Kamerun
| |||||
Lugha rasmi | Kifaransa, Kiingereza | ||||
Mji Mkuu | Yaounde | ||||
Mji Mkubwa | Douala | ||||
Serikali | Jamhuri | ||||
Rais | Paul Biya | ||||
Wazir Mkuu | Joseph Dion Ngute | ||||
Eneo | km² 475,442 | ||||
Idadi ya wakazi | 25,216,267 (2018) | ||||
Wakazi kwa km² | 39.7 | ||||
Uchumi nominal | Bilioni $38.445 | ||||
Uchumi kwa kipimo cha umma | $1,544 | ||||
Pesa | CFA frank (XFA) (Frank ya Afrika ya Kati) | ||||
Kaulimbiu | "Amani - Kazi - Taifa" | ||||
Wimbo wa Taifa | Ewe Kamerun, Mwanzo wa mababu wetu | ||||
![]() | |||||
Saa za Eneo | UTC +1 | ||||
Mtandao | .cm | ||||
Kodi ya Simu | +237 |
Jamhuri ya Kamerun (pia: Cameroon) ni jamhuri ya muungano katika Afrika ya Magharibi.
Imepakana na Nigeria, Chadi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Gabon, Guinea ya Ikweta na Ghuba ya Guinea.
Lugha rasmi na lugha za taifa ni Kifaransa (kinachoongoza kwa zaidi ya asilimia 80) na Kiingereza.
Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mito[hariri | hariri chanzo]
Milima[hariri | hariri chanzo]
Maeneo kiutawala[hariri | hariri chanzo]
Kamerun imegawiwa katika mikoa (regions) 10 na wilaya (départements) 58.
Mikoa ni:
- Mkoa wa Adamawa,
- Mkoa wa Kati,
- Mkoa wa Mashariki,
- Mkoa wa Kaskazini ya Mbali,
- Mkoa wa Pwani,
- Mkoa wa Kaskazini,
- Mkoa wa Kaskazini-Magharibi,
- Mkoa wa Magharibi,
- Mkoa wa Kusini, na
- Mkoa wa Kusini-Magharibi
Ona pia: Orodha ya miji ya Kamerun
Historia[hariri | hariri chanzo]
Historia ya awali[hariri | hariri chanzo]
Katika karne za BK Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi walianza uenezi wao kutoka huko kwenda kutawala maeneo mengi ya Afrika ya Kati, Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki.
Wakati wa ukoloni[hariri | hariri chanzo]
Kamerun ilikuwa koloni la Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya Ujerumani kushindwa vita, nchi ikagawiwa kati ya Uingereza na Ufaransa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kama eneo la kudhaminiwa.
Tangu uhuru hadi leo[hariri | hariri chanzo]
Mwaka wa 1960, Wafaransa waliacha Kamerun ikawa nchi huru. Wananchi wa Kamerun ya Kiingereza walipiga kura kuamua kama walitaka kuwa sehemu ya Nigeria au ya Kamerun. Kaskazini wengi walipendelea kukaa Nigeria, hivyo maeneo hayo sasa ni sehemu ya Nigeria. Wananchi wengi wa kusini waliamua wajiunge na Kamerun[1]. Kwa kusudi la kuheshimu tofauti za kiutamaduni kulikuwa na katiba mpya kwenye mwaka 1961 Shirikisho la Jamhuri ya Kamerun.
Tangu 1972 muundo wa nchi ulibadilishwa kuacha mfumo wa shirikisho na kuwa jamhuri ya muungano inayokazia zaidi matumizi ya lugha ya Kifaransa ingawa Kiingereza bado ni moja ya lugha rasmi. Jina la nchi pia likabadilishwa kuwa Jamhuri ya Muungano ya Kamerun mwaka wa 1972. Hapo sehemu ya Wakamerun wanaotumia lugha ya Kiingereza walijisikia kuwa wananyimwa haki zao.[2] Baadaye, mwaka wa 1984 jina likabadilishwa tena kuwa Jamhuri ya Kamerun (kwa Kifaransa République du Cameroun).
Tangu mwaka 2016 upinzani uliongezeka kati ya watu wa magharibi wanaotumia Kiingereza. Harakati hiyo ilijibiwa na serikali na polisi kwa ukali na hii umeleta kuanzishwa kwa wanamgambo wenye silaha wanaoshambulia polisi na jeshi la serikali kuu. Tangu mwaka 2017 wapinzani wamedai uhuru wa sehemu yenye lugha ya Kiingereza wakitangaza wameunda nchi mpya ya "Ambazonia". Serikali iliundwa inayokaa Nigeria; lakini kuna vikundi tofauti ambavyo wanapigana kati yao[3]. Nchi hii haitambuliwi kimataifa. Mwaka 2021 kulikuwa na majadiliano kuhusu amani kati kundi linalojiita serikali ya Ambazonia na serikali ya Kamerun[4], lakini makundi mengine yaliendelea na mapigano ya silaha[5].
Siasa[hariri | hariri chanzo]

Uchumi[hariri | hariri chanzo]
Watu[hariri | hariri chanzo]
Wakazi walikuwa 22,534,532 mwaka 2013, ambao wamegawanyika sawasawa kati ya wanaoishi mijini na wale wa vijijini.
Lugha rasmi ni Kifaransa pamoja na Kiingereza. Hata hivyo wakazi wanaongea pia lugha za makabila yao mengi.
Upande wa dini, 70% ni Wakristo (40% Wakatoliki na 30% Waprotestanti), 18% ni Waislamu, 3% ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika. 6% hawana dini yoyote.
Utamaduni[hariri | hariri chanzo]



Elimu[hariri | hariri chanzo]
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
- Ukristo nchini Kamerun
- Kanisa Katoliki nchini Kamerun
- Uislamu nchini Kamerun
- Mawasiliano nchini Kamerun
- Mambo ya kigeni ya Kamerun
- Orodha ya miji ya Kamerun
- Jeshi la Kamerun
- Usafirishaji nchini Kamerun
- Chama cha Wanaskauti Kamerun
- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
- ↑ 1961 British Cameroons Plebiscite, kwenye tovuti ya africanelections.tripod.com/referenda, iliangaliwa Januari 2019
- ↑ Anglophone crisis: Cameroon must return to federal system abolished under Ahidjo, Abdur Rahman Alfa Shaban kwenye tovuti ya africanews.com tar. 11/03/2018
- ↑ Ahead of peace talks, a who’s who of Cameroon’s separatist movements, tovuti ya The New Humanitarian tar. 8 July 2020
- ↑ Cameroon's separatist leader is willing to talk peace, but only with UN backing, Tovuti ya Deutsche Welle ya 23.03.2020
- ↑ Cameroon Events of 2020, tovuti ya Human Rights Watch, taarifa kuhusu Kamerun mwaka 2021
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
Serikali
- Urais wa Nchi ya Kamerun Tovuti rasmi ya serikali
- Bunge ya Kamerun Archived 14 Machi 2008 at the Wayback Machine. Tovuti rasmi
Habari
- allAfrica - Cameroon viungo via habari
- CRTV - Cameroon Radio Television ya serikali
- The Post – Gazeti lenye sifa linalochapwa huko Buea
- (Kifaransa) Le Messager Archived 30 Desemba 2005 at the Wayback Machine. Gazeti la binafsi
- (Kifaransa) (Kiingereza)Radio Siantou Archived 11 Aprili 2006 at the Wayback Machine.
Elimu
Uchambuzi
- (Kiingereza)BBC News - Country Profile: Cameroon
- (Kiingereza) (Kitabu cha wadadisi wam marekani) - Cameroon Archived 14 Oktoba 2002 at the Wayback Machine.
Makabila na koo
- Baka Pygmies of Cameroon Utamaduni na miziki ya watu wa Kamerun
- Anthropological researches in Cameroon Fieldwork among Cameroonian populations
- Bamileke, watu wa Kamerun
- Bakweri, watu wa Kamerun ya Kiingereza. Archived 30 Aprili 2006 at the Wayback Machine.
Miongozo
- CMCLICK Online! Cameroon Portal - Cameroon Archived 17 Mei 2021 at the Wayback Machine. Cameroon Internet Community. Cameroon Business Directory. Cameroon Information. Cameroon Culture.
- Open Directory Project - Cameroon Archived 23 Aprili 2006 at the Wayback Machine. directory category
- Stanford University - Africa South of the Sahara: Cameroon Maelezo kuhusu Afrika, kusini kwa Sahara.
- University of Pennsylvania - African Studies Center: Cameroon directory category
- Yahoo! - Cameroon Archived 4 Aprili 2006 at the Wayback Machine. uelekezo, kamerun
Utalii
- Cameroon tourism Picha kuhusu utalii kamerun
- Cameroon In Colour Archived 9 Mei 2021 at the Wayback Machine. Picha za Kamerun
Nchi za Afrika | ![]() |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kamerun kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |