Mwanamuziki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mguso bora wa muziki

Mwanamuziki ni mtu anayepiga vyombo vya muziki kama vile gitaa au piano au mtu mwenye kuimba.

Mwanamuziki ni mtu anayetunga muziki, hata kama anaandika nyimbo kwa ajili ya kupigwa na watu wengine. Mtu anayetunga nyimbo anaitwa mtunzi. Kawaida mtunzi huwa haimbi, lakini kuna kipindi mtunzi naye huwa anaimba japokuwa yeye ni mtunzi.

Hapa kuna orodha chache ya wanamuziki maarufu duniani:

Mwanamuziki pia anaweza kuunda kundi la muziki na kuweza kuimba nao pamoja. Kama kundi la muziki lina watu wengi wanaopiga vyombo vya muziki kwa pamoja, kama vile muziki wa kina Beethoven, basi inaitwa orchestra. Na kama watu wengi wanaimba, kama jinsi inayokuwa katika kanisa, hiyo inaitwa kwaya. Na kama watu wachache tu wanaimba na kutumia viyombo kadhaa, basi hao wanaitwa bendi. Kuna kipindi hata bendi nayo huwa na jina sawa tu na lile la mwimbaji.

Hapa kuna orodha chache ya mabendi maarufu duniani:

Na hapa kuna orodha tena ya orchestra mashuhuri duniani:


Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwanamuziki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.