Mpira wa miguu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mechi ya kandanda Angola dhidi ya Moroko mwaka 2013.

Mpira wa miguu (pia soka au kandanda) ni mchezo unaochezwa na jumla ya wachezaji ishirini na wawili katika timu mbili, kila timu ikiwa na wachezaji kumi na mmoja.

Lengo hasa la mchezo huu ni wachezaji kuumiliki mpira kwa kutumia miguu na kuuingiza katika wavu wa wapinzani mara nyingi zaidi.

Matumizi ya mikono ni marufuku isipokuwa kwa mlinda mlango katika eneo maalumu na wakati wa kurudisha mpira baada ya kutoka nje ya uwanja.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mchezaji wa mpira wa miguu, Ugiriki wa Kale.

Michezo mbalimbali ya kuchezea mpira inaweza kupatikana katika kila uwanja wa jiografia na historia. Wachina, Wajapani, Wakorea na Waitalia, wote hao walikuwa wakicheza mpira zamani kabla ya enzi zetu. Wagiriki na Waromania walitumia michezo hiyo kuwaandaa wapiganaji kabla ya vita.

Hata hivyo, ni nchini Uingereza ambapo umbo la soka la kisasa lilianza kulipuka.

Ilianza wakati mashirikisho mawili (Shirikisho la Mpira wa miguu na Mpira wa Ragbi) yalipotawanyika. Shirikisho la kwanza lilibakia Uingereza. Mnamo Oktoba 1963, Vilabu 11 vya London vilituma wawakilishi katika mkutano wa Freemasons ili kujadili na kuweka kanuni zilizokubalika kusimamia mechi zilizochezwa kati yao.

Mkutano huu ulipelekea kuanzisha kwa Shirikisho la Kandanda (Football Association).

Miongoni mwa kanuni zilizowekwa ni zile za kukataa utumiaji wa mikono kushika mpira na kunyang'anyana kwa nguvu. Soka na Ragbi zilifarakana tarehe hiyo.

Miaka minane baada ya kuanzishwa, Shirikisho la Kandanda (FA) lilikuwa na wanachama 50. Shindano la kwanza la kandanda - Kombe la FA - lilianza mwaka huo, likifuatiwa na lile la Ligi ya Ubingwa miaka 17 baadaye.

Wachezaji wawili wa Kilabu ya Darwin, John Dove na Fergus Suter walikuwa wa kwanza kulipwa kwa mchezo wao. Kitendo hiki kilikuwa mwanzo wa soka ya kulipwa iliyohalalishwa mwaka wa 1885.

Mwamko huu ulipelekea kuanzishwa kwa Mashirikisho ya kitaifa nje ya Uingereza (Great Britain). Baada ya Shirikisho la Kandanda la Uingereza, Mashirikisho yaliyofuatia ni ya Uskoti (1873), Wales (1875) na Eire (1880).

Kutokana na ushawishi mkuu wa Uingereza katika mataifa ya dunia, soka ilisambaa kote duniani.

Mataifa mengine mengi yalianzisha Mashirikisho ya Kandanda kufikia 1904 wakati Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) lilipoanzishwa. Tangu hapo, kandanda ya kimataifa imekuwa ikikua licha ya vikwazo mbalimbali.

Kufikia 1912, FIFA ilikuwa na uanachama wa mashirikisho 21, idadi iliyoongezeka na kufikia 36 mwaka 1925.

Kufikia 1930 - mwaka ambapo kwa mara ya kwanza kulikuwa na mashindano ya Kombe La Dunia, FIFA ilikuwa na wanachama 41. Idadi hii ilizidi kuongezeka na kufika 51 mnamo 1938 na 76 kufikia 1950.

Baada ya Kongamano la FIFA la mwaka 2000, kulikuwa na wanachama 204 na idadi hii inazidi kukua kila mwaka.

Kanuni[hariri | hariri chanzo]

Maagizo ya Kandanda hupitiwa na kufanyiwa mabadiliko kila mwaka (Mwezi Julai) na Shirikisho la Kandanda Duniani (FIFA).[1]

Uwanja[hariri | hariri chanzo]

Vipimo vya uwanja wa soka.

Uwanja una umbo la mstatili. Hakuna kipimo kamili, ila kanuni zinasema urefu ni baina ya mita 90 na 120, upana baina ya mita 45 na 90. Kwa michezo ya kimataifa urefu uwe baina ya mita 100 - 110 na upana baina ya mita 64 na 75.

Goli ziko kwenye pande fupi zaidi. Kuna alama ya bendera kwenye kona za uwanja. Mwaka 2008 IFAB ilijaribu kusanifisha vipimo kuwa mita 105 kwa 68, lakini kanuni hii ilisimamishwa baadaye.

Mstari ni mpaka wa uwanja. Wakati mpira uko kwenye mstari hata kwa kiasi kidogo unahesabiwa bado uko ndani ya uwanja. Kwa goli kukubaliwa sharti mpira uwe umepita mstari wa goli kabisa.

Mpangilio wa wachezaji[hariri | hariri chanzo]

[2] [3] Kuna wachezaji wa aina tatu: walinzi, wachezaji wa kiungo na wachezaji wa mbele au straika. Goli kipa au mlinda lango ni mmoja kati ya walinzi.

Ni uamuzi wa kocha kuhusu idadi ya wachezaji wa kulinda lango, wa kiungo au wa mbele, ikitegemea mfumo uliotumika. Mfumo wa 4-4-2[4] umekuwa maarufu miongoni mwa timu nyingi. Mfumo huu hujumlisha walinzi wanne pamoja na mlinda lango, wachezaji wanne wa kiungo na wawili wa mbele.

Utunukizi wa Alama[hariri | hariri chanzo]

Golikipa akiokoa mpira uliopigwa shuti ndani ya eneo la penati

Katika ligi za kitaifa na kimataifa, alama hutunukiwa kwa timu baada ya mchezo. Timu iliyoshinda hupewa alama tatu huku timu zilizotoka sare hupewa alama moja kila moja.

Ikiwa ni lazima mshindi apatikane, hasa kwenye mechi za finali, mchezo huwa na muda wa ziada kama timu hizo ziko sare. Iwapo sare hiyo huendelea mchezo huamuliwa kwa mikwaju ya penalty.

Shirikisho la Kandanda Duniani[hariri | hariri chanzo]

[5] Shirikisho la Soka Duniana (FIFA) ndilo shirikisho kuu linalosimamia kandanda duniani. Wanachama wake ni mashirikisho ya kandanda ya nchi mbalimbali. Kufikia mwaka wa 2000, lilikuwa na wanachama 204 kutoka pembe zote za dunia. Shirikisho hili huandaa mashindano mbalimbali ya soka kama vile Kombe la Dunia na pia huwatunuku wachezaji.

Orodha ya Wachezaji Maarufu Duniani[hariri | hariri chanzo]

Orodha ifuatayo inaonyesha baadhi ya wanasoka maarufu duniani, lakini haiashirii usanjari huu kulingana na ubora. Wapo wengine wengi ambao hawajatajwa hapa.[6]

Mpira wa miguu barani Afrika[hariri | hariri chanzo]

Kwa Tanzania na nchi nyingi za Afrika kuna uhaba wa wafadhiliː hiyo husababisha timu ambazo hazina uwezo wa kiuchumi kukata tamaa.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Kanuni za Soka, www.fifa.com [1]
  2. Soccer Formations, www.soccerhelp.com [2]
  3. Formations, www.expertfootball.com [3]
  4. Mfumo wa 4-4-2, www.soccer-training-guide.com [4]
  5. Kuhusu FIFA, www.fifa.com [5]
  6. Orodha ya Wachezaji Maarufu wa Soka, www.soccer-fans-info.com [6]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]