Santiago Bernabéu Stadium

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
adrid Santiago Bernabéu Stadium
Santiago Bernabéu Stadium.

Uwanja wa Santiago Bernabéu (kwa Kihispania: Estadio Santiago Bernabéu) ni uwanja wa mpira wa miguu uliopo Madrid, Hispania.

Umekuwa uwanja wa nyumbani wa Real Madrid tangu kukamilika kwake mnamo 1947.

Kwa sasa uwanja una uwezo wa kuchukua watazamaji 89,044. Ni uwanja wa 2 kwa ukubwa nchini na mkubwa zaidi katika Jumuiya ya Madrid.

Santiago Bernabéu ni kimoja kati ya viwanja maarufu duniani. Imeshuhudia fainali za Ligi la Mabingwa Ulaya mara nne: mnamo mwaka 1957, 1969, 1980 na 2010 na ilisimamia mzunguko wa pili wa fainali za Copa Libertadores. M

echi za fainali za UEFA UERO za mwaka 1964 na Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 1982 pia zilifanyika Santiago Bernabéu, ikaufanya uwanja huu kuwa uwanja wa kwanza Ulaya kusimamia Ligi la Mabingwa Ulaya, Fainali za Kombe la Dunia la FIFA na Fainali za Copa Libertadores.

Football.svg Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Santiago Bernabéu Stadium kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.