Nenda kwa yaliyomo

Tottenham Hotspur F.C.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wachezaji wa timu ya Tottenham katika mechi dhidi ya manchester united akiwemo Harry Kane, Dele Alli, Son Heung-min, Christian Eriksen, Victor Wanyama, na Jan Vertonghen
Uwanja wa Tottenham

Tottenham Hotspur F.C. ni klabu ya mpira wa miguu nchini Uingereza iliyopo Tottenham, London na inashiriki Ligi Kuu Uingereza (EPL).[1][2]

Uwanja wa Tottenham Hotspur umekuwa uwanja wa klabu tangu aprili 2019, baada ya kubadilisha uwanja wao wa zamani White Hart Lane,ambao waliubomoa ili wajenge uwanja mwingine.Uwanja wa mazoezi upo kwenye njia ya Hotspur.[3]

Tottenham Hotspur F.C. iliundwa 1882 na ilishinda Kombe la F.A. kwa mara ya kwanza mwaka 1901.Tottenham Hotspur F.C. ilikuwa ni klabu ya kwanza kwenye karne ya ishirini kushinda katika ligi kuu na kombe la F.A. msimu wa 1960–1961.[4][5]

Baada ya kufanikiwa kutetea Kombe la FA mwaka 1962 mwaka 1963 ilikuwa klabu ya kwanza ya Uingereza kushinda mashindano ya klabu ya UEFA. Walikuwa pia washindi wa uzinduzi wa Kombe la UEFA mwaka 1972 na kuwa klabu ya kwanza ya Uingereza kushinda vikombe viwili tofauti vya Ulaya katika kipindi hicho. [6][7]

Spurs imeshinda mataji mawili ya ligi, vikombe nane vya FA, Vikombe vinne vya Ligi na vikombe saba vya ngao ya hisani ya FA. Katika soka la Ulaya wameshinda kombe la Ulaya moja na vikombe viwili vya UEFA. Tottenham pia wamekua washindani wa ligi ya mabingwa ya UEFA tangu mwaka 2018-19. Tottenham inamilikiwa na kampuni ya ENIC Group ambayo ilinunua klabu hiyo mnamo mwaka 2001. Klabu inakadiriwa kuwa na thamani ya £ bilioni 1.67 (dola bilioni 2.3) mwaka 2021 na ilikuwa klabu ya tisa ya soka duniani, na mapato ya kila mwaka ya £ milioni 390.9 mwaka 2020. Mnamo mwaka 2022 imekuwa klabu ya kumi duniani kwa kukusanya mapato ya kila mwaka ya £ milioni 406.2.[8][9]

  1. Wells, John C. (2008), Longman Pronunciation Dictionary (tol. la 3rd), Longman, ISBN 9781405881180, iliwekwa mnamo 30 Juni 2018{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Jones, Daniel; Roach, Peter (2011), Cambridge English Pronouncing Dictionary (tol. la 18th), Cambridge: Cambridge University Press, ISBN 9780521152532, iliwekwa mnamo 30 Juni 2018{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Tottenham legend Nicholson dies", BBC Sport, 23 October 2004. 
  4. Delaney, Miguel. "Christian Eriksen says Tottenham are determined to end their nine-year silverware drought", 11 March 2017. 
  5. "Manchester United football club honours". 11v11.com. AFS Enterprises. Iliwekwa mnamo 3 Julai 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Delaney, Miguel. "Christian Eriksen says Tottenham are determined to end their nine-year silverware drought", 11 March 2017. 
  7. "Manchester United football club honours". 11v11.com. AFS Enterprises. Iliwekwa mnamo 3 Julai 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "The Business of Soccer - Full List". Forbes. Iliwekwa mnamo 2 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Deloitte Football Money League 2021". Deloitte. 26 Januari 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Tottenham Hotspur F.C. kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.