Kombe la Dunia la FIFA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kombe la Dunia la FIFA ni mchuano wa kimataifa wa mchezo wa soka wa wanaume. Kombe hili hutambulika pia kama kombe la dunia la soka, kombe la dunia la mpira wa miguu au Kombe la Dunia. Kombe hili hushindaniwa na nchi wanachama wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA - Fédération Internationale de Football Association). Mashindano haya hutazamwa na watu wengi zaidi duniani kuliko mashindano yoyote yale. Mashindano ya mwaka 2002 watu wapatao bilioni 1.1 walitazama.

Baada ya hatua za mwanzo za kugombea kushirikia katika mchuano huu, nchi 32 hushiriki katika mchuano ambao hufanyika katika nchi inayoandaa/zinazoandaa mashindano hayo.

Hadi sasa ni nchi saba tu ambazo zimeweza kuchukua kombe hili toka lilipoanza kushindaniwa hapo mwaka 1930. Mashindano haya hufanyika kila baada ya miaka minne. Mwaka 1942 na 1946 hakukuwa na Kombe la Dunia kutokana na Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Brazili ndio nchi pekee ambayo imeweza kutwaa kombe hili mara tano mfululizo. Ujerumani na Italia zimelitwaa mara tatu. Nchi nyingine ambazo zimewahi kulitwaa ni Uruguay, Ufaransa, Argentina, na Uingereza.

Ujerumani ndio nchi iliyoandaa Kombe la Dunia 2006 kati ya 9 Juni hadi 9 Julai. Bingwa wa kombe hilo, Brazili, imetolewa kwenye mashindano hayo kwa kufungwa 1-0 na Ufaransa. Kombe la Dunia 2010 lilifanyika katika bara la Afrika kwa mara ya kwanza katika nchi ya Afrika Kusini. Kombe la Dunia 2014 lilifanyika Brazili.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: