Ligi la Mabingwa Ulaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Timu ya Real Madrid washindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2018

Ligi la Mabingwa Ulaya ni mashindano ya mpira wa miguu yaliyoanzishwa na UEFA na timu zinazoshiriki ni za Ligi kuu ZA Ulaya ili kupata bora Ulaya nzima.

Ilianzishwa 1955 kama Kombe la Ulaya awali mashindano haya yalikuwa na hatua ya mtoano tu,Mashindano haya yalipewa hili jina 1992,waliongeza hatua ya makundi na kuruhusu washiriki kutoka nchi kadhaa.Sasa baadhi ya nchi za Ulaya ni bingwa tu ndiye anayeshiriki lakini ligi kubwa washiriki wanaweza wakawa watano. Klabu ambayo itamaliza ya pili katika ligi la nchi yake zitachaguliwa kwenye Ligi la Europa la UEFA (Kwanzia 2021, Ligi Kuu ya Mabingwa Ulaya itaanzisha mashindano ya tatu yaitwayo Ligi la Europa la UEFA la pili,ambayo yatakuwa na timu ambazo hazijafuzu Ligi la Europa la UEFA).

Mwaka 2019 Ligi la Mabingwa Ulaya litaanza mwezi Juni, Timu thelathini na mbili zitagawanywa kwenye makundi nane.Washindi nane wa kila kundi na wa pili wa kila kundi zitaendelea hatua ya mtoano na fainali itachezeka Mei mwishoni au Juni mwanzoni. Mshindi atakuwa amefuvu kwenye Ligi la Mabingwa Ulaya la mwaka ujao,Kombe la Super la UEFA na Kombe la Dunia la Klabu la FIFA.

Mashindano haya yameshindwa na klabu ishirini na mbili,Kumi na mbili zimeshinda zaidi ya mara moja.Real Madrid ni klabu yenye mafanikio makubwa katika historia mashindano haya imeshinda mara kumi na tatu.Liverpool F.C. ni mabingwa wa sasa,baada ya kuifunga Tottenham Hotspurs F.C. 2–0 fainali ya 2019. Klabu za Hispania ndizo zinazoongoza zikiwa zimeshinda mara kumi na nane, zikifuatiwa na za Uingereza zimeshinda mara kumi na tatu na za Italia.

Sports icon.png Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Ligi la Mabingwa Ulaya kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.