Bundesliga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Pciha inayoonyesha sehemu ya timu za mpira zamashindano ya Bundesliga.
Tuzo ya Kijerumani kwa ajili ya mshindi wa mashindano ya mpira wa miguu.

Bundesliga ni jina la michezo ya hali ya juu katika nyanja za michezo mbalimbali katika Ujerumani na Austria. Bundesliga ina maana ya kutaja ligi kuu ya nchi nzima. Mpira wa miguu ni mchezo mashuhuri sana katika nchi hizo mbili. Na ndiyo maana mchezo wa mpira wa miguu unajulikana sana katika nchi hizo kwa jina la Bundesliga.

Timu za mpira zinaingia katika Bundesliga kwakuwa washindi katika moja kati ya ligi ndogo za nchini humo. Timu itakayoongoza katika msimu wa mashindano hayo inaitwa Meister. Meister ni neno la Kijerumani likiwa na maana ya bingwa au mshindi. Kisheria, msimu wa michezo ya mpira huwa na kawaida ya kuanza mwezi wa sita katika mwaka uliopo hadi mwezi wa sita mwaka unaofuatia.

Timu itakayoongoza itategemea na ushindi au pointi walizozipata wakati wa msimu huo. Msimu huo umegawanyika katika sehemu mbili. Katika kila sehemu mmoja, kila timu zitashindana dhidi ya mwenzake. Katika mambo ya mpira wa miguu, timu itakayoshinda itapata pointi tatu. Kama mchezo utaisha bila kupattikana mshindi, basi timu zote mbili zitapata pointi mojamoja.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Football.svg Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bundesliga kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.