Jamaika
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Out of many, one people (kutoka wengi - taifa moja) | |||||
Wimbo wa taifa: Jamaica, Land We Love Wimbo wa kifalme: God Save the King | |||||
Mji mkuu | Kingston | ||||
Mji mkubwa nchini | Kingston | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza | ||||
Serikali | Ufalme wa kikatiba Charles III Sir Patrick Allen Andrew Holness | ||||
Uhuru kutoka Uingereza |
6 Agosti 1962 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
10,991 km² (ya 166) 1.5 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2012 kadirio - Msongamano wa watu |
2,889,187 (ya 139) 252/km² (ya 49) | ||||
Fedha | Dollar ya Jamaika (JMD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-5) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .jm | ||||
Kodi ya simu | +1-876]]
- |
Jamaika ni nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi. Iko km 150 kusini mwa Kuba na 150 upande wa magharibi wa Haiti na ni kisiwa kikubwa cha tatu kati ya Antili Kubwa. Katika lugha ya Kiingereza visiwa hivyo huitwa "West Indies" (visiwa vya Uhindi wa Magharibi).
Jina limetokana na neno la Kiarawak "Xaymaca" au "Chaymaka" linalomaanisha "nchi ya chemchemi" (yaani kisiwa chenye maji matamu).
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Kisiwa kina urefu wa km 240 na upana hadi km 85. Eneo lake ni km² 10.991.
Visiwa vidogo vya Pedro Cays vyenye eneo la ha 23 jumla ni sehemu ya nchi ya Jamaika.
Mashariki mwa kisiwa kuna safu ya milima ya buluu yenye urefu wa km 100 penye kilele cha Blue Mountain Peak (m 2256 juu ya UB).
Katikati kuna nyanda za juu zilizojengwa kwa mawe ya chokaa yenye mabonde marefu.
Upande wa kusini nyanda za juu zina mtelemko mkali hadi mwambao wa bahari.
Iko mito mingi mifupi; mto mrefu ni Black River yenye km 53.4. Mto wa Hector's River una mwendo wa km 6 chini ya ardhi.
Hali ya hewa
[hariri | hariri chanzo]Hali ya hewa ni ya kitropiki. Hakuna tofauti kubwa ya halijoto mwaka wote. Halijoto ya wastani katika Kingston ni 25 °C wakati wa Januari na 27 °C wakati wa Julai.
Usimbishaji hutofautiana katika kanda mbalimbali ya kisiwa. Milima ya kaskazini-mashariki hupokea zaidi ya mm. 5.000 lakini Kingston ina mm 813 pekee. Mvua inanyesha hasa Mei, Juni, Oktoba na Novemba. Miezi ya Septemba na Oktoba inaona dhoruba kali za tufani mara kwa mara.
Miji
[hariri | hariri chanzo]Miji muhimu iko mwambaoni kwa sababu ya milima ya ndani.
- Kingston ni mji mkubwa wenye wakazi karibu laki sita. Ni mji mkuu na mahali pa chuo kikuu kikubwa cha Jamaika. Mji ulikuwa na matatizo makubwa ya usalama katika miaka ya nyuma.
- Spanish Town ni mji wa pili wenye wakazi 145.000. Ni kitovu cha eneo la kilimo cha ndizi na miwa.
- Mji wa Montego Bay upo kaskazini mwa kisiwa karibu na mahali ambako Kristoforo Kolumbus alifika mara ya kwanza. Bandari yake ni mhimili wa biashara ya nje. Ni eneo la utalii.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Wakazi wa kwanza wa Jamaika walikuwa Wataino ambao ni kabila mojawapo la Waarawak kutoka Amerika Kusini. Walikuwa wakulima na wavuvi. Wamepotea kama utamaduni wa pekee baada ya kufika kwa Wazungu kutokana na magonjwa mageni yaliyofika na Wahispania na mauaji wakati wa vita. Waliobaki waliingia katika ndoa na Wazungu au Waafrika waliofika baadaye na kuwa sehemu ya wakazi chotara kisiwani.
Kristoforo Kolumbus alifika mwaka 1494 na kuweka kisiwa chini ya utawala wa Hispania. Aliamini ya kwamba alifika Uhindi akaita visiwa hivi "Uhindi wa Magharibi" na wenyeji wakaitwa "Indios" (kwa Kihispania "Wahindi") na baadaye mara nyingi "Wahindi wekundu".
Mwaka 1655 Waingereza waliteka kisiwa wakaanzisha uchumi wa mashamba makubwa ya miwa. Jamaika imekuwa mahali pakuu pa kutengeneza sukari duniani kote. Watumwa wengi Waafrika walipelekwa kisiwani kama wafanyakazi kwenye mashamba hayo. Ndio mababu wa 90% wa wakazi wa leo wa Jamaika.
Kati ya miaka 1834 na 1838 utumwa ulifutwa.
Mwaka 1958 Jamaika ilianza kuelekea uhuru kama jimbo la "Shirikisho la Uhindi wa Magharibi".
Uhuru kamili ulipatikana mwaka 1962.
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2012 Jamaika ilikuwa na wakazi 2,889,187. Nusu yao waliishi mjini. Umri wa wastani ni miaka 23, thuluthi moja ni watoto hadi miaka 14.
Takriban 91.4 % ya wakazi ni wa asili ya Afrika. Mababu walikuwa watumwa kutoka Afrika waliofikishwa kisiwani katika karne ya 17 na karne ya 18 au ni machotara au wa asili ya Ulaya na Uchina.
Wakazi asilia walikuwa Waarawak na Wataino ambao hawako tena kama vikundi vya pekee; wengi walikufa kutokana na magonjwa ya Wazungu au vita vya miaka ya kwanza baada ya kufika kwa Wahispania. Wengine walichanganyikana na vikundi vingine.
Mbali ya wakazi, Wajamaika au wenye asili ya kisiwa kama 2,500,000 wanaishi nje ya nchi.
Lugha
[hariri | hariri chanzo]Pamoja na lugha rasmi ambayo ni Kiingereza kuna pia aina ya Krioli yenye asili ya Kiingereza: ndiyo inayotumika kawaida.
Dini
[hariri | hariri chanzo]Wakazi walio wengi hufata Ukristo hasa katika madhehebu ya Uprotestanti kama vile:
- Church of God (24%)
- Wasabato (11%)
- Wapentekoste (10%)
- Wabaptisti (7%)
- Waanglikana (4%)
- United Church (2%)
- Wamethodisti (2%)
- Wamoravian (1%)
- Brethren (1%)
Wakatoliki ni 2%, na vilevile Mashahidi wa Yehova.
Dini iliyoanzishwa Jamaika ni Rastafari ambayo mwaka 2001 ilikuwa na wafuasi 24.000.
Utamaduni
[hariri | hariri chanzo]Muziki ni sehemu muhimu sana katika utamaduni wa Jamaika. Hasa muziki ya Reggae umejulikana kote duniani. Mwanamuziki mashuhuri hasa wa Jamaika alikuwa Bob Marley na kikundi chake cha "The Wailers".
Pia Wajamaika wana mafanikio makubwa katika riadha, hasa ya masafa mafupi.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Ahmed, Faiz (2008). The Development Path Taken by Jamaica: A brief account of the islands natural-history, economic policies, and social conditions (PDF). (pp. 45–83)
- Arbell, Mordehay (2000). The Portuguese Jews of Jamaica. Canoe Press. ISBN 978-976-8125-69-9.
- Ammar, N. From Whence they came. The Jamaica Journal.
- Bahadur, Gaiutra. Coolie Woman: The Odyssey of Indenture. The University of Chicago (2014) ISBN 978-0-226-21138-1
- Chapman, Valentine Jackson (1963). The marine Algae of Jamaica: Part II: Phaeophyceae and Rhodophyceae.
- Hall, D. Bounties European Immigration with Special Reference of the German Settlement at Seaford Town, Parts 1 and 2. Jamaica Journal, 8, (4), 48–54 and 9 (1), 2–9.
- Issa, Suzanne (1994). Mr Jamaica, Abe Issa: a pictorial biography. S. Issa. ISBN 978-976-8091-69-7.
- Jacobs, H. P. (2003). Germany in Jamaica. Indian heritage in Jamaica. The Jamaica Journal, 10, (2,3,4), 10–19,
- Mullally, R. (2003). "One Love' The Black Irish of Jamaica. The Jamaica Journal, 42, pp. 104–116.
- Parboosingh, I. S. An Indo-Jamaica beginning in The Jamaica Journal, 18, (3), 2–10, 12.
- Senior, Olive (2003). Encyclopedia of Jamaican heritage. Twin Guinep Publishers. ISBN 978-976-8007-14-8.
- Sherlock, Philip Manderson; Bennett, Hazel (1998). The story of the Jamaican people. Ian Randle Publishers. ISBN 978-1-55876-145-2.
- Thomson, Ian (2009). The dead yard: tales of modern Jamaica. Nation Books. ISBN 978-0-571-22761-7. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-18. Iliwekwa mnamo 2015-02-14.
{{cite book}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - Williams, Joseph John (1932). Whence the "black Irish" of Jamaica?. L. MacVeagh, Dial Press, Inc.
- The Gleaner. Seaford Town Advertising Feature. 14 August 2003, D7-8,
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Government of Jamaica Ilihifadhiwa 20 Februari 2009 kwenye Wayback Machine.
- Official webpage of Queen Elizabeth as Queen of Jamaica
- Official website of the Jamaica Information Service Ilihifadhiwa 25 Februari 2011 kwenye Wayback Machine.
- The Cabinet Office of the Government of Jamaica Ilihifadhiwa 29 Aprili 2011 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jamaika kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |