Kipato

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kipato (kutoka kitenzi "kupata") ni kitu chochote au malipo anayopata mtu baada ya kufanya kazi fulani.

Kila mmoja lazima awe na kipato chake, haijalishi ni kiasi gani, tena kipato cha mtu ni siri yake mwenyewe.

Hata hivyo watafiti wanajitahidi kujua kipato cha taifa zima na cha wastani wa wananchi wake ili kuratibu uchumi n.k.