Nenda kwa yaliyomo

Kiungo (michezo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Andrea Pirlo wa Italia akipasi mpira mbele.

Kiungo (kutoka kitenzi “kuunga”) ni mchezaji ambaye anaunganisha pasi za mipira ya nyuma na eneo la mbele la ushambuliaji ili kufunga goli katika michezo mbalimbali kama vile: mpira wa miguu, ragbi, hoki ya ugani[1].

Viungo kwa jumla hucheza katikati ya mabeki na washambuliaji wa timu yao. Baadhi ya viungo hucheza kwa nidhamu ya ukabaji, kuvunja mashambulizi ya timu pinzani na hujulikana zaidi kama viungo wakabaji. Wengine huwa wanyumbulifu zaidi katika upigaji pasi na hujulikana zaidi kama viungo wachezeshaji au viungo wa juu. Idadi ya viungo katika timu pamoja na majukumu hutegemea zaidi mfumo unaotumika na timu; mjumuisho wa wachezaji hao wakiwa uwanjani hujulikana kwa jina la kati (kwa Kiingereza midfield).[2]

Makocha wengi hupendelea kutumia kiungo mmoja kuvuruga mashambulizi ya timu pinzani, na wengine wakiwa na jukumu la kutengeneza magoli au makujumu sawa ya ukabaji na ushambuliaji. Kwa jumla, viungo ndio wachezaji wanaozunguka sehemu kubwa ya uwanja. Kwa sababu viungo ndio wachezaji wanaomiliki mpira kwa asilimia kubwa wakiwa uwanjani, nafasi hii inahitaji wachezaji walio timamu sana.[3]

Viungo wa kati[hariri | hariri chanzo]

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania kiungo Xavi alifanikiwa kuwa katika kikosi cha fifa kwa mara ya nane mfululizo

Viungo wa kati ni wachezaji ambao majukumu yao yamegawajika kwa usawa katika ukabaji na ushambuliaji ili kumiliki mchezo katikati ya uwanja. Wachezaji hawa hujaribu kupiga pasi kwa wachezaji wenzao hasa viungo washambuliaji na washambuliaji na pia kusaidia timu katika ushambuliaji kwa kukokota mipira katika eneo la wapinzani na kupiga mashuti.

Timu pinzani ikiwa na umiliki wa mpira, kiungo wa kati anaweza kushuka chini kabisa kulinda goli au kusogea mbele kumbana anayemiliki mpira ili kuuchukua. Kiungo wa kati akiwa analinda goli lake hucheza juu kidogo ya beki wa kati ili azuie mashuti ya mbali yatakayopigwa au viungo wa timu pinzani watakaojaribu kupenya kuelekea golini kwao.

(Mfumo wa)#4.E2.80.933.E2.80.933|4–3–3 na #4.E2.80.935.E2.80.931|4–5–1 zote hutumia viungo watatu wa kati. Mfumo wa 4-4-2 |4−4−2unaweza kutumia viungo wa kati wawili[4] na mfumo wa kisasa wa #4-2-3-1|4–2–3–1 mmoja kati ya viungo wa kina wawili huweza kuwa kiungo wa kati.

Viungo wa pembeni[hariri | hariri chanzo]

Viungo wa kulia na kushoto wana majukuimu yaliyo na usawa wa ukabaji na ushambuliaji sawa na viungo wa kati, ila wao hucheza pembeni karibu na mstari wa mwisho wa uwanja. Wanajukumu la kupenyeza pasi za krosi wakati wa ushambuliaji na kukaba winga wakati wakiwa wanashambuliwa.[5]

Mifumo ya kisasa ianyochezesha viungo wa pembeni ni pamoja na Mfumo wa #4.E2.80.934.E2.80.932|4−4−2, Mfumo wa #4.E2.80.934.E2.80.931.E2.80.931|4−4−1−1, Mfumo wa #4.E2.80.932.E2.80.933.E2.80.931|4–2–3–1 na Mfumo wa #4.E2.80.935.E2.80.931|4−5−1.[6] Katika maelezo yake, bwana Jonathan Wilson anaelezea maendeleo ya mfumo wa 4−4−2: "…winga wamekua viungo wa pembeni, mtu anayetegemewa kupiga krosi lakini pia kuwa katika ulinzi."[7] Wachezaji mashuhuri waliocheza kama viungo wa pembeni ni pamoja na David Beckham na Ryan Giggs.[8] [[File:2-3-2-3 formation.svg|thumb|upright|left|120px|mfumo wa #Metodo (2–3–2–3): winga nusu rangi ya njano wanacheza nafasi ya ukabaji zaidi na kusaidia washambuliaji.

Nusu winga[hariri | hariri chanzo]

Historia ya nafasi ya nusu winga mwanzoni walipewa (nusu beki) waliokua wanacheza pembezoni kabisa mwa uwanja. Imekuja kuzoeleka kwamba wachezaji wenye majukumu ya ulinzi kuwa sehemu ya mabeki wa timu.[9][10]

Viungo wakabaji[hariri | hariri chanzo]

[[File:Mario Balotelli shot Euro 2012 final 02 cropped.jpg|right|thumb|Kiungo mkabaji wa timu ya taifa ya Hispania Sergio Busquets (16, jezi nyekundu) akijaribu kuzuia shuti lililopigwa na Mario Balotelli.]] Viungo wakabaji ni wachezaji wenye majukumu makubwa ya kuimarisha safu ya ulinzi ya timu. Wachezaji hawa huweza kulinda eneo la mbele ya mabeki wake au kulinda mchezaji binafsi.[11][12][13] Viungo wakabaji wana jukumu la kuziba nafasi za beki wakati au mabeki wakabaji wakati wowote nafasi hizo zinapoachwa wazi, hasa mabeki hao wakipanda kuongeza idadi ya wachezaji wanaoshambulia.[14][15] Sergio Busquets alielezea uchezaji wake: "Kocha anatambua kua mimi ni mtiifu na ninapenda kusaidia wakati wowote, kama itanibidi kwenda pembezoni mwa uwanja kuziba nafasi ya winga, sina tatizo."[15] Kiungo mkabaji mzuri anahitaji uelewa mzuri wa kujiweka katika nafasi, kubashiri aina ya mchezo anaotumia mpinzani, kushika nafasi, kuzuia pasi kwa kukatiza, kupiga pasi na stamina pamoja na nguvu.

Viungo washambuliaji[hariri | hariri chanzo]

Kiungo mshambuliaji ni nafasi nyuma ya washambuliaji, mara nyingi hucheza katikati ya kiungo wa kati na washambuliaji, na majukumu yake ya msingi ni kutengeneza mashambulizi.[16]

Kutokana na mfumo unaotumika uwanjani, viungo washambuliaji huweza kugawanywa katika makundi matatu, viungo washambuliaji wa kushoto, kulia na wa kati. Kiungo mshambuliaji wa kati anafahamika pia kwa jina la playmaker]', au namba kumi.[17][18] Kiungo mshambuliaji mzuri lazima awe na uwezo wa kupiga pasi za mwisho kwa ufasaha, kuona nafasi za kupiga pasi, uwezo wa kupiga mashuti ya mbali na kukokota mpira bkwa ufasaha.

Winga[hariri | hariri chanzo]

Katika soka la kisasa, winga ni mchezaji asiye sehemu ya beki anayecheza nafasi za pembeni mwa uwanja kulia na kushoto. Hii inaweza kujumuisha viungo wa pembeni, viungo washambuliaji wa kulia au kushoto, au washambuliaji wa kulia na kushoto.[5]. Katika Mfumo wa#2.E2.80.933.E2.80.935 .28Pyramid.29|2−3−5 mfumo maarufu katika karne ya 19, winga walicheza pembezoni kabisa mwa uwanja karibu na mstari wa pembeni, na walitegemewa kupiga krosi kwa washambuliaji wake.[19] Kwa kawaida, winga walikua kushambulia na hawakutegemewa kushuka kusaidia ukabaji. Aina hii ya winga ulianza kubadilika miaka ya 60. Katika kombe la dunia la mwaka 1966 timu ya taifa ya Uingereza chini ya kocha wao Alf Ramsey hawakutumia winga kuanzia hatua ya robo fainali, timu hiyo ilijulikana kwa jina la "Wingless Wonders" na ndipo mfumo wa 4–4–2 ulipoanzia.[20][21]

winga wanaonyeshwa kwa rangi nyekundu, wachezaji wa pembezoni wanaonyeshwa kwa rangi buluu.

Winga ni kiungo mshambuliajia anayecheza pembezoni mwa uwanja.[22] Majukumu ya winga ni pamoja na:

 • Kutoa nafasi ya pasi pembeni mwa uwanja kwa uwepo wao.
 • Kumshinda beki kwa mbio au uwezo wa kuchezea mpira.
 • Kupokea pasi kutoka kwa viungo na kuigawa kwa njia ya krosi kwa washambuliaji wake.

Winga halisi ni mjanja, mwenye mbio na hupendelea kucheza kwenye mstari wa mwisho wa uwanja, maana hii inajumuiisha kukokota mipira kuelekea eneo la wapinzani na kupiga krosi. Mbali na hivyo, wacheaji wenye aina tofauti tofauti za kiuchezaji wanaweza kucheza kama winga. Badhi ya winga wanapendelea kuingia ndani zaidi kuliko kucheza pembeni, aina hii ya uchezaji huleta athari kubwa kwani winga hugeuka kua mchezeshaji kwani kwa kuingia huweza kupiga pasi za kukatiza kwa ufasaha mkubwa au hata kupiga shuti. Hata wachezaji ambao hawana kasi wanaweza kucheza katika nafasi hii kwa ngazi ya klabu n ahata timu za taifa..

Uwezo wa winga hujumuisha:

 • Uwezo wa kiuchezaji wa kumtoka beki wakikutana moja kwa moja.
 • Kasi ya kumshinda beki wakikutana mmoja kwa mmoja.
 • Uwezo wa kupiga krosi zenye manufaa.
 • Uwezo mkubwa akiwa hana mpira wa kusoma aina ya pasi inayopigwa na viungo washambuliaji au washambuliaji.
 • Uwezo mzuri wa kupiga pasi au kukaba mipira inayopotea wakiwa eneo la mpinzani.
 • Winga wa kisasa inampasa kua na uwezo wa kucheza pande zote za uwanja ili kumudu mabadiliko ya kiufundi yatakayofanywa na kocha.

Japokuwa winga ni nafasi inayofahamika sana, haimaanishi kwamba inatumika kila sehemu ya ulimwengu. Kuna timu nyingi zenye mafanikio zinazocheza bila ya winga. Mfano mzuri ni klabu ya Milan chini ya kocha Carlo Ancelotti katika miaka ya 2000 walicheza mfumo wenye umbo la almasi au mti wa krismasi (4–3–2–1), mfumo huu ulitegemea beki wa pembeni kutoa msaada nafasi ya winga.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. "Positions guide: Central midfield". London: BBC Sport. 1 Septemba 2005. Iliwekwa mnamo 27 Agosti 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 2. "Football / Soccer Positions". Expert Football. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-11-23. Iliwekwa mnamo 21 Juni 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 3. Di Salvo, V. (6 Oktoba 2005). "Performance characteristics according to playing position in elite soccer". International Journal of Sports Medicine. 28 (3): 222–7. doi:10.1055/s-2006-924294. PMID 17024626.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 4. "Formations guide". BBC. Iliwekwa mnamo 31 Oktoba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 5. 5.0 5.1 "Wide midfielder". BBC. Iliwekwa mnamo 1 Novemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 6. "Formations guide", London: BBC Sport. Retrieved on 22 July 2013. 
 7. Wilson, Jonathan (24 Machi 2010). "The Question: Why are so many wingers playing on the 'wrong' wings?". The Guardian. Iliwekwa mnamo 1 Novemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 8. Taylor, Daniel. "Milan wrong to play David Beckham in central midfield says Sir Alex Ferguson", 18 February 2010. Retrieved on 22 July 2013. 
 9. "Old football formations explained - Classic soccer tactics & strategies". Football Bible. n.d. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-05. Iliwekwa mnamo 31 Machi 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 10. "Football Glossary, Letter W". Football Bible. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-16. Iliwekwa mnamo 12 Agosti 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 11. Cox, Michael (20 Januari 2013). "Manchester United nullified Gareth Bale but forgot about Aaron Lennon". The Guardian. Iliwekwa mnamo 31 Oktoba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 12. Cox, Michael (16 Julai 2010). "The final analysis, part three: brilliant Busquets". zonalmarking.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-06. Iliwekwa mnamo 28 Julai 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 13. Cox, Michael (10 Februari 2013). "How Manchester United nullified threat of Everton's Marouane Fellaini". The Guardian. Iliwekwa mnamo 31 Oktoba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 14. Cox, Michael (3 Machi 2010). "Analysing Brazil's fluid system at close quarters". zonalmarking.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-06. Iliwekwa mnamo 28 Julai 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 15. 15.0 15.1 Lowe, Sid. "Sergio Busquets: Barcelona's best supporting actor sets the stage". The Guardian. Iliwekwa mnamo 30 Oktoba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 16. "Positions in football". talkfootball.co.uk. Iliwekwa mnamo 21 Juni 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 17. Wilson, Jonathan (18 Agosti 2010). "The Question: What is a playmaker's role in the modern game?". TheGuardian.com. Iliwekwa mnamo 1 Desemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 18. Cox, Michael (26 Machi 2010). "How the 2000s changed tactics #2: Classic Number 10s struggle". ZonalMarking.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-08. Iliwekwa mnamo 1 Desemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 19. Wilson, Jonathan (2013). "It's a Simple Game". Football League 125. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-04-05. Iliwekwa mnamo 1 Desemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 20. Galvin, Robert. "Sir Alf Ramsey". National Football Museum. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Juni 2011. Iliwekwa mnamo 11 Julai 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unfit URL (link)
 21. "Chelsea prayers fly to the wings". FIFA. 5 Machi 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-10-24. Iliwekwa mnamo 25 Juni 2008. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20131024161128/http://www.fifa.com/tournaments/archive/tournament= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
 22. "Positions guide: Wide midfield". London: BBC Sport. 1 Septemba 2005. Iliwekwa mnamo 21 Juni 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Kiungo (michezo) kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.