Nenda kwa yaliyomo

Suruali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Suruali ya kawaida.

Suruali ni vazi linaloshonwa na linalovaliwa kutoka kiunoni hadi miguuni chini na lenye nafasi mbili zinazotenganishwa kupenyezea miguu.

Kwa asili ni nguo ya wanaume, lakini inavaliwa na wanawake pia mradi yamefanyika mabadiliko kadhaa katika ushonaji.

Suruali ndefu

[hariri | hariri chanzo]

Suruali ndefu lianalojulika kwa kimombo kama trousers au pants ni vazi linalovaliwa kufunika mwili kutoka kwa kiuno kwenda chini hadi kwa miguu. Vazi hili lilikuwa la wanaume katika tamaduni nyingi. Kwa sasa, hata wanawake wamelikumbatia na kuanza kulivaa.

Vazi hili hutengenzwa kwa vitambaa mbalimbali kama vile pamba, polyester,denim na vingine.

Suruali fupi (Kaptula)

Katika jamii nyingi za Kiafrika, vazi la suruali ndefu huvwaliwa na wazee huku watoto wavulana wakivalia kaptula ambayo ni kama suruali ndefu lakini huwa ndogo na hufikia kwa magoti.

Suruali ndefu za kazini

[hariri | hariri chanzo]

Ugumu au uzito wa kitambaa kinachotengenezewa suruali ndefu hutegemea na kazi ambazo mtu anafanyia. Kwa mfano wanafanya kazi za ofisi watavalia suruali ndefu zilizo na kitambaa chepesi huku wanafanyia kazi kwa mijengo au katika kampuni za kutengenezea vitu watavalia suruali zenye kitambaa kizito. Kulingana na makala ya work pants Ilihifadhiwa 22 Septemba 2018 kwenye Wayback Machine., unaponunua suruali za kazi za ujenzi wafaa ungalie kwamba vazi hilo laweza kukuruhusu kufanya kazi na vilevile kukaa kwa muda mrefu kabla ya kuharibika.

Historia ya suruali ndefu

[hariri | hariri chanzo]

Suruali ndefu ambayo yakadiriwa kuwa ndiyo ya kwanza kuwahi tengenezwa ilipatikana katika makaburi ya Yanghai, Turpan kule nchini China na yasemekana kwamba ilitengenezwa katika karne ya 10 kabla ya Kuzaliwa kwa Kristo.

Wanawake na uvaaji wa suruali

[hariri | hariri chanzo]
Suruali ya harem pants ya hapo zamani.

Hivi leo, ni jambo la kawaida kuona wanawake wakiwa wamevalia suruali ndefu. Kumekuwa pia na suruali zao za kwenda kazini na hata suti ambazo hujumuisha koti na suruali ndefu. Uvaaji huo haukuwepo katika karne ya 17. Kulikuwa hata na vikao ambavyo vilikataza wanawake kuvalia vazi hili katika miji mikuu ya Amerika katika karne ya 19.

Hata hivyo watu kama Paul Poiret walileta mabadiliko ya kuleta suruali ndefu inayojulikana kama harem pants Ilihifadhiwa 29 Agosti 2018 kwenye Wayback Machine. au sirwal ambayo huwa pana sana kwa katikati na kushikwa kwa nyonga za miguu.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Suruali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.