Nenda kwa yaliyomo

München

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanisa kuu na jumba la manispaa ya München
Nguzo ya Bikira Maria.

München (kwa Kibavaria: Minga; kwa Kiingereza Munich; tamka: Munik) ni mji mkubwa wa tatu nchini Ujerumani (baada ya Berlin na Hamburg) na mji mkuu wa jimbo la Bavaria lililopo kusini mwa Ujerumani.

Uko kando ya mto Isar takriban mita 500 juu ya UB.

Milima ya Alpi iko karibu.

Idadi ya wakazi ni 1,320,000, lakini rundiko la jiji lina wakazi milioni mbili na nusu.

München ni kati ya vitovu muhimu vya uchumi, utamaduni na sayansi vya Ujerumani.

Klabu ya soka ya Bayern München imeshinda mara 19 kombe la kitaifa na mara tatu kombe la Ulaya.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Jina la mji linatokana na makazi ya wamonaki waliokuwa na nyumba kando ya Isar yaliyotajwa mara ya kwanza katika hati ya mwaka 1158.

Mji ukawa soko kwenye daraja la kuvuka mto.

Baada ya kuwa makao makuu ya watawala wa Bavaria mji ulianza kukua. Mnamo mwaka 1700 ulikuwa na wakazi 24,000 pekee walioongezeka kuwa 170,000 mnamo 1871 na 840,000 mwaka 1933.

Usafiri wa masafa marefu

[hariri | hariri chanzo]
Kituo cha mabasi ya masafa marefu München (nyuma) na kituo cha treni za mkoani Hackerbruecke (mbele)
  • Kuna huduma za treni za masafa marefu katika kituo kikuu cha reli na kituo cha reli mashariki pia.
  • Kuna huduma za mabasi ya masafa marefu kwenye Kituo cha mabasi ya masafa marefu München.
  • Uwanja wa ndege wa München una huduma za taifa na kimataifa.

Usafiri wa mjini na mkoani

[hariri | hariri chanzo]
Kituo cha treni za mjini Westfriedhof

Kuna treni za barabarani, treni za mjini (U-Bahn) na treni za mkoani (S-Bahn) na mabasi ya mjini na mabasi ya kieneo pia.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu München kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.