BBC

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta


British Broadcasting Corporation
Nembo la BBC
Nembo la BBC
Kutoka mji London
Nchi Uingereza
Eneo la utangazaji Kote duniani
Kituo kilianzishwa mwaka 1922
Mwenye kituo Shirika la umma katika Uingereza
Programu zinazotolewa Redio na TV kwa lugha nyingi
Tovuti www.bbc.co.uk
BBC Broadcasting House, London

The British Broadcasting Corporation (BBC) ni shirika la utangazaji la Uingereza. Shirika hili lilianzishwa mwaka 1922 kwa jina la British Broadcasting Company Ltd kama kampuni binafsi. Baadaye mwaka 1927 lilibadilishwa hadhi yake na kuwa shirika la umma. BBC ndio shirika kubwa la habari kuliko yote duniani likiwa linatoa habari na taarifa mbalimbali kwa njia ya redio, luninga, na Intaneti.

Kwa mujibu wa BBC, lengo lake ni kutoa habari, kuelimisha, na kuburudisha. Kauli mbiu yake ni "Nation Shall Speak Peace Unto Nation."

Shirika hili linaongozwa na Bodi ya Magavana wanaochaguliwa na Malkia au Mfalme wa Uingereza kwa ushauri toka kwa mawaziri wa serikali ya Uingereza. Hata hivyo, BBC inasema katika katiba yake kuwa inafanya kazi zake bila shinikizo toka kwa wanasiasa au wafanyabiashara na kuwa linawajibika kwa wasikilizaji na watazamaji wake tu.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu BBC kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.