Lukas Podolski

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lukas Podolski

Lukas Podolski (alizaliwa 4 Juni 1985) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Vissel Kobe ya nchini Japani.

Timu yake ya kwanza kuichezea ilikuwa ni FC Köln ya nchini Ujerumani na baadaye mwaka 2008 alihamia Bayern Munich ambapo aliisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa bundesiliga.

Mwaka 2012 Podolski aliuzwa kwenda klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza na baada ya hapo alitolewa kwa mkopo kwenda Inter Milan.

Mwaka 2015 Podolski alijiunga na Galatasaray ya Uturuki. Podolski alikuwa miongoni mwa mastaa walioisaidia timu ya taifa ya Ujerumani kutwaa kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lukas Podolski kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.