Cherehani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Cherehani cha zamani cha Singer
Jinsi ya kuunganisha uzi wa juu na uzi wa chini katika cherehani

Cherehani (pia: charahani; kutoka Kiajemi چرخ, charakh, "gurudumu" na خان, khan "nyumba") ni mashine ya kushonea vitu kama kitambaa, nguo, viatu au mifuko.

Inatumia uzi kwa kuunganisha vipande viwili vya kitambaa au ngozi. Tofauti na ushonaji kwa mkono, cherehani hutumia nyuzi mbili, moja ya juu na nyingine ya chini, zinazounganishwa.

Siku hizi mwendo wa cherehani unatokana mara nyingi na injini ya umeme. Kuna pia vyerehani vinavyosukumwa kwa mguu au kwa mkono.

Siku hizi kuna aina nyingi kwenye viwanda zilizobuniwa kwa shughuli maalum.

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Cherehani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.