FC Augsburg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa FC Augsburg

Augsburg ni klabu ya soka ya Ujerumani iliyopo mjini Augsburg, Bavaria. FC Augsburg inacheza katika ligi ya soka ya Bundesliga nchini Ujerumani. Timu hii ilianzishwa mnamo mwaka 1907 na ilijulikana kama BC Augsburg kwanzia mwaka 1921 hadi 1969 [1]. FC Augsburg inawanachama zaidi ya 18,800 ni klabu kubwa ya mpira wa miguu huko Bavaria nchini Ujerumani.

Klabu ya Augsburg ilipanda daraja hadi ligi kuu ya Bundesliga kwa mara ya kwanza mwaka 2011 hadi sasa. Augsburg imeimarisha mifumo yao ya uchezaji katika ligi ya Bundesliga na kumaliza katika nafasi ya tano msimu wa 2014-15 na kucheza kwa mara ya kwanza katika ligi ya Ulaya UEFA Europa League mnamo mwaka 2015-16 na klabu hiyo kufika nafasi ya mzunguko wa timu 32 bora na kuondolewa na timu ya Liverpool kwa kufungwa bao 1-0.

Tangu mwaka 2009, uwanja wa FC Augsburg umekuwa uwanja wa 30,660 wenye uwezo WWK ARENA.Timu ya Augsburg inajulikana kama Fuggerstädter au FCA. Uwanja wao unajulikana kwa jina la Ulrich-Biesinger-Tribüne.

Uwanja wa fc augsburg[hariri | hariri chanzo]

Augsburg inaendelea na upinzani mkali kwa timu kama Ingolstadt na TSV 1860 Munich. Mechi kati ya klabu hizi kwa kawaida huvutia umati mkubwa wa watu.[2]

Rangi za klabu ni nyekundu, kijani na nyeupe ambazo zinaweza kupatikana kwenye kiti cha klabu wakati beji ya klabu ni sawa na nembo ya mji wa Augsburg. Duka la klabu liko karibu na Augsburg Hauptbahnhof iliyopo katikati ya jiji.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "mnamo mwaka 1907 na ilijulikana kama BC Augsburg" (kwa Kijerumani). fcaugsburg.de. Nov 2019. Iliwekwa mnamo 24 December 2019.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Tangu mwaka 2009, uwanja wa FC Augsburg umekuwa uwanja wa 30,660 wenye uwezo WWK ARENA". fcaugsburg.de (kwa Kijerumani). 16 April 2008. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-09. Iliwekwa mnamo 10 September 2019.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu FC Augsburg kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.