Ushonaji
Mandhari
Sanaa ya ushonaji ni ufundi unaotumika tangu zamani sana kutengeneza vitu mbalimbali kwa kutumia vifaa maalumu au mikono. Mfano wa vitu hivyo ni nguo, mapazia n.k.
Ushonaji unasaidia kuongeza ujuzi wa kubuni; pia ushonaji unamsaidia binadamu kukidhi mahitaji yake ya kila siku na unaingiza pato kwa taifa.
Kwa maelfu ya miaka, ushonaji wote ulifanywa kwa mikono. Uvumbuzi wa cherehani katika karne ya 19 na kuongezeka kwa utumiaji wa kompyuta katika karne ya 20 ulisababisha uzalishaji mkubwa na usafirishaji wa vitu vilivyoshonwa, lakini kushona kwa mkono bado kunafanywa ulimwenguni kote.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |