pamoja na mtupa mpira "bowler", wapiganaji wawili wa timu nyingine na refa

Kriketi (ing. cricket, tamka krikit) ni aina ya michezo ya timu inayopendwa hasa katika nchi zenye urithi wa utamaduni wa Uingereza kama vile nchi za Jumuiya ya Madola (Australia, Uhindi, Pakistan, Sri Lanka, Bangladesh, Afrika Kusini, Nyuzilandi, Visiwa vya Karibi au Zimbabwe na mengine) na katika nchi kadhaa ina sifa ya kuwa mchezo wa kitaifa (Antigua na Barbuda, Bahamas, Barbados, Bermuda, Grenada, Guyana, Jamaika na Visiwa vya Turks na Caicos). Baseball imezaliwa kutoka kwa kriketi ya Kiingereza.

Kriketi ni mchezo kati ya timu mbili unaoendelea kwa zamu kati yao. Kwa kawaida kila timu huwa na zamu 1 au 2.

Wanacheza kwenye uwanja mwenye sehemu mbili:

  • mstatili unaoitwa „cricket pitch“ mwenye urefu wa mita 20.12 (yard 22) na upana wa mita 3.05 (futi 10)
  • pitch hii iko ndani ya uwanja usio na vipimo maalumu, kwa kawaida mwenye umbo la mviringo au yai mwenye kipenyo cha mita 137 hadi 150.

Kila upande wa mstatili wa „pitch“ kuna mafimbo matatu yaliyowekwa katika ardhi yanayobeba mafimbo madogo juu yao. Uundaji huu huitwa „wiketi“. Timu moja inapelekea mwanamichezo mmoja mbele anayetupa mpira mdogo. Timu nyingine inamsimamija mpiganaji fimbo dhidi yake anayejaribu

Kila timu huwa na zamu ya kutupa mpira mdogo kwa wiketi ilhali timu nyingine inajaribu kutetea wiketi kwa kurudisha mpira kwa kuipiga kwa fimbo. Wale wanaotupa mpira hupeleka wachezaji 11 uwanjani wanaitwa “bowler”.

Wale wa timu yingine wanaojaribu kurudisha mpira kwa kuupiga kwa fimbo waitwa “batter” au “batsman” wanapeleka wachezaji 2 tu (wengine wanaingia kwenye zamu ujao).

Mwanzoni washambulizi wa “bowler” yaani wanaotupa mpira wako karibu na wiketi upande mmoja. Akina “batter” wa timu nyingine wako mmoja-mmoja kila upande karibu na wiketi.

Mtupa mpira analenga mpira kwa wiketi. Mpiga fimbo anajaribu kugonga mpira na kuirudisha. Akifaulu wachezaji wa timu nyingine wanakimbia kukamata mpira, kuushika na kuutupa tena kwa wiketi. Katika muda ambako wanafuata mpira uliopo mbali na “pitch” mpiganaji anaweza kukimbia kwa wiketi nyingine na kurudi tena, na kurudia yote wakichelewa kurudisha mpira. Kila mbio baina ya wiketi inaleta maksi kwao.

Wakati mchezaji wa mabowler amekamata mpira anairusha kwa batter upande mwingine. Kuna sheria namna gani kurusha mpira.

Wakati mpiga fimbo anakosea anatoka, na mchezaji mwingine wa timu yake anaingia kama mpiganaji. Baada ya mabadiliko 10 zamu inakwisha, na timu zinabadilishana kazi.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Kriketi kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.