Nenda kwa yaliyomo

Kombe la Dunia la FIFA 2018

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
2018 Kombe la Dunia la FIFA
Чемпионат мира по футболу FIFA 2018
Chempionat mira po futbolu FIFA 2018
Tournament details
MwenyejiBendera ya Urusi Urusi
Tarehe14 Juni – 15 Julai
Timu32 (kutoka 5 nchi)
Miji ya mashindano12 (katika miji11 )
Final positions
Champions Ufaransa
Runner-up Kroatia
Third place Ubelgiji
Fourth place Uingereza
Takwimu ya mashindano
Idadi ya mechi62
Goli iliyofungiwa161 (2.6 kwa mechi)
Mwenye goli nyingiKigezo:Fbicon Harry Kane (6 goals)
Kigezo:AlignKigezo:Align

Kombe la Dunia la FIFA 2018 ilikuwa michuano ya 21 ya Kombe la Dunia la FIFA inayohusisha timu za taifa za wanaume katika mchezo wa soka. Michuano hii ilishirikisha timu za wanaume kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo ni wanachama wa FIFA na hufanyika mara moja kila baada ya miaka minne. Ilifanyika nchini Urusi ikaanza tangu tarehe 14 Juni na kilele cha michuno hii kilikuwa 15 Julai 2018 ambapo timu zilizoingia fainali Ufaransa na Kroatia zilicheza kuamua bingwa wa dunia. Ufaransa ilishinda kwa 4:2.

Urusi ilishinda zabuni ya kuwa mwenyeji wa michuani hii katika mkutano wa FIFA wa tarehe 2 Desemba 2010.

Ni mara ya kwanza kwa michuano hii ulifanyika katika ukanda wa Ulaya Mashariki,[1] na ni mara ya 11 kufanyika katika bara la Ulaya. Kwa mara ya kwanza michuano hii ilifanyika katika mabara mawili yaani Ulaya na Asia.[2] kwani Urusi ipo katika mabara haya mawili ambapo asilimia 75 ni bara la Asia na asilimia 25 ni bara la Ulaya[3]. Viwanja vyote kasoro kimoja vilivyotumika katika mashindano haya vipo katika upande wa Urusi ya Ulaya, lengo lilikuwa kuweza kumudu muda wa kusafiri kwa wachezaji.

Kwa gharama ya takribani $14.2 bilioni, hili ndilo Kombe la Dunia ghali zaidi katika historia. Ni Kombe la kwanza la Dunia kutumia teknolojia ya video kumsaidia mwamuzi (VAR).

Jumla ya timu 32 zishiriki michuano ya Kombe la Dunia, ambapo 31 zilipatikana kwa njia ya kufuzu na Urusi iliingia kikanuni kama mwenyeji wa michuano. Katika timu 32 zilizoshiriki mwaka 2014, timu 20 zimefanikiwa kufuzu tena kwa mara nyingine katika mashindano ya waka 2018, hizi ni pamoja na Ujerumani mabingwa watetezi, Iceland na Panama zikiwa zimeshiriki kwa mara ya kwanza kabisa michuano hii.

Jumla ya mechi 64 zilichezwa katika viwanja 12 viliviopo ndani ya miji 11 nchini Urusi na fainali ya kombe la dunia 2018 ilifanyika katika kiwanja cha “Luzhnik Stadium” mjini Moscow tarehe 15 juni 2018. [4].

Mabingwa watetezi Ujerumani walitolewa tarehe 27 juni, wameongeza idadi ya mabingwa watetezi waliowahi kutoka hatua za mwanzo kabisa katika mashindano hayo kuanzia (2002 -2018) kufikia 4, nyingine ni Ufaransa, Italia na Hispania.[5]

Mchakato wa zabuni[hariri | hariri chanzo]

Mchakato wa kumtafuta wenyeji wa mashindano ya kombe la Dunia 2018 na 2022 yalianza januari 2009, mashirika ya soka ya kitaifa waliombwa kujiandikisha kabla ya tarehe 02 Februari 2009. Nchi 9 ziliweza kutuma maombi lakini baadaye Mexico ilijitoa kutoka katika kinyanganyiro hicho. Indonesia pia ilifutwa au kutolewa kwa kushindwa kukizi vigezo baada ya serikali ya nchi hiyo kushindwa kuwasillisha barua ya kuthibitisha kuwa itashiriki katika kuiwezesha Indonesia kuandaa Michuano hiyo. Katika mchakato huo, Australia, Japan na USA waliweza kuhamishwa kutoka katika mashindano ya kuwa wenyeji 2018 kwenda kuwa washindani katika Zabuni ya 2022. Hatimaye zikasalia zabuni nne, kati yake mbili zikiwa ni za kuungana kwa nchi mbili: Uholanzi/Ubelgiji,Ureno/Uhispania,Uingereza na Urusi.

Wajumbe 22 wa Kamati kuu ya FIFA, walikutana Zurich tarehe 2 Desemba 2010 kupiga kura ili kuchagua nani atakuwa wenyeji wa michuano hiyo. Urusi ilifanikiwa kuibuka kidedea katika chaguzi hizo. Matokeo ya Zabuni yalikuwa kama ifuatavyo:[6]

Zabuni za FIFA 2018
Wazabuni Kura
Round 1 Round 2
Urusi 9 13
Ureno /Uhispania 7 7
Ubelgiji /Uholanzi 4 2
Uingereza 2 0

Timu[hariri | hariri chanzo]

Kufuzu[hariri | hariri chanzo]

Ni kwa mara ya kwanza katika historia ya kombe la dunia ambapo nchi zote 209 ambazo zipo katika umoja wa FIFA, ukitoa Urusi ambayo inaingia katika mashindano haya kutokana na kanuni ya kuwa mwenyeji, walituma maombi ya kushiriki mashindano ya kufuzu kushiriki katika mashindano ya kombe la Dunia 2018.[7]

Katika timu 32 zilizofanikiwa kufuzu kushiriki kombe la dunia la fifa 2018,Nchi 20 zilishiriki katika mashindano ya kombe la dunia ya fifa 2014.Iceland na panama hii ni mara yao ya kwanza ,huku Iceland akifahamika kuwa nchi yenye idadi ndogo sana ya watu kufanikiwa kufuzu kucheza kombe la dunia la fifa .[8].

Timu nyingine zilizofanikiwa kurudi baada ya kitambo kidogo ni,Misri mara ya mwisho ilishiriki 1990, Morocco tokea 1998, Peru tangu 1982 na Senegal ambayo ilishiriki mwaka 2002 na kufika hatua ya robo fainali. Ni kwa mara ya kwanza pia kwa nchi tatu kutoka “Nordic countries” na nchi nne za Kiarabu kufanikiwa kushiriki katika mashindano hayo. [9]


Nchi maarufu zilizoshindwa kupita ni pamoja na Italia waliowahi kuchukua kombe hilo mara nne, Uholanzi, Cameroon.

Mpangilio wa makundi ya mashindano[hariri | hariri chanzo]

Namba kwenye mabano zinaonyesha nafasi ya timu katika utathmini wa ubora wa FIFA[10].

Kundi A Kundi B Kundi C Kundi D
Bendera ya Urusi Urusi (70) Bendera ya Ureno Ureno (4) Bendera ya Ufaransa Ufaransa (7) Bendera ya Argentina Argentina (5)
Bendera ya Saudi Arabia Uarabuni wa Saudia (67) Bendera ya Hispania Hispania (10) Bendera ya Australia Australia (36) Bendera ya Iceland Iceland (22)
Bendera ya Misri Misri (45) Bendera ya Moroko Moroko (41) Bendera ya Peru Peru (11) Bendera ya Kroatia Kroatia (20)
Bendera ya Uruguay Uruguay (14) Bendera ya Uajemi Iran (37) Bendera ya Denmark Denmark (12) Bendera ya Nigeria Nigeria (48)
Kundi E Kundi F Kundi G Kundi H
Bendera ya Brazil Brazil (2) Bendera ya Ujerumani Ujerumani (1) Bendera ya Ubelgiji Ubelgiji (3) Bendera ya Poland Poland (8)
Bendera ya Uswisi Uswisi (6) Bendera ya Mexiko Meksiko (15) Bendera ya Panama Panama (55) Bendera ya Senegal Senegal (27)
Bendera ya Costa Rica Kosta Rika (23) Bendera ya Uswidi Uswidi (24) Bendera ya Tunisia Tunisia (21) Bendera ya Kolombia Kolombia (16)
Bendera ya Serbia Serbia (34) Bendera ya South Korea Korea Kusini (57) Bendera ya Uingereza Uingereza (12) Bendera ya Japani Japan (61)

Matokeo ya makundi[hariri | hariri chanzo]

Washindi wawili wa kila kundi waliendelea (rangi ya kibichi).

Kundi A[hariri | hariri chanzo]

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungiwa Tofauti ya goli
1 Bendera ya Uruguay Uruguay 9 3 3 0 0 5 0 +5
2 Bendera ya Urusi Urusi 6 3 2 0 1 8 4 +4
3 Bendera ya Saudi Arabia Uarabuni wa Saudia 3 3 1 0 2 2 7 -5
4 Bendera ya Misri Misri 0 3 0 0 3 2 6 -4

Kundi B[hariri | hariri chanzo]

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungiwa Tofauti ya goli.
1 Bendera ya Hispania Hispania 5 3 1 2 0 6 5 +1
2 Bendera ya Ureno Ureno 5 3 1 2 0 5 4 +1
3 Bendera ya Uajemi Iran 4 3 1 1 1 2 2 0
4 Bendera ya Moroko Moroko 1 3 0 1 2 2 4 -2

Kundi C[hariri | hariri chanzo]

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungiwa Tofauti ya goli.
1 Bendera ya Ufaransa Ufaransa 7 3 2 1 0 3 1 +2
2 Bendera ya Denmark Denmark 5 3 1 2 0 2 1 +1
3 Bendera ya Peru Peru 3 3 1 0 2 2 2 0
4 Bendera ya Australia Australia 1 3 0 1 2 2 5 -3

Kundi D[hariri | hariri chanzo]

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungiwa Tofauti ya goli.
1 Bendera ya Kroatia Kroatia 9 3 3 0 0 7 1 +6
2 Bendera ya Argentina Argentina 4 3 1 1 1 3 5 -2
3 Bendera ya Niger Niger 3 3 1 0 2 3 4 -1
4 Bendera ya Iceland Iceland 1 3 0 1 2 2 5 -3

Kundi E[hariri | hariri chanzo]

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungiwa Tofauti ya goli.
1 Bendera ya Brazil Brazil 7 3 2 1 0 5 1 +4
2 Bendera ya Uswisi Uswisi 5 3 1 2 0 5 4 +1
3 Bendera ya Serbia Serbia 3 3 1 0 2 2 4 -2
4 Bendera ya Costa Rica Kosta Rika 1 3 0 1 2 2 5 -3

Kundi F[hariri | hariri chanzo]

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungiwa Tofauti ya goli.
1 Bendera ya Uswidi Uswidi 6 3 2 0 1 5 2 +3
2 Bendera ya Mexiko Meksiko 6 3 2 0 1 3 4 -1
3 Bendera ya South Korea Korea Kusini 6 3 1 0 2 3 3 0
4 Bendera ya Ujerumani Ujerumani 3 3 1 0 2 2 4 -2

Kundi G[hariri | hariri chanzo]

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungiwa Tofauti ya goli.
1 Bendera ya Ubelgiji Ubelgiji 9 3 3 0 0 9 2 +7
2 Bendera ya Uingereza Uingereza 6 3 2 0 1 8 3 +5
3 Bendera ya Tunisia Tunisia 3 3 1 0 2 5 8 -3
4 Bendera ya Panama Panama 0 3 0 0 3 2 11 -9

Kundi H[hariri | hariri chanzo]

Na.
Timu
Pointi Michezo Ushindi Sare Kushindwa Goli waliofunga Goli waliofungiwa Tofauti ya goli.
1 Bendera ya Kolombia Kolombia 6 3 2 0 1 5 2 +3
2 Bendera ya Japani Japan 4 3 1 1 1 4 4 0
3 Bendera ya Senegal Senegal 4 3 1 1 4 4 3 0
4 Bendera ya Poland Poland 3 3 1 0 2 2 5 -3

Michezo ya ngazi za fainali mwaka 2018[hariri | hariri chanzo]

Mashindano ya timu 16 Mashindano ya timu 8 Nusufainali ya timu 4 Fainali ya timu 2
                           
30 Juni - Sochi            
  Bendera ya Uruguay Uruguay   2
6 Julai - Nizhniy Novgorod
  Bendera ya Ureno Ureno   1  
  Bendera ya Uruguay Uruguay   0
30 Juni - Kazan
    Bendera ya Ufaransa Ufaransa  2  
  Bendera ya Ufaransa Ufaransa   4
10 Julai - Sankt Peterburg
  Bendera ya Argentina Argentina   3  
  Bendera ya Ufaransa Ufaransa   1
2 Julai - Samara
    Bendera ya Ubelgiji Ubelgiji  0  
  Bendera ya Brazil Brazil   2
6 Julai - Kazan
  Bendera ya Mexiko Meksiko   0  
  Bendera ya Brazil Brazil   1
2 Julai - Rostov
    Bendera ya Ubelgiji Ubelgiji  2  
  Bendera ya Ubelgiji Ubelgiji   3
15 Julai - Moscow
  Bendera ya Japani Japan   2  
  Bendera ya Ufaransa Ufaransa  4
1 Julai - Moscow
    Bendera ya Kroatia Kroatia  2
  Bendera ya Hispania Hispania  1(3)
7 Julai - Sochi
  Bendera ya Urusi Urusi  1(4)  
  Bendera ya Urusi Urusi   2(3)
1 Julai - Nizhniy Novgorod
    Bendera ya Kroatia Kroatia  2(4)  
  Bendera ya Kroatia Kroatia   1(3)
11 Julai - Moscow
  Bendera ya Denmark Denmark   1(2)  
  Bendera ya Kroatia Kroatia  2
3 Julai - Sankt Peterburg
    Bendera ya Uingereza Uingereza   1   Mshindi wa tatu
  Bendera ya Uswidi Uswidi   1
7 Julai - Samara 14 Julai - Sankt Peterburg
  Bendera ya Uswisi Uswisi   0  
  Bendera ya Uswidi Uswidi   0   Bendera ya Ubelgiji Ubelgiji  2
3 Julai - Moscow
    Bendera ya Uingereza Uingereza  2     Bendera ya Uingereza Uingereza  0
  Bendera ya Kolombia Kolombia   1(3)
  Bendera ya Uingereza Uingereza   1(4)  

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Your Ultimate Guide to Watching the 2018 World Cup". Time. Iliwekwa mnamo 20 Juni 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Vyatchanin, Nikita (14 Juni 2018). "В России стартовал чемпионат мира по футболу". pnp.ru (kwa Kirusi). Iliwekwa mnamo 15 Juni 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. https://www.reference.com/geography/continent-russia-located-cf555e85dd1bbc87
  4. "Russia united for 2018 FIFA World Cup Host Cities announcement". FIFA. 29 Septemba 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Novemba 2013. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2013. {{cite web}}: More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20131113044933/http://www.fifa.com/worldcup/russia2018/news/newsid= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Defending champion Germany knocked out of World Cup while Mexico survives", 27 June 2018. Retrieved on 27 June 2018. 
  6. "World Cup 2018 and 2022 decision day – live!", The Guardian, 2 December 2010. 
  7. "Road to Russia with new milestone". FIFA. 15 Januari 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-21. Iliwekwa mnamo 2018-07-01. {{cite web}}: More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20150321054553/http://www.fifa.com/worldcup/russia2018/news/newsid= ignored (help); Unknown parameter |rchive-date= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. T.A.W.. "How Iceland (population: 330,000) qualified for the World Cup", The Economist, 12 November 2017. 
  9. "In first, 4 Arab countries qualify for FIFA World Cup Finals . Retrieved on 13 November 2017.
  10. FIFA World Ranking Archived 25 Juni 2016 at the Wayback Machine., tovuti ya FIFA, iliangaliwa Julai 2018; nafasi ya ubora hukadiriwa kufuatana na pointi za mechi za timu husika katika miaka minne iliyopita pamoja na pointi kadhaa kwa wastani wa miaka yote iliyotangulia.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Kombe la Dunia la FIFA 2018 kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.