Nenda kwa yaliyomo

Karate

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kareti)
Mwanafunzi wa karate akiwa amevaa karategi.
Mashindano ya Karate
Kanda za karate zenye rangi mbalimbali
Mwalimu Hanashiro Chomo
Mashindano ya Karate duniani mnamo mwaka 2006 mjini Tampere, Finland, fainali ya uzani mzito kwa wanaume
Mashindano ya Karate duniani mnamo mwaka 2006 mjini Tampere, Finland, fainali ya uzani mzito kwa wanaume
Neno 'Karate' kwa maandishi ya kichina

Karate (pia kareti, kutoka Kijapani: 空手) ni aina ya michezo ya mapigano kutoka nchini Japani.[1] Ilianzishwa kwenye kisiwa cha Okinawa ikaenea Japani kwenye mwanzo wa karne ya 20 na kusambaa duniani baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.[2]

Karate inatumia kama silaha za mapigano pande zote za mwili kama vile mkono, ngumi, kisugudi au mguu.

Mafunzo ya karate huwa na ngazi tatu:

  • kihon inahusu misingi
  • kata ni namna ya kutumia misingi hiyo
  • kumite ni matumizi yake katika mapigano

Kati ya michezo ya mapigano kama mchezo wa ngumi au kupiga mwereka karate inaweka mkazo kwa nguvu ya kiroho sawa na nguvu ya mwili.

Karate imefahamika duniani zaidi kutoka filamu za karate kuanzia miaka ya 1960.

Mwalimu wa karate kwa Kijapani huitwa "sensei" (kwa Kiingereza "master").

Nguo za Karate

[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa kucheza karate watu huvaa nguo za pekee zinazoitwa karategi ambazo ni suruali na jaketi nyeupe. Juu ya jaketi huwa na mkanda wenye rangi fulani. Rangi inaonyesha cheo ambacho mtu amefikia katika ujuzi wa karate. mkanda mweusi huonyesha cheo cha juu.

Karate katika Mchezo ya Olimpiki

[hariri | hariri chanzo]

Karate itachezwa kwa mara ya kwanza katika Michezo ya Olimpiki mwaka 2021 mjini Tokyo.[3]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  1. Nussbaum, Louis-Frédéric. (2005). "Karate" in Japan Encyclopedia, p. 482.
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-02. Iliwekwa mnamo 2009-03-02.
  3. "Olympic karate at Tokyo 2020: Top five things to know". Olympic Channel. Iliwekwa mnamo 2021-05-25.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Karate kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.