Miroslav Klose
Miroslav Klose | ||
Maelezo binafsi | ||
---|---|---|
Jina kamili | Miroslav Klose | |
Tarehe ya kuzaliwa | 9 Juni 1978 | |
Mahala pa kuzaliwa | Opole, Poland | |
Urefu | mita 1.82 | |
Nafasi anayochezea | Mshambuliaji | |
Maelezo ya klabu | ||
Klabu ya sasa | S.S. Lazio | |
Namba | 25 | |
Klabu za ukubwani | ||
Miaka | Klabu | |
2007- | S.S. Lazio | |
Timu ya taifa | ||
2001 | Ujerumani | |
* Magoli alioshinda |
Miroslav Klose (jina kamili: Miroslaw Marian Klose; amezaliwa Opole, Poland, 9 Juni 1978) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchini Ujerumani, mshambuliaji katika Timu ya Taifa ya Ujerumani na S.S. Lazio katika Serie A (Ligi kuu ya Italia).
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Klose alizaliwa katika mji wa Opole, katika mkoa wa Silesia nchini Poland. Baba yake na mama yake walikuwa wanariadha; mama yake, Barbara Jez, alikuwa mchezaji katika timu ya taifa ya mpira wa mikono ya Poland. Baba yake Josef Klose alicheza mpira wa miguu wa kulipwa katika klabu ya Odra Opole, kabla ya kuacha nchi ya Poland nakuelekea Ufaransa kucheza katika klabu mashuhuri Ufaransa ya AJ Auxerre. Katika mwaka 1985 Miroslav na mama yake walielekea kujiunga na baba yake Klose ambae alihahamia kuishi katika mji wa Kusel, Ujerumani huko Ujerumani ndio walifika wanaishi moja kwa moja, Klose alijifunza Lugha ya Kijerumani katika shule inayopatikana katika mji wa Kindergarten, Klose alimuoa mwanamke mwenye asili ya Poland aitwae Sylwia Klose na anawatoto wa wili Luan na Noah.
Namna ya uchezaji wake
[hariri | hariri chanzo]Klose ni mchezaji maarufu duniani kwa kufunga magoli kwakutumia kichwa na hata umaliziaji wake kwakutumia miguu ni mkali pia, lakini zaidi hujulikana kwakutumia kichwa, na umaarufu wake kuhusu kutumia kichwa ni katika kombe la dunia lililofanyika Korea Kusini na Japani maana magoli mengi aliyoyafunga alifunga kwakutumia ufundi wa kichwa na alichukua na fasi ya pili baada ya Ronaldo kwakufunga magoli mengi katika shindano hilo.
Klose na Mpira wa miguu
[hariri | hariri chanzo]Klose alijifunza mpira wa miguu katika klabu ya kijiji iitwayo Blaudach-Diedelkopf, katika Ligi ya saba ya Ujerumani.Klose Umashuhuri wake ulijitokeza zaidi kuanzia kwenye klabu iitwayo 1.FC Kaiserslautern katika Bundesliga iliyomnunua kutoka kwenye klabu iitwayo FC Homburg, mwaka 2001 aliweza kujiunga na timu ya taifa ya Ujerumani Aliichezea klabu hiyo ya Kaiserslautern kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 2004 na umashuhuri wake zaidi ulijitokeza katika kombe la dunia 2002 huko Japan na Korea Kusini hata bei yake ilipanda kutokana na umashuhuri wake na uchezaji wake mpaka klabu nyingi ziliweza kujitokeza nakutaka kumnunua hadi ilipofika mwaka 2004 klabu mashuhuri Ujerumani na barani ulaya iitwayo Werder Bremen iliweza kumnunua kwa kiwango cha pesa Milioni 5 €(Euro). Klose mara nyingi hulinganishwa na wachezaji wakubwa na maarufu duniani kama vile Michael Owen na Ruud Van Nistelrooy na Ronaldo na wengine pia mashuhuri.
Kutoka Werder Bremen kuelekea Bayern Munich
[hariri | hariri chanzo]Tar 26 mwezi Juni Raisi wa klabu ya FC Bayern Munich Bwana Karl-Heinz Rummenigge alithibitisha kua klabu yake ya Bayern Munich imefikia makubaliano na klabu ya Werder Bremen kuweza kumnunua Klose na alinunuliwa kwa kiwango cha pesa Milioni 15 € (Euro) na alipimwa afya yake yote tar 28 Juni 2007 kabla yakuweka mkataba wakujiunga na klabu ya Bayern Munich kwa muda wa miaka 4.
Hakuchelewa kufaanikisha haraka nakuonekana mchezaji mzuri zaidi katika baadhi ya mechi za kirafiki alizozicheza na klabu yake mpya hiyo. Klose mechi yake rasmi ilikua dhidi ya timu yake ya zamani ya Werder Bremen katika kombe liitwalo DFB-Ligapokal (Kiswahili ni: Kombe la ligi ya Ujerumani),kombe hilo huanza kabla ya ligi ya UjerumaniBundesliga mechi hiyo iliisha kwa kufungwa Werder Bremen magoli ma 4 kwa moja lakini Klose hakuweza kucheza nusu fainali ya kombe hilo dhidi ya timu mashuhuri nyingine ya VfB Stuttgart kwani aliumia kwenye mechi ya Werder Bremen lakini alipona haraka nakuweza kushiriki fainali dhidi ya timu nyingine mashuhuri ya FC Schalke 04 na alifunga goli la ushindi katika mechi hiyo na ndio lilikua goli lake la kwanza katika mechi rasmi.
Bundesliga
[hariri | hariri chanzo]Bwana Klose mechi yake ya kwanza katika Bundesliga Ligi ya Ujerumani ilikua dhidi ya klabu iitwayo Hansa Rostock tar 11 Agosti 2007 katika mechi hiyo iliisha 3-0 na alifunga magoli ma 2 la tatu alilifunga mshirika mwenziwe katika ushambuliaji aitwae Luca Toni kutoka Italia aliefunga la 3. Baadae mwezi wa Septemba alifunga magoli matatu(Hat-trick]] dhidi ya timu iitwayo Energie Cottbus katika Bundesliga mechi hiyo iliisha 5-0.
Baada ya kuanza kwake vizuri na klabu yake hiyo, Klose alifunga magoli 20 katika mashindano yote aliyoshiriki Bundesliga na kombe la Ujerumani na magoli yake yote hayo yalisaidia kuchukua ubingwa wa mashindano yote hayo.Kombe la Ujerumani na Bundesliga na Kombe la ligi ya Ujerumani
Timu ya Taifa
[hariri | hariri chanzo]Alivyoonekana kua ni mfungaji mzuri wakati anaichezea klabu ya 1. FC Kaizerslautern, mwaka 2001 kocha wa Poland alimuomba kujiunga na timu ya taifa ya Poland baada ya yeye kusafiri kwenda Ujerumani nakumshauri kijana Klose kujiunga na timu hiyo, lakini Klose alikataa nakusema kua yuko na Paspoti ya Kijerumani na alisema kua kama mambo yatakwenda vizuri Kwa dhati nitapendelea kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani chini ya kocha Rudi Völler. Sio mbali kocha wa timu hiyo ya taifa ya Ujerumani alimuitisha kushiriki mechi dhidi ya timu ya taifa ya Albania mechi hiyo Ujerumani ilishinda 2-1. Klose alisema kuchagua kuichezea Ujerumani badala ya Poland haikua vyepesi alisema kama watu wa Poland wangeliharakia kuna uwezekano angeliichezea timu ya Taifa ya Poland,lakini alirejea nakusema kua hajuti hata kidogo kuamua kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani.
Kombe la dunia 2002 na 2006
[hariri | hariri chanzo]Kombe la dunia lilolofanyika Ujerumani,Klose alichukua tuzo ya mfungaji magoli mengi katika shindano hilo la kombe la dunia kwakupewa zawadi ya (Kiato cha Dhahabu) kwakufunga magoli ma 5 katika kombe la dunia 2002 alifunga magoli ma 5 pia na akachukua na fasi ya pili baada ya mshambuliaji maarufu kutoka Brazil aitwae Ronaldo, Kutokana na magoli hayo aliyofunga yalimfanya awe na magoli 10 katika shindano hizo alizoshiriki za mwaka 2002 na 2006.
Kombe la dunia 2002
[hariri | hariri chanzo]Katika kombe la dunia 2002 katika Korea na Japani Alifunga magoli ma 5 kwa timu yake ya Ujerumani ambayo yalimfanya achukue na fasi ya pili ya mfungaji bora akiambatana na mchezaji mashuhuri kutoka Brazil Rivaldo miongoni mwa magoli hayo alifunga magoli matatu (hat-trick) katika mechi Ujerumani ilimcharaza Saudi Arabia magoli ma 8 kwa sifuri, na magoli yake yote matano katika kombe la dunia 2002 yalikua ni ya kutumia kichwa.
Kombe la dunia 2006
[hariri | hariri chanzo]Kombe la dunia lililofanyika mwaka 2006 Ujerumani, katika mechi ya kwanza dhidi ya Kosta Rika Klose alifunga mabao mawili dhi ya timu hiyo ambayo mechi iliisha 4-2,Mechi ya kufatia ilikua dhidi ya nchi yake ya asili ya Poland mechi hiyo iliisha moja bila Klose mwenyewe hakufunga goli na la ajabu katika sehemu ya ushambuliaji alikua akishirikiana na mchezaji mungine mwenye asili ya Poland aitwae Lukas Podolski kwa ujumla wote wa wili walifunga magoli ma 8. Mechi nyingine ilikua dhidi ya Ekuador alifunga magoli yote ma wili na mechi yakufuatia ya mwenye kufungwa nakuaga mashinda ilikua dhidi ya Uswidi alitoa mchango mkubwa kwakusaidia kupatikana magoli ma wili na magoli hayo aliyafunga mchezaji Lukas Podolski. Mechi dhidi ya Argentina tar 30 Juni mwaka 2006 katika robo fainali mechi hiyo Argentina walikua wanaongoza moja bila dhidi ya Ujerumani lakini mshambuliaji huyo aliweza kugomboa goli hilo mechi hiyo iliendelea hadi zikapigwa penalti na Ujerumani ilishinda 4-2. Klose ni Mjerumani wa pili kuchukua (Golden boot) mfungaji bora katika mashindano ya kombe za duni baada ya Gerd Müller ambae alichukua zawadi hiyo mwaka 1970,Klose ana magoli kumi katika mashindano ma wili yote ya kombe za dunia. Kombe la dunia 2002 alichaguliwa katika timu iliyochaguliwa na Fifa ya wachezaji walionekana wazuri katika shindano hilo katika hiyo timu alikua pamoja na mchezaji mwenziwe Michael Ballack na pia alichaguliwa katika kombe la dunia la 2006 na wengine wachezaji wa Ujerumani wa 3,Klose ameweka rikodi yakua mchezaji wa kwanza kufunga magoli ma 5 katika kombe za dunia tofauti za kufatana 2002 na 2006.
Kombe la Ulaya 2008
[hariri | hariri chanzo]Kombe la Ulaya katika nchi mbili Uswisi na Austria. Klose alishiriki katika mechi ya mwanzo katika kundi lao dhidi ya nchi yake ya asili na alitoa mchango wa magoli mawili yote yaliyofungwa na Lukas Podolski,alicheza mechi zote zilizobaki katika kundi lao dhidi ya Kroatia na Austria katika mechi hizo mbili za mwisho katika kundi lao hakufunga goli hata li moja,ila alirejea haraka katika ufungaji wake nakufunga ma goli ma wili moja lilikua dhidi ya Ureno na Uturuki lakini Klose hakufunga goli hata limoja katika mechi ya fainali dhidi ya Uhispania
Zawadi na Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Klabu
[hariri | hariri chanzo]- SV Werder Bremen
- DFB Ligapokal Bingwa wa kombe la ligi ya Ujerumani: 2006
- FC Bayern Munich
- Bundesliga Ligi ya Ujerumani: 2007-2008
- DFB Pokal Bingwa wa kombe la Ujerumani: 2008
- DFB Ligapokal Bingwa wa kombe la ligi ya Ujerumani: 2007
Timu ya Taifa ya Ujerumani
[hariri | hariri chanzo]- Kombe la Dunia la FIFA 2002 nafasi ya pili
- Kombe la Dunia la FIFA 2006 nafasi ya tatu
- Kombe la mataifa la Ulaya 2008 nafasi ya pili
Zawadi binafsi
[hariri | hariri chanzo]- Mfungaji bora katika Bundesliga (Magoli 25) 2006
- Mchezaji wa mpira wa miguu bora wa mwaka Ujerumani: 2006
- Kiatu cha fedha katika kombe la dunia (Silver shoes): 2002
- Kiatu cha dhahabu katika kombe la dunia (Golden Shoes): 2006
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti Rasmi ya Klose
- Kuhusu Klose katika tovuti ya FC Bayern Archived 30 Aprili 2011 at the Wayback Machine.
- Klose katika Uefa.com
- Kuhusu Klose katika Gazeti mashuhuri la spoti la Kijerumani
- Klose katika Fussballdaten.de
- Klose katika Transfermarkt.de Archived 22 Desemba 2008 at the Wayback Machine.
- Klose´s Klose kutoka Silesia, Poland
!Ilani: Neno msingi la kupanga "Klose, Miroslav" linafunika neno msingi la kupanga la awali "Klose".