Pelé
Jinsia | mume |
---|---|
Nchi ya uraia | Brazil |
Nchi anayoitumikia | Brazil |
Jina la kuzaliwa | Edson Arantes do Nascimento |
Jina halisi | Edson |
First family name in Portuguese name | Arantes |
Jina la familia | do Nascimento |
Pseudonym | Pelé |
Nickname | O Rei, Pelé |
Tarehe ya kuzaliwa | 23 Oktoba 1940 |
Mahali alipozaliwa | Três Corações |
Tarehe ya kifo | 29 Desemba 2022 |
Mahali alipofariki | Albert Einstein Israelite Hospital |
Chanzo cha kifo | natural causes |
Sababu ya kifo | colorectal cancer, multiple organ dysfunction syndrome |
Sehemu ya kuzikwa | Memorial Necropole Ecumenica |
Baba | Dondinho |
Mama | Celeste Arantes |
Ndugu | Zoca, Maria Lusia Nascimento |
Mwenzi | Rosemeri dos Reis Cholbi, Assíria Nascimento, Marcia Aoki |
Mchumba | Xuxa |
Mtoto | Edson Cholbi Nascimento, Sandra Regina Machado |
Lugha ya asili | Kireno |
Lugha zinazozungumzwa, zilizoandikwa au zilizotiwa sahihi | Kireno, Kiingereza, Kihispania |
Kazi | association football player, politician, film actor, mwigizaji |
Taaluma | mpira wa miguu |
Mwajiri | Umoja wa Mataifa |
Nafasi ilioshikiliwa | Minister of Sports of Brazil |
Nafasi anayocheza kwenye timu | Forward (association football), Kiungo |
Eneo la kazi | Brasilia |
Mwanachama wa timu ya michezo | Santos F.C., Timu ya Taifa ya Kandanda ya Brazil, New York Cosmos, Bauru Atlético Clube, Santos F.C. |
Kabila | African Brazilians |
Mchezo | mpira wa miguu |
Handedness | right-handedness |
Namba ya Mchezaji | 10 |
Ameshiriki | 1970 FIFA World Cup, 1966 FIFA World Cup, 1962 FIFA World Cup, 1958 FIFA World Cup, 2014 Copa Libertadores |
Ameitwa baada ya | Thomas Edison |
Tukio muhimu | death and funeral of Pelé |
Tovuti | https://www.pele10.org |
Pelé (jina lake halisi ni Edison Arantes do Nascimento; 23 Oktoba 1940- 29 Desemba 2022) alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Brazili. Anahesabiwa na wengi, kama waandishi wa habari na mashabiki, kuwa mchezaji Bora zaidi wa wakati wote.
Alicheza kama mshambuliaji wa kati. Aliisaidia Brazili kutwaa kombe la dunia 1958, 1962 na baadaye tena mwaka 1970. Aliweka rekodi mwaka 1958 ya kuwa mchezaji mdogo kuliko wote duniani kucheza katika fainali ya kombe la dunia alipocheza akiwa na umri wa miaka 17. Alivuma sana katika miaka ya 1970 duniani kote.
Mwaka 1999 alichaguliwa na shirikisho la mpira wa miguu duniani kuwa mchezaji bora wa karne. Kwa mujibu wa shirikisho la mpira wa miguu alikuwa mfungaji bora wa muda wote kwa kufunga magoli 1281 kati ya mechi 1363. Ana wastani wa goli moja kwa kila mechi katika uchezaji wake wote. Katika kipindi cha uchezaji wake alikuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi duniani.
Pelé alianza kuichezea Santos akiwa na umri wa miaka 15 na timu ya taifa ya Brazil akiwa na miaka 16.Katika ngazi za kimataifa alishinda kombe la dunia mara tatu 1958,1962 na 1970,akiwa ni mchezaji wa pekee kufanya hivyo.Ni mchezaji wa kibrazili anayeongoza kwa magoli mengi zaidi kwa kufunga magoli 77 kwenye mechi 92.Kwenye ngazi ya klabu ni mfungaji bora wa muda wote katika klabu ya Santos, na aliisaidia kubeba taji la Copa Libertadores kwa miaka ya 1962 na 1963.Kwa mchezo wake wa haraka ,chenga zake na magoli yake ya ajabu yalimpa umaarufu duniani kote.Tangu alipostaafu mwaka 1977,Pelé amekuwa balozi wa mpira wa miguu duniani.
Pelé alikuwa na uwezo wa kuupiga mpira kwa mguu wowote ili kuwazidi ujanja wapinzani wake uwanjani.Akiwa bila mpira kwa muda mrefu hurudi nyuma na kufanya kazi ya kukabana kusambaza mipira na kutumia uwezo wake wa kupiga pasi kwa kutoa pasi za zinazozaa mabao na kutumia uwezo wake wa kukokota mpira kuwapita wapinzani.Brazil wanamuheshimu kama shujaa wa taifa kwa mchango wake wa kisoka na sera zilizosaidia katika kupunguza umaskini katika nchi hiyo.Katika uchezaji wake na mpaka kustaafu amepokea tuzo nyingi za timu na za binafsi kwa uwezo wake anapokuwa uwanjani na uvunjaji rekodi wake.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Pelé alizaliwa mjini Três Corações, Minas Gerais, Brazil, na ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Fluminense Dondinho (mtoto wa João Ramos do Nascimento) na Celeste Arantes.Ni mkubwa kati ya watoto wawili. Alipewa jina la shujaa wa Kimarekani Thomas Edison. Wazazi wake waliamua kuitoa herufi "i" na kumuita "Edson",lakini kulikuwa na makosa kwenye cheti chake cha kuzaliwa kusababisha litumike jina la "Edison" badala ya "Edson".F amilia yake walimpa jina la "Dico". Alipewa jina la "Pelé" alipokuwa shule inaposemekana kuwa alishindwa kutamka jina la golikipa wa timu ya Vasco Da Gama anayeitwa Bilé,alivyozidi kulitamka ndivyo alivyozidi kuchapia. Pelé aliwahi kusema hakujua maana ya jina hilo wala marafiki zake waliompa jina hilo.Lakini jina hilo lilitokana na jina la Bilé lakini kwa Kiebrania maana yake ni maajabu (פֶּ֫לֶא),lakini jina halina maana yoyote kwa KIreno.
Pelé alikulia katika hali ya umaskini huko Bauru kwenye mji wa Paulo.Alijikusanyia fedha kidogo alipofanya kazi kwenye duka la chai.Alfundishwa kucheza mpira wa miguu na baba yake lakini hakuweza mara acheze na soksi iliyojazwa na magazeti au magada ya mapera huku akifunga na kamba.Amechezea klabu nyingi za vijana kama Sete de Setembro, Canto do Rio, São Paulinho, na Amériquinha. Pelé aliisaidia Bauru Athletic Club klabu ya vijana (ikifundishwa na Waldemar de Brito) kushinda mataji mawili ya mashindano ya klabu za vijana za São Paulo.Pelé alishindana mashindano ya mpira wa miguu ya ndani ya chumba ambapo aliisaidia timu yake ya Bauru.
Pelé aliwahi kukiri kuwa mashindiano hayo yana changamoto kubwa,alisema kuwa kuwa mchezo huo ulikuwa wa haraka kidogo kuliko mpira wa miguu wa kwenye nyasi na kwamba mchezo huo ulihitaji uwezo mkubwa wa kufikiri haraka kwa kuwa kila watu wanakuwa karibukaribu ndani ya uwanja.Pelé anauheshimu sana mchezo huo kwa kuwa ulimpa uwezo mkubwa wa kufikiri papo kwa papo anapokuwa uwanjani.Licha ya hivyo mchezo huo ulimpa uwezo wa kuchezaccredits indoor football for helpin na wakubwa zaidi rika lake alipokuwa na umri wa miaka 14.Katika kila mashindano aliyowahi kucheza alikuwa akichukuliwa kama mdogo asingeweza kucheza lakini kila mashindano yanapoisha yeye ndiye anayekuwa mfungaji bora akiwa na magoli kumi na nne au kumi na tano."Hicho kilinipa kujiamini zaidi", Pelé alisema"Hapo nilijua kuwa nisiwe mwoga kwa chochote kile".
Ngazi ya klabu
[hariri | hariri chanzo]Santos
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1956, de Brito alimpeleka Pelé Santos,mji wa viwanda na bandari karibu na São Paulo,alienda kwa majaribio kwenye klabu ya Santos FC,akiwaambia mabosi kuwa kijana wa miaka 15 atakuwa mchezaji mkubwa duniani.Pelé alimshangaza kocha Lula wakati majaribio kwenye uwanja wa Estádio Vila Belmiro, na akasaini mkataba na klabu hiyo Juni 1956.Pelé alitangazwa sana kwenye vyombo vya habari kuwa nyota wa baadae.Alianza vizuri Septemba 7 1956 akiwa na umri wa miaka 15 kwenye ushindi wa 7-1 dhidi ya Corinthians Santo Andre akishinda goli la kwanza.
Wakati msimu wa 1957 ulipoanza, Pelé alipewa nafasi katika kikosi cha kwanza akiwa na umri wa miaka 16 akawa mfungaji bora wa ligi.Miezi kumi baadaye aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil.Baada ya kombe la dunia la 1958 na 1962,klabu tajiri za Ulaya kama Real Madrid, Juventus and Manchester United, walijaribu kutaka kumsajili.Mwaka 1958 Iner Milan walimsajili lakini Angelo Moratti ilimbidi akatishe mkataba huo baada ya mwenyekiti wa klabu ya Santos kushambuliwa na shabiki wa Kibrazili.Lakini mwaka 1961 serikali ya Brazil chini ya rais Jânio Quadros ilisema kuwa Pelé ni mchezaji kivutio kwa nchi hivyo haruhusiwi kuhamishwa kwenda nje ya nchi.
Pelé alishinda taji kubwa kwa mara ya kwanza akiwa na Santos mwaka 1958 ambapo timu ailishinda taji la Campeonato Paulista; Pelé alimaliza mashindano akiwa mfungaji bora wa magoli 58, rekodi inayoshikiliwa hadi sasa.Mwaka mmoja baaadaye aliisaidia nchi yake kushinda mabao 3-0 dhidi ya Vasco Da Gama kwenye michuano ya Torneio Rio-São Paulo Santos hawakuwa na uwezo wa kushindana kwenye michuano hiyo.Mwaka 1960, Pelé alifunga magoli 33 akiisaidia timu yake kurudi tena kwenye michuano ya Campeonato Paulista na kubeba taji hilo lakini walifungwa kwenye michuano ya Rio-São Paulo baada ya kumaliza wakiwa nafasi ya nane.Kwenye msimu wa 1960, Pelé alifunga magoli 47 na kuisaidia Santos kubeba taji la Campeonato Paulista.Walisonga mbele na kubeba taji la Taça Brasil mwaka huohuo kwa kuwafunga Bahia kwenye fainali.Kwenye fainali,Pelé aliibuka mfungaji bora akiwa na magoli 9.
Mwaka 1973 Pele aliitwa mpira wa miguu bora katika Amerika ya Kusini.
Ngazi ya kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Mechi ya kwanza ya Pelé kimataifa ilikuwa dhidi ya Argentina waliposhinda 2-1 Julai 7 1957 uwanja wa Maracanã.Kwenye mechi hiyo alifunga goli lake la kwanza akiwa na timu yake ya taifa akiwa na miaka 16 na miezi tisa na anabaki kuwa mchezaji mdogo wa Brazili kuwahi kufinga goli kwenye timu yake ya taifa.
Kombe la dunia 1958
[hariri | hariri chanzo]Pelé alienda nchini Sweden akiwa na jeraha la goti lakini wenzake walimtetea ili aitwe kwenye kikosi.Mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya USSR kwenye mechi ya tatu kwenye mzunguko wa kwanza wa kombe la dunia la mwaka 1958,ambapo alimpa pasi Vavá iliyozaa goli la pili.Alikuwa mchezaji mdogo kuliko wote kwenye michuano na mchezaji mdogo kuwahi kucheza kombe la dunia.Dhidi ya Ufaransa kwenye nusu fainali,Brazili walikuwa wakiongoza 2-1.
Kifo
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Desemba 29, 2022, Pelé alifariki akiwa na umri wa miaka 82 katika hospitali ya Israeli ya Albert Einstein huko São Paulo, Brazil. Wakala wake Joe Fraga alithibitisha kifo chake. Pelé alikuwa akitibiwa kansa ya utumbo mkubwa tangu mwaka 2021 na alikuwa amelazwa hospitalini kwa mwezi mmoja uliopita.[1][2][3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Pelé kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ Azzoni, Tales; Savarese, Mauricio (29 Desemba 2022). "Pelé, Brazil's mighty king of 'beautiful game,' has died". Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Pele: Brazil football legend dies aged 82", BBC.
- ↑ "Pele: Brazil football legend dies aged 82", The Athletic.