Nenda kwa yaliyomo

Luis Figo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Luis Figo

Luis Figo (alizaliwa 4 Novemba 1972) ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu wa timu ya taifa ya Ureno na klabu za Barcelona F:C:, Real Madrid za nchini Hispania na Inter Milan ya nchini Italia.

Figo alijiunga na Barcelona akitokea timu ya klabu ya Sporting CP ya nchini Ureno mwaka 1995 na kufanikiwa kuchukua kombe la UEFA la mwaka 1997.

Mwaka 2000 Figo alisajiliwa na klabu ya Real Madrid kwa ada ya paundi milioni 62 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Florentino Pérez wakati alipokuwa anagombea urais wa klabu ya Real Madrid.Mpaka sasa Figo huitwa msaliti na mashabiki wa klabu ya Barcelona.

Mwaka 2001 Figo alifanikiwa kuchukua kombela LA LIGA na kufanikiwa kuwa mchezaji bora wa mwaka.Mwaka 2005 alihamia klabu ya Inter Milan kwauhamisho huru nakucheza kwenye klabu hiyo mpaka 2009 na kustaafu soka la ushindani.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Luis Figo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.