Michezo ya mapigano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shindano la mwereka.

Michezo ya mapigano ni jumla ya michezo ambayo kwa kawaida watu wawili wanapigana kufuatana na kanuni za mchezo.

Mifano ni mchezo wa ngumi, mwereka, judo au karate. Michezo mingi ya mashindano yatumia mikono, miguu au hata mwili kwa jumla.

Silaha zinatumiwa katika aina kadhaa za michezo kama mchezo wa vitara au kendo ambako kanuni zinahakikisha usalama wa washindani. Hivyo hakuna matumizi ya silaha za moto katika michezo ya mapigano.

Kanuni zinahakikisha ya kwamba washindani wana uwezo wa kulingana. Hivyo wanapangwa mara nyingi kwa ngazi mbalimbali kufuatana na uzito wao.

Shabaha ya mchezo wa mashindano ni kumshinda mpinzani katika uwanja wa mchezo bila kumwudhi mno, yaani bila kumpa jeraha za kudumu.

Azimio la ushindi limo mkononi mwa refa (mwamuzi) anayesimamia mashindano na kuhakikisha ya kwamba kanuni zinafuatwa.

Michezo ya mapigano inatumia mara nyingi fani za sanaa ya mapigano.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Michezo ya mapigano kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.