Karate

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mwanafunzi wa karate akiwa amevaa karategi.
Mashindano ya Karate
Kanda za karate zenye rangi mbalimbali

Karate (pia kareti, jap. 空手) ni aina ya michezo ya mapigano kutoka nchini Japan.[1] Ilianzishwa kwenye kisiwa cha Okinawa ikafika Japani penyewe kwenye chanzo cha karne ya 20 na kusambaa duniani baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.[2]

Karate inatumia pande zote za mwili kama silaha za mapigano kama vile mkono, ngumi, kisugudi au mguu.

MAfunzo ya karate huwa na ngazi tatu:

  • kihon inahusu misingi
  • kata ni namna ya kutumia misingi hii
  • kumite ni matumizi yake katika mapigano

Kati ya michezo ya mapigano kama mchezo wa ngumi au kupiga mwereka karate inaweka mkazo kwa nguvu ya kiroho sawa na nguvu ya mwili.

Karate ilifahamika duniani zaidi kutoka filamu za karate kuanzia miaka ya 1960s.

Nguo za Karate[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa kucheza karate watu huvaa nguo za pekee zinazoitwa karategi ambazo ni suruali na jaketi nyeupe. Juu ya jaketi huwa na ukanda mwenye rangi fulani. Rangi inaonyesha cheo mtu amefikia katika ujuzi wa karate. Ukanda mweusi huonyesha cheo cha juu.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nussbaum, Louis-Frédéric. (2005). "Karate" in Japan Encyclopedia, p. 482.
  2. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-03-02. Iliwekwa mnamo 2009-03-02.