Manchester United F.C.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Manchester United F.C.
Jezi za Manchester United
Rangi nyumbani
Rangi za safari

Manchester United ni kilabu cha kandanda cha Uingereza, ambacho ni kimojawapo kati ya vilabu maarufu sana ulimwenguni, na kina makao katika Old Trafford eneo la Greater Manchester. Kilabu hiki kilikuwa mwanachama mwanzilishi wa Ligi ya Premier mwaka 1992, na kimeshiriki katika divisheni ya juu ya kandanda ya Uingereza tangu mwaka wa 1938, isipokuwa msimu wa 1974-1975. Mahudhurio ya wastani kwenye kilabu yamekuwa ya juu kuliko timu nyingine yoyote katika kandanda ya Uingereza kwa misimu yote isipokuwa sita tangu 1964-65.[1]

Manchester United ndiyo bingwa wa sasa wa Uingereza na washikilizi wa Kombe la Dunia la Vilabu, baada ya kushinda Ligi ya Primia 2008-09 na Kombe la Dunia la FIFA. Kilabu hicho ni miongoni mwa vilabu vyenye ufanisi mkubwa katika historia ya kandanda ya Uingereza na kimeshinda mataji makubwa 22 tangu Alex Ferguson alipochukua wadhifa wa meneja wake mnamo Novemba 1986. Mwaka wa 1968, kilikuwa kilabu cha kwanza kushinda Kombe la Uropa kwa kucharaza Benfica 4-1. Walishinda kombe la pili la Ulaya kama sehemu ya ushindi wa mataji matatu mwaka 1999, na la tatu mwaka wa 2008, kabla ya kumaliza katika nafasi ya pili mwaka wa cha 2009. Kilabu hicho kinashikilia rekodi mbili ya kushinda mataji mengi ya Ligi ya Uingereza mara 18 na pia kushikilia rekodi kwa wingi wa kutwaa kombe la FA ikiwa imeshinda mara 11.[2]

Tangu mwisho wa mwaka ya 1990, kilabu hicho kimekuwa mojawapo ya vilabu tajiri duniani kilicho na mapato ya juu kuliko kilabu chochote,[3] na sasa kinatajwa kama kilabu chenye thamani zaidi katika mchezo wowote, na makisio ya thamana ya takriban bilioni £ 1.136 (bilioni € 1.319 ) Aprili 2009.[4] Manchester United ilikuwa mwanachama mwanzilishi wa kundi la vilabu la G-14 la Vilabu kuu vya kandanda Uingereza, ambalo halipo tena, na European Club Association, muungano uliochukua nafasi yake.[5]

Alex Ferguson amekuwa meneja wa kilabu hicho tangu 6 Novemba 1986 alipojiunga na kilabu hicho kutoka Aberdeen baada ya kung'atuka kwa Ron Atkinson.[6] Nahodha wa kilabu wa sasa ni Garry Neville, aliyechukua nafasi ya Roy Keane Novemba 2005.[7]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya mwanzo (1878–1945)[hariri | hariri chanzo]

Chati inayoonyesha maendeleo ya Manchester United F.C katika mfumo wa ligi ya kandanda Uingereza tangu kujiunga kama Newton Heath mwaka 1892-93 kwa sasa

Kilabu kilianzishwa kikijulikana kama Newton Heath L & YR F.C. mwaka wa 1878 kama timu ya kazi ya bohari la Reli la Lancashire na Yorkshire huko Newton Heath. Mashati ya kilabu hiyo yalikuwa ya kijani na nusu dhahabu. Walicheza kwenye uwanja mdogo, uliochakaa huko North Road kwa miaka kumi na mitano, kabla ya kuhamia Bank Street katika mji wa karibu wa Clayton mwaka wa 1893. Kilabu kilikuwa kimeingia ligi ya kandanda ya Football Leagu mwaka uliotangulia na kuanza kukatiza uhusiano wake na bohari la reli, na ikawa kampuni ya kujitegemea, ikimteua katibu wa kilabu na kudondoasha herufi “L&YR” kutoka jina lao na kujiita Newton Heath F.C. Muda mrefu haukupita, mwaka 1902, kilabu kilikaribia kufilisika, kikawa na madeni ya zaidi ya £2,500. Wakati mmoja, uwanja wao wa Bank Street ulifungwa na wadai wao.[8]

Kabla ya kufungwa kabisa, kilabu kilipokea uwekezaji mkubwa kutoka kwa J. H. Davies, mkurugenzi mtendaji wa Manchester Breweries.[9] Kuna tetesi kuwa Harry Stafford, nahodha wa kilabu alikuwa akijivunia mbwa wake wa thamani wa aina ya St. Bernard katika mkutano wa kuchangishia kilabu fedha, wakati Davies alipomwendea ili kumnunua mbwa huyo. Stafford alikataa, lakini aliweza kumshawishi Davies kuwekeza katika kilabu na kuwa mwenyekiti wake.[10] Iliamuliwa katika kikao cha bodi ya mapema kuwa kilabu kilihitaji kubadilishwa jina ili kuashiria mwanzo huo mpya. Manchester Central na Manchester Celtic ni miongoni mwa majina yaliopendekezwa kabla ya Louis Rocca, mhamiaji mchanga kutoka Italy aliposema "Ndugu zangu, mbona tusijiite Manchester united?"[11] Jina hilo lilibakia hivyo, na Manchester United likawa jina rasmi tarehe 26 Aprili 1902. Davies pia aliamua itakuwa vyema kubadili rangi za kilabu, walitupilia mbalirangi za kijani na nusu dhahabu za Newton Health na kuchagua nyekundu na nyeupe kuwa rangi za Manchester United.

Ernest Mangnall aliteuliwa kama katibu wa kilabu baada ya James West ambaye alikuwa amejiizulu kama meneja tarehe 28 Septemba 1902. Mangnall alitwikwa jukumu la kujitahidi kukifika kilabu kwenye Divisheni ya kwanza, na kushindwa kidogo tu katika jaribio la kwanza kusudio hilo kwa jaribuio la, walipomaliza katika nafasi ya tano katika Divisheni ya pili. Mangnall aliamua kwamba ilikuwa muhimu kuleta machipukizi katika klabu, na kuwasajili wachezaji kama vile Harry Moger katika lango, Dick Duckworth, beki wa nyuma na Jack Picken mbele lakini ilikuwa na beki wa nyuma mwingine kwa jina la Charlie Roberts aliyeleta mabadiliko makubwa. Alinunuliwa kwa £750 kutoka Grimsby Town Aprili 1904, na kuisaidi klabu kumaliza msimu wa 1903-04 kikiwa kimekosa alama moja tu kipandishwe ngazi iliyofuata.

Hata hivyo, haikuchukua muda mrefu, kilabu kilipandishwa cheo hadi Divisheni ya Kwanza kwa mara ya kwanza chini ya jina mpya na kumaliza katika nafasi ya pili katika Divisheni ya Pili mwaka wa 1905-06. Msimu wa kujiiimarisha ulifuatia, huku kilabu ikimaliza katika nafasi ya nane, kabla ya kutwaa taji lao la kwanza la ligi mwaka wa 1908. Katika siku za karibuni,Manchester City ilikuwa ikichunguzwa kwa kuwalipa baadhi ya wachezaji wao mshahara uliozidi kiwango kilichopendekezwa na masharti ya FA. Walipigwa faini ya £250 na wachezaji wao kumi na wanane wakapigwa marufuku kuwachezea tena. United hawakusita kukabiliana na hali hiyo na kuwatwaa Billy Meredith (almaarufu Welsh Wizard) na Sandy Turnbull, miongoni mwa wengine. Vijana hao wageni kutoka mji jirani hawakuruhusiwa kucheza hadi tarehe mosi mwaka wa 1907, kwa sababu ya marufuku yao, kwa hivyo hatua hiyo iliahirishwa hadi msimu wa 1907-08 ili waweze kuendeleza jitihada za united kutwaa taji. Na hilo walifanya, walianza kampeni yao kwa kishindo kwa kuishinda Sheffield United 2-1 na kuanzisha msururu wa ushindi mfululilizo mara kumi. Licha ya msimu kuonekana wenye tatizo mwishoni, United ilifaulu kushikilia na kumaliza msimu kwa pointi tisa mbele ya wapinzani wao wa karibu Aston Villa.

Msimu uliofuatia ulianza kwa United kujitwalia fedha nyingine, Charity Shield,[12] ambayo ilikuwa ya kwanza kuwahi kutolewa na kumalizia kwa taji jingine, taji la kwanza kwa kilabu cha FA, ambalo lilipanda mbegu njema ya kile kimekuwa rekodi ya mataji ya FA. Jinsi walivyokuwa katika kampeni ya taji la kwanza la klabu, Turnbull na Meredith walikuwa na umuhimu katika msimu huu, Turnbull akifunga bao la ushindi katika Finali ya kombe la FA. Ilibidi Klabu kusubiri miaka mingine miwili kabla ya kushinda makombe mengine zaidi, kilishinda Divisheni ya Kwanza kwa mara ya pili katika msimu wa 1910-11. Wakati huo huo, United ilihamia uga wao mpy wa Old Trafford. Walichezea mmchuano wao wa kwanza huko tarehe 19 Februari 1910 dhidi ya Liverpool, lakini wakapoteza 4-3 baada ya kupoteza ushindi wao wa 3-0. Kisha wakasalia bila kombe tena katika msimu wa 1911-12, ambao haukuwa tu wa mwisho kwa Mangnall kuhusikia (alihamia Manchester City baada ya miaka kumi na United), lakini pia wakati wa mwisho kwa klabu kushinda Divisheni ya Kwanza baada ya miaka 41, muda mrefu zaidi ambao klabu imekaa bila kushinda ligi katika historia yake.

Kwa miaka kumi iliyofuata, klabu kilishuhudia hali ya kudidimia polepole kabla ya kushushwa ngazi ya chini, Division ya pili katika 1922. Walipandishwa ngazi tena mwaka 1925, wakang'ang'ana kufika nusu ya msimamo wa ligi, na wakashushwa ngazi tena mwaka wa 1931. Katika miaka minane iliyotangulia Vita vya Pili vya Dunia, klabu kilididimia na kuwa klabu yo-yo, kikafikia kiwango chao cha chini zaidi cha nafasi ya 20 katika Divisheni ya Pili mwaka wa 1934. Walipandishwa tena katika msimu wa mwisho kabla ya Vita vya Pili vya Dunia. Walijihakikishia nafasi yao katika kiwango cha juu baada ya vita kwa kumaliza katika nafasi ya 14 katika msimu wa 1938-39.

Kipindi cha Busby (1945-1969)[hariri | hariri chanzo]

1945 ilishuhudia kuteuliwa kwa Matt Busby kuwa msimamizi katika Old Trafford. Alitumia mtindo usio wa kawaida kufanya kazi yake, akisisitiza kuwa aruhusiwe kuchagua timu yake mwenyewe, kuchagua wachezaji atakaowaajiri na kuwafunza mwenyewe. Mwenyewe alikuwa tayari amepoteza kazi ya usimamizi kwenye kilabu chake cha awali, Liverpool, kwa sababu klabu kiliona kazi hizo kama za wakurugenzi lakini United ikaamua kujaribu mawazo bunifu ya Busby. Wa kwanza kusajiliwa na Busby hakuwa mchezaji, bali meneja msaidizi mpya kwa jina la Jimmy Murphy. Hatua hatari ambayo klabu ilichukulia kumteua Bushy ilileta mazao ya mara moja, klabu kilipomaliza katika nafasi ya pili katika ligi ya 1947, 1483 na 1949 na kushinda kombe la FA 1948, kutokana na juhudi za wazao wa hapo watatu, Stan Pearson, Jack Rowley na Charlie Mitten (Rowley na Pearson walifunga katika fainali ya kombe la 1948), na pia kiungo wa kati kutoka Kazini Mashariki, Allenby Chilton.

Charlie Mitten alikuwa amekimbilia Kolombia kutafuta mshahara bora,lakini wachezaji waliobaki waliweza kushinda taji la Divisheni ya Kwanza baadaye mwaka 1952. Hata hivyo, Busby alijua kwamba timu za kandanda zilihitaji zaidi ya tajriba, kwa hivyo alitumia sera ya kuleta wachezaji kutoka katika timu ya vijana pale ilipowezekana. Mara ya kwanza, wachezaji wachanga kama vile Roger Byrne, Bill Foulkes, Mark Jones na Dennis Viollet, walichukua muda kuzoea timu kuu, na kuteremka hadi nafasi ya nane mwaka 1956, lakini timu hiyo ilishinda ligi tena katika mwaka wa 1956 kwa umri wa wastani miaka 22 tu, na kufunga mabao 103 wakati huo. Sera ya kuteua vijana iliyowekwa na Busby sasa imekuwa fadhila mahususi kwa vipindi vilivyofanikiwa zaidi katika historia ya klabu (katikati ya 1950, kati na mwisho wa miaka ya 1960 na miak 1990). Kundi asilia la vijana wachezaji lilijulikana kama Busby Babes, ambapo aliyevuma sana alikuwa kiungo wa pembeni Duncan Edwards. Kijana huyo kutoka Dudley, West Midlands aliichezea United kwa mara ya kwanza kabisa akiwa na umri wa miaka 16 tu mwaka 1953. Ilisemekana kuwa Edwards angeweza kucheza katika nafasi yoyote uwanjani, na wengi waliomwona akicheza walisema kuwa yeye ndiye alikuwa mchezaji maarufu kabisa katika historia ya mchezo huo. Msimu uliofuata, 1956-57, walishinda ligi tena na kufikia fainali ya Kombe la FA, na kupoteza kwa Aston Villa. Pia ilikuwa timu ya kwanza ya Uingereza kushindana katika kombe la Uropa, kwa amri ya FA, ambayo ilikuwa imeiinyima Chelsea fursa sawa na hiyo msimu uliotangulia, na kufika nusu fainali kabla ya kung'olewa na Real Madrid. Ikielekea nusu fainali hizo, United pia iliacha rekodi kwa ushindi ambayo bado ipo kama washindi wakuu katika mashindano yote, kwa kuwachapa mabingwa wa Ubelgiji Anderlecht mabao 10-0 ugani Maine Road.

Bamba la taarifa Old Trafford kwa heshima ya wachezaji walikufa katika ajali ya ndege ya Munich.

Janga liliikumba msimu uliofuata, wakati ndege iliyokuwa imewabeba wachezaji kurejea nyumbani kutoka mchuano wa European Cup ilipoanguka pindi ilipoanza kupaa baada ya kutua kujaza mafuta huko Munich, Ujerumani. Ajali hiyo ya ndege Munich ya 6 Februari 1958 ilisababisha vifo vya wachezaji - Geoff Bent, Roger Byrne, Eddie Colman, Duncan Edwards, Marko Jones, Daudi Pegg, Tommy Taylor na Liam "Billy" Whelan - na abiria wengine kumi na watano, pamoja na wafanyikazi wa United Walter Crickmer, Bert Whalley na Tom Curry.[13] Tayari kulikuwa na majaribio mawili ya kupaa kabla hilo la tatu lililoishia maafa, lilisababishwa na kujazana kwa tope mwishoni mwa barabara ya ndege na hivyo kupunguza kasi ya ndege hadi kiwango kisichotosha kupaa. Ndege iliteleza nje ya mwishoni mwa barabara ya kupaa, kupitia uani na kuingia katika nyumba ambazo hazikuwa na watu watu. Mlindalango wa United Harry Gregg alifanikiwa kutozirai baada ya ajali, na kwa kuhofia kulipuka kwa ndege wakati wowote, aliwakamata Bobby Charlton-ambaye alikuwa ameichezea United mechi yake ya kwanza kabisa miezi 18 tu iliyopita – na Denni Viollet viunoni na kuwavuta mahali salama. Wachezaji 7 wa United walikufa katika eneo la tukio, huku Duncan Edwards akifa majuma mawili baadaye hospitalini. Wing'a wa kulia Johnny Berry pia alinusurika ajali hiyo, lakini majeraha aliyopata kwenye ajali yalisitisha ghafla uchezaji wa kandanda. Matt Busby hakutumainiwa kuishi zaidi na madaktari wa Munich na wakati mmoja alifanyiwa Maombi ya Mwisho, lakini alipata afueni kimiujiza na hatimaye aliruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kulazwa kwa zaidi ya miezi miwili.

Kulikuwa na uvumi kuwa klabu ingefilisika na kujiondoa kutoka mashindano yote, lakini Jimmy Murphy aliposhikilia usukani kama meneja huku Busby akiendelea kupona majeraha, klabu kiliendelea kucheza kwa timu hafifu. Licha ya ajali hiyo, walifika fainali ya kombe la FA tena, ambapo walipoteza dhidi ya Bolton Wanderers. Mwishoni mwa msimu, UEFA iliipa FA nafasi ya kuwasilisha United na mabingwa wa msimu Wolverhampton Wanderers, kushiriki kombe la Uropa mwaka 1958-59 kama heshima kwa waathiriwa lakini FA ilikataa. United ilimudu kuikaba Wolves koo msimu uliofuata, huku ikimaliza katika nafasi ya kuridhisha ya pili; haikuwa mbaya kwa timu iliyokuwa imepoteza wachezaji tisa katika ajali ya ndege ya Munich.

Busby aliijenga upya tena timu hiyo mapema miaka ya 1960, akisajili wachezaji kama vile Denis Law na Pat Crerand, wakati huo huo akilea kizazi chake kipya cha vijana chipukizi. Huenda maarufu zaidi katika kundi hili jipya alikuwa kijana kutoka Belfast aliyeitwa George Best. Best alikuwa na uanariadha wa kipekee , lakini kipawa chake cha thamani zaidi kilikuwa kudhibiti mpira. Miguu yake ya kasi ilimruhusu kupenya kwenye mwanya wowote katika ngome ya wapinzani, hata uwe mdogo kiasi gani. Timu hiyo ilitwaa Kombe la FA mwaka wa 1963, ingawa ilimaliza katika nafasi ya 19 katika Daraja la Kwanza. Shangwe za ushindi wa Kombe la FA zilionekana kuwaimarisha wachezaji, waliosaidia klabu kufikia nafasi ya pili 1964, na kuimarika zaidi kwa kushinda ligi katika mwaka wa 1965 na 1967. United ilishinda kombe la Uropa 1968 kwa kuinyuka Eusébio's Benfica 4-1 kwenye fainali na kuwa kilabu cha kwanza Uingereza kushinda shindano hilo. Timu hii ya United ilikuwa maarufu kwa kuwa na wanakandanda watatu bora wa Mwaka barani Uropa: Bobby Charlton, Denis Law na George Best. Matt Busby alijiuzulu kama meneja 1969 na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa akiba na pia aliyekuwa mchezaji wa United, Wilf McGuinness.

1969-1986[hariri | hariri chanzo]

United ilijitahidi kujaza nafasi ya Busby, na timu ilitatizika chini ya Wilf McGunness katika msimu wa 1969-70, ilipomaliza katika nafasi ya kukatisha tamaa ya nane, na kufuatiwa na kuanza vibaya katika msimu wa 1970-1971, McGunnies alishushwa madaraka na kuwa kocha wa timu ya akiba. Busby alishawishwa kurudi klabuni, japo kwa miezi sita pekee. Matokeo yalikuwa bora chini ya uongozi wa Busby, lakini hatimaye aliondoka klabuni kwa mara ya mwisho katika majira ya joto ya 1971. Hayo yakijiri, United ilikuwa imewapoteza wachezaji wa hali ya juu kama Nobby Stiles na Pat Crerand.

Licha ya kumwomba maneja aliyeiongoza Celtic kushinda kombe la Uropa Jock Stein, kuwa meneja wake, Stein alikubali kwa mkataba wa mazungumzo kujiunga na United, lakini akaghairi msimamo dakika za mwisho- Frank O’Farrell aliteuliwa kumrithi Busby. Hata hivyo, kama Mc Guinness, O’Farrell alidumu chini ya miezi 18, tofauti kati ya wawili hao ni kuwa O’Farrell aliitikia matokea ya timu yasiyo ya kuridhisha kwa kuleta vipaji vipya, wakutajika hasa ni Martini Buchaman kutoka Aberdeen kwa malipo ya £125,000. Tommy Docherty akawa meneja mwishoni mwa 1972. Docherty, au "Doc", aliiokoa United kutoshushwa ngazi msimu huo lakini walishushwa mwaka 1974, wakati ambapo nyota watatu , Best, Law na Charlton walikuwa wamekihama klabu. Denis Law alikuwa amehamia Manchester City katika majira ya joto ya 1973, na kuishia kufunga bao ambalo watu wengi husema liliishusha ngazi ya United, kwa adabu alikataa kusherehekea pamoja na wanatimu wenzake. Wachezaji kama vile Lou Macari, Stewart Houston na Brian Greenhoff waliletwa kuchukua nafasi za Best, Law na Charlton lakini hakuna aliyefikia kimo cha watatu hao waliotangulia.

Timu iliweza kupandishwa ngazi katika jaribio la kwanza, huku kijana Steve Coppell akishiriki mchuano wake wa kwanza kuelekea mwisho wa msimu baada ya kujiunga na klabu kutoka Tranmere Rovers na kufika fainali za Kombe la FA mwaka 1976, lakini walishindwa na Southampton. Walifika fainali tena mwaka 1977, walipoishinda Liverpool 2-1. Pamoja na mafanikio na umaarufu wake miongoni mwa mashabiki, Docherty alipigwa kalamu mara baada ya fainali ilipopatikana kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa mtaalamu wa tibamaungo (physiotherapist).

Dave Sexton alichukua nafasi ya Docherty kama meneja katika majira ya joto ya 1977 na kuifanya timu kucheza mtindo wa kujihami zaidi. Mtindo huu haukupendwa na mashabiki ambao walikuwa wamezoea mtindo wa kandanda ya kushambulia iliyopendelewa na Docherty na Busby. Usajili mkuu wa wachezaji uliofanyika chini ya Sexton ulihusisha Joe Jordan, Gordon McQueen, Gary Baileyna na Ray Wilkins lakini kwa sababu ya mtindo wa kujihamu wa Sexton, United ilishindwa kutoka katika safu ya kati isipokuwa mara moja tu, ilipomaliza katika nafasi ya timu mbili bora na ikaweza kufikia finali ya kombe la F.A mara moja, ilipoteza kwa timu ya Arsenal. Kwa sababu ya ukosefu huu wa vikombe, Sexton alifutwa mwaka wa 1981, ingawa alikuwa ameshinda michuano yake yote saba ya mwisho.

Nafasi yake ilichukuliwa na mshaufu Ron Atkinson ambaye fikra zake za ucheshi zilidhihirika katika vilabu alivyosimamia. Mara moja alivunja rekodi ya Uingereza ya ada ya uhamisho kwa kumsajili Bryan Robson kutoka klabu yake ya zamani, West Bromwich Albion. Robson aliibuka kuwa kile wengi[who?] walifikiria kuwa mchezaji bora kiungo cha kati wa United tangu Duncan Edwards. Timu ya Atkinson iliweza kushuhudia usajili mpya wa wachezaji kama vile Jesper Olsen, Paul McGrath na Gordon Strachan ambao walicheza na wliokuwa wachezaji wa timu ya vijana wakiwemo Norman Whiteside na Mark Hughes. United ilishinda Kombe la FA mara mbili katika miaka mitatu, katika mwaka wa 1983 na 1985, walipigiwa upatu kushinda Ligi katika msimu wa 1985-86 kabla ya kushinda mechi zao kumi za kwanza ligini jambo lililopelekea kuwepo na tofauti ya pointi kumi kati yao na wapinzani wao mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba. Hata hivyo, muundo wa timu uliporomoka na United ikamaliza msimu huo katika nafasi ya nne. Uhafifu wa timu uliendelea katika msimu uliofuata, na United ilikuwa ikichungulia kushushwa ngazi kuanzia mwanzo wa Novemba 1986, Atkinson alifutwa.

Enzi ya Alex Ferguson, kabla ya Treble [1986-1998][hariri | hariri chanzo]

Alex Ferguson amekuwa meneja wa Manchester United tangu Novemba 1986.

Alex Ferguson aliwasili kutoka Aberdeen kuchukua nafasi ya Atkinson siku hiyo hiyo aliyofutwa Atkinson, alikuja pamoja na meneja msaidizi wake, Archie Knox. Ingawa mechi yake ya kwanza uongozini, dhidi ya Oxford United tarehe 8 Novemba 1986 alishindwa 2-0, Ferguson aliiongoza klabu kumalizia nafasi ya 11 katika ligi. Kumaliza katika nafasi ya pili 1987-88, pamoja na Brian McClair kuwa mchezaji wa kwanza wa United tangu George Best na kufunga mabao ishirini katika msimu wa ligi, huenda kuliwafanya mashabiki kuwa na matumaini kidogo kwa siku za usoni lakini walirejelea haraka uhafifu kwa kumalizia nafasi ya 11 mwaka 1989.

Wachezaji wengi waliosajiliwa na Ferguson hawakufikia matarajio ya mashabiki, na meneja iliripotiwa nusura aachishwe kazi mwanzoni mwa 1990, wengi waliamini kwamba kushindwa kwao na Nottingham Forest katika duru ya tatu ya Kombe la FA kungetia muhuri hatma yake. Bao la Marko Robins kunako dakika 56 liliiwezesha United kushinda mchuano huo na kuwaweka katika king'ang'anyiro kilichowapeleka hadi fainali iliyofanyika Wembley, ambapo waliitinga Crystal Palace 1-0 katika mchuano wa marudio baada ya sare ya 3-3 katika mechi ya awali. Mwaka uliofuata, United ilifika fainali ya League Cup na kupoteza kwa bao 1-0 kwa timu ya aliyekuwa meneja wao Ron Atkinson Sheffield Wednesday. Hata hivyo, msimu ulimalizika kwa ushindi wa kwanza wa Kombe la Washindi wa Vilabu (Cup Winners 'Cup), walipoiadhibu Barcelona 2-1 katika fainali ugani Rotterdam. Ushindi wa taji la Cup Winners uliiruhusu timu kucheza katika UEFA Super Cup mwaka 1991 ambapo waaliwashinda waliokuwa washindi wa Kombe la Ulaya Red Star Belgrade 1-0 uwanjani Old Trafford. Mechi hiyo ilipaswa kuchezwa kwa michuano miwili lakini kutokana na ukosefu wa utulivu wa kisiasa nchini Yugoslavia wakati huo, UEFA iliamua kwamba mchuano wa Old Trafford tu ndio utakaochezwa. Kushiriki kwa mara ya pili mfululizo katika fainali ya kombe la Ligi kulitokea mwaka 1992, United wakati huo iliifunga Nottingham Forest 1-0 ugani Wembley.

Wakati huo huo, matukio yalikuwa yakiendelea nje ya uwanja mwishoni mwa mwongo, huku mwenyekiti Martin Edwards akijaribu kuiuza klabu kwa mkwasi Michael Knighton mwaka 1989. Uuzaji huo wa milioni £20 ulikuwa karibu kuthibitishwa huku Knighton akiingia Old Trafford akiwa na sare ya Manchester United na akifanya mbwembwe kadha kabla ya kuvurumisha mpira kuelekea langoni upande wa Stretford ugani humo. Knighton aliweza kuona rekodi za kifedha za klabu, lakini, kabla ya mkataba wa uuzaji kukamilishwa washauri wake wa kifedha walikataa na mpango huo ukafutiliwa. Hata hivyo, kwa kuwa Knighton alikuwa na ufahamu wa jinsi mambo yalivyokuwa yakiendeshwa klabuni, alipewa wadhifa katika bodi ya klabu kama njia ya kumfanya kubaki kimya kuhusu jambo hilo. Mwaka 1991, ikihitaji msaada zaidi wa kifedha kufuatia Ripoti ya Taylor klabu ilianza uuzaji katika Soko la Hisa la London kwa thamana iliyokisiwa kuwa paundi milioni 47, na kuleta katika macho ya umma hali yake ya kifedha. Martin Edwards alihifadhi wadhifa wake kama mwenyekiti, lakini sasa klabu ilikuwa ikimilikiwa na umma.

Majira ya joto ya mwaka 1991 pia yalishuhudia kuwasili kwa mlindalango raiya wa Denmak Peter Schmeichel, ambaye kutofungwa kwake katika michuano 17 kuliipa United rekodi bora ya kujihami katika Divisheni ya kwanza msimu wa 1991-92na kuwasaidia kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Leeds United, ndani ya safu hizo kulikuwa na sogora fulani Mfaransa aliyeitwa Eric Cantona. Alex Ferguson alitambua haja ya United ya kuwa na mshambulizi kama njia ya kumzuia Mark Hughes na Brian McClair na alijaribu - na kushindwa - mara kadhaa kumsajili mshambuliaji wa Sheffield Wednesday David Hirst, lakini wakati meneja wa Leeds Howard Wilkinson alipompigia Martin Edwards mwezi Novemba 1992 kuuliza kuhusu uwezekano wa kupatikana kwa Denis Irwin, mazungumzo hayo yaligeuka haraka na kumhusu Cantona. Kwa mshangao wa Edward na Ferguson, vilabu hivyo viwili viliweza kukubaliana kwa ada ya pauni milioni 1.2 ili kumpata Mfaransa huyo thabiti. Kuwasili kwa Cantona kuliipa United mwamko muhimu sana na kuisaidia timu hiyo kuweza kujishindia taji la kwanza la Ligi tangu mwaka wa 1967. Baada ya kusajiliwa kwa Roy Keane kutoka Nottngham Forest mnamo mwaka wa Julai 1993, United iliweza kushinda taji la pili mtawalia kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1957 kwenye mwaka uliofuata, kabla ya kushinda kombe la FA ili kukamilisha "Ushindi pacha" wa kwanza katika historia ya Kilabu hiyo. Mwaka huo, hata hivyo, klabu kiliomboleza kufuatia kifo cha aliyekuwa meneja na mkurugenzi wa klabu Matt Busby, aliyekufa tarehe 20 Januari 1994.

Msimu wa 1994-95 ulikuwa wa kwanza kwa klabu kumaliza bila kombe tangu 1988-89, ingawa walicheza vizuri hadi katika wiki ya mwisho wa msimu na kufikiwa fainali ya FA Cup, ambapo walipoteza kwa Everton. Andy Cole alisajiliwa kutoka Newcastle United kwa gharama iliyoweka rekodi Uingereza ya paundi milioni £6 pamoja na Keith Gillespie. Hata hivyo, baada mchuanio wa kwanza wa Cole akiwa United, Eric Cantona alipokea marufuku ya miezi nane kwa kuruka ndani ya eneo umati na kumuumiza Mathayo Simmons shabiki wa Crystal Palace, ambaye alikuwa amemdhihaki Cantona kutokana na rangi ya ngozi yake akiondoka uwanjani wakati wa mchuano wa United ugani Selhurst Park. Kusimamishwa kwa Cantona kulitolewa na baadhi kama sababu ya United kushindwa kukamilisha kwa mataji matatu "hat-trick" msimu huo. Kutofanikiwa kama ilivyotarajiwa msimu huo kulimsababisha Ferguson kufanya marekebisho makuu katika timu aliwauza Paul Ince, Andrei Kanchelskis na Mark Hughes na kujaza nafasi zaoo kwa wachezaji kutoka katika timu ya vijana wa klabu hiyo, akiwemo David Beckham, Gary Neville, Phil Neville na Paul Scholes. Baada ya kushindwa 3-1 na Aston Villa katika siku ya ufunguzi wa msimu 1995-96, mwanahabari wa televisheni maarufu Alan Hansen alitoa kauli maarufu kwa kusema "kamwe hamtashinda chochote mkiwa na watoto."[14] Wachezaji kadhaa wapya, ambao baadhi yao kwa haraka walijumuishwa katika michuano ya kimataifa ya mara kwa mara na timu ya Uingereza, waliitikia vizuri na kutokana na motisha ya kurejea kwa Cantona Oktoba 1995, United ikawa klabu ya kwanza ya Uingereza kuwahi kushinda mataji mawili mara mbili, ufanisi uliokuja kujulikana kama "Double Double".[15]

Nahodha Steve Bruce aliondoka kuelekea Birmingham City mwezi Julai 1996, na Alex Ferguson akamtaja Eric Cantona kama nahodha mpya wa klabu. Aliiongoza timu kutwaa taji la nne la ligi kati ya miaka mitano katika 1996-97 kabla ya kustaafu kutoka kandanda akiwa na umri wa 30 ilipofika mwisho wa msimu huo. Teddy Sheringham aliletwa kuchukua nafasi yake, na shati yake tambulika nambari 7 ikakabidhiwa David Beckham. Walianza msimu wa 1997-98 vizuri, lakini wakapoteza michuano mitano baada ya Krismasi na kumaliza katika nafasi ya pili, pointi moja nyuma ya washindi mara mbili Arsenal. Baada ya kipindi bila mshindani wa kila mara kuwania taji ligi, hii ilikuwa dhibitisho ya kuwasili kwa Arsenal kama mshindani halisi ambao wangegombea katika miaka michache iliyofuata.

Ushindi mara tatu, Treble (1998–99)[hariri | hariri chanzo]

Mataji ya Utatu - ya Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA (kushoto kuelekea kulia)

Msimu wa 1998-99 kwa Manchester United ulikuwa na mafanikio sana katika historia ya vilabu vya kandanda nchini Uingereza kwani walikuwa timu ya pekee ya Uingereza iliyowahi kushinda mataji matatu - Ligi Kuu (Premier), kombe la FA na taji la mabingwa UEFA Champions Leaguae katika msimu huo.[16] Baada ya msimu wa wasiwasi wa Ligi ya Premier, Manchester United ilitwaa taji hilo kwenye siku ya mwisho ya fainali kwa kuwashinda Tottenham Hotspur mabao 2-1, huku Arsenal ikiishinda Aston Villa bao 1-0.[17] Kutwaa taji la Ligi ya Premier kulikuwa sehemu ya kwanza ya ushindi mara tatu (treble), sehemu moja ambayo meneja Alex Ferguson aliieleza kuwa ngumu zaidi.[17] Katika Fainali ya kombe la FA United ilikabiliana na Newcastle United na kushinda 2-0 kwa mabao kutoka kwa Teddy Sheringham na Paul Scholes.[18] Katika mechi ya mwisho ya msimu wa 1999 walicheza UEFA Chapions League Final na kuishinda timu ya Bayern Munich katika kile kinafikiriwa kuwa mwamko mkuu sana kuwahi kushuhudiwa, mchuano ulikuwa umeingia muda wa ziada wakiwa wameshindwa kwa bao moja kabla ya kutoka nyuma na kufunga mara mbili na hivyo kushinda 2-1.[16] Ferguson baadaye alipongezwa kwa huduma zake katika kandanda na kutunukiwa heshima ya taifa inayompa ruhusa kuitwa "sir".[19] Kuhitimisha mwaka huo wa kuvunja rekodi, Manchester United ilishinda kombe la Intercontinental baada ya kuinyuka Palmeiras bao 1-0 mjini Tokyo.[20]

Baada ya kipindi cha ushindi Mara Tatu (1999-hadi sasa)[hariri | hariri chanzo]

United ilishinda ligi mwaka 2000 na 2001, lakini vyombo vya habari vikaona kana kwamba klabu kimeshindwa msimu huo kwa sababu kilishindwa kutwaa tena taji la Ulaya.[onesha uthibitisho] Mwaka 2000, Manchester United ilikuwa mojawapo ya timu 14 waanzilishi wa G-14, kundi la vilabu vya soka mashuhuri Ulaya.[21] Klabu hicho pia kilikataa kushiriki kombe la FA 1999-2000 na badala yake kushiriki katika mashindano ya uzinduzi wa taji la FIFA la Klabu Bingwa Duniani Brazil, kilitaja shinikizo kutoka kwa FA, UEFA na kamati ya Uingereza iliyokuwa ikishughulikia kombe la dunia la 2006. Ferguson aliweka mikakati ya kujihami ili kufanya iwe vigumu kwa United kushindwa Ulaya, lakini mikakati hiyo haikuwa na mafanikio kwani United ilikamilisha msimu wa Ligi Kuu ya 2001-02 katika nafasi ya tatu. Walitwaa tena ligi msimu uliofuata (2002-03) na kuanza msimu uliofuata vizuri, lakini hali yao ilishuka kwa kiasi kikubwa baada ya Rio Ferdinand kupokezwa marufuku tata ya miezi minane kwa kutohudhuria upimaji wa madawa ya kulevya. Walishinda kombe la FA 2004, hata hivyo, waliibandua nje Arsenal (hatimaye Arsenal ilishinda taji la Ligi Kuu msimu huo) wakiwa njiani kuelekea fainali ambako waliishinda Millwall.

Msimu wa 2004-2005 ulijawa na hali ya kutofunga mabao, hasa kutokana na jeraha la mshambulizi Ruud van Nistelrooy na United ikamaliza msimu huo bila taji lolote na katika nafasi ya tatu. Wakati huu, hata kombe la FA liliwaponyoka kwani Arsenal iliishinda United kwa mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare baada ya kucheza kwa dakika 120. Nje ya uwanja, hadithi kuu ilikuwa uwezekano wa klabu kuchukuliwa, tarehe 12 Mei 2005 na mfanyibiashara wa Kimarekani Malcom Glazer ambaye aliweza kupata udhibiti wa klabu hiyo kupitia uwekezaji kutumia kampuni yake ya Red Football Ltd. katika ununuzi uliothaminiwa kufikia kima cha takribani milioni £800 (wakati huo ikikisiwa kuwa sawa na dola bilioni 1.5).[22][23] Tarehe 16 Mei, aliziongeza hisa zake hadi 75% zinazohitajika kukiondoa klabu hicho kutoka Soko la Hisa na kukifanya kuwa binafsi tena, alitangaza nia yake kufanya hivyo katuka muda wa siku 20.[23] Tarehe 8 Juni, aliwateua wanawe katika bodi ya Manchester United kama wakurugenzi wasio watendaji.[24]

United ilianza vibaya msimu wa 2005-06, huku kiungo wa kati Roy Keane akiondoka kujiunga na Celtic baada ya kuwakosoa hadharani wachezaji wenzake kadhaa. Klabu pia ilikuwa imeshindwa kuhitimu kufuzu kwa awamu ya mwondoaano wa UEFA Champions League kwa zaidi ya mwongo mmoja, baada ya kupoteza kwa Benfica. Msimu huu pia walikumbwa na mikosi kadhaa ya majeraha kwa wachezaji wakuu kama vile Gabriel Heinze, Alan Smith, Ryan Giggs na Paul Scholes. Hata hivyo, walizuiliwa kuachwa mikono mitupu katika misimu mifululizo- masikitiko ambayo yalikuwa hayajashuhudiwa kwa miaka 17 iliyopita-kwa kushinda kombe la Ligi ya 2006, baada ya kuwalaza majirani zao waliopandishwa cheo Wigan Athletic katika fainali kwa mabao 4-0. United pia ilijihakikishia nafasi ya pili na kufuzu moja kwa moja kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa (Champions League) siku ya mwisho ya msimu kwa kuishinda Charlton Athletic 4-0. Mwishoni mwa msimu wa 2005-06, mmoja wa washambuliaji wa United, Ruud van Nistelrooy, alikihama klabu na kujiunga na Real Madrid, kutokana na ugomvi baina yake na Alex Ferguson.[25]

Mnamo Julai 2006, klabu kilitangaza mpango wa ufadhili mpya. Kiasi cha jumla kitakuwa £ milioni 660, ambayo italipiwa riba ya £ milioni 62 kwa mwaka.[26] Matokeo ya mpango huu mpya wa ufadhili utakuwa punguzo la asilimia 30 ya malipo ya kila mwaka.[27] Uwanjani, msimu wa 2006-07 ulishuhudia United ikirejea na mtindo wao wa kandanda ya kushambulia ambao ndio ulikuwa msingi wa miaka yao ya ufanisi mwishoni mwa miaka ya 1990, wakifunga takriban mabao 20 zaidi ya Chelsea waliokuwa katika nafasi ya pili baada ya michuano 32. Januari 2007, United ilimsajili Henrik Larsson kwa mkopo wa miezi miwili kutoka Helsingborg ya Uswidi, mshambuliaji alitekeleza jukumu muhimu sana katika kuisaidia United kuingia nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa,[28] huku ikiwa na matumaini ya kushinda mataji matatu kwa mara ya pili, hata hivyo, baada ya kufikia nusu fainali, United iliaibishwa na Milan kwa jumla ya mabao 3-5.[29] Miaka minne baada taji lao la mwisho, United ilishinda taji la Premier League tarehe 6 Mei 2007 baada ya Chelsea kutoka sare na Arsenal jambo lililoiacha The Blues pointi saba nyuma ikiwa imesaza michuano miwili ili kumaliza, kufuatia ushindi wa United wa 1-0 katika mchuano wa timu kutoka mji wa Manchester "Derby" siku iliyopita na kuifanya kombe lao la 9 la Ligi ya Premier katika misimu 15 ya uwepo wa ligi hiyo. Hata hivyo, ushindi pacha "Double" wa mara ya nne ambao haukutarajiwa haukutokea baada ya Chelsea kuifunga United 1-0 katika muda wa ziada katika kombe la kwanza la FA kufanyika katika uwanja mpya wa Wembley; wa kwanza kufanyika nchini Uingereza tangu uwanja wa zamani kubomolewe miaka saba iliyopita.

Kipindi cha kati ya 2007-08 kilishuhudia United ikimaliza kwa kushinda mataji mawili ya Ulaya licha ya kuanza vibaya msimu huo walipojipata katika nafasi 17 katika Ligi Kuu baada ya kushiriki katika mechi tatu. Hata hivyo, tarehe 11 Mei 2008, United ilihifadhi taji la Ligi ya Premier kufuatia ushindi dhidi ya Wigan Athletic. Huku washindani wao katika taji hilo Chelsea wakiweza tu kutoka sare na Bolton Wanderers, United iliweza kumaliza msimu kwa alama mbili mbele. Klabu pia ilifika fainali ya Kombe la Ulaya kwa mara ya tatu katika historia yake, baada ya kuvishinda vilabu kama Barcelona na Roma ili kufuzu kwa fainali. Waliifunga Chelsea katika mikwaju ya penalti 6-5 katika fainali ugani Luzhniki Moscow baada ya kutoka sare ya 1-1 katika muda wa kawaida tarehe 21 Mei 2008. Kupitia ushindi huu , walijipatia taji lao la tatu la Ulaya na kuweka rekodi yao kutowahi kupoteza fainali kubwa ya Ulaya. Kisadfa, msimu huu ulikuwa wa miaka 100 tangu Manchester United iliposhinda taji lao la kwanza la Ligi, ilikuwa miaka 50 baada ya ajali ya ndege ya Munich na miaka 40 baada ya Manchester United kuwa timu ya kwanza ya Uingereza kushinda taji la Ulaya. Fainali ya Kombe la Ulaya ilishuhudia pia Ryan Giggs akiichezea klabu hiyo kwa mara ya 759, na kumpita Bobby Charlton aliyekuwa akishikilia rekodi ya kuichezea mara nyingi zaidi klabu hicho.

Kabla ya kuanza kwa msimu wa 2008-09, United walishiriki na kushinda tuzo ya ngao yaFA Community Shield ya 2008. United walifunga Portsmouth katika mikwaju ya penalti 3-1, washindi wa Kikombe cha FA cha 2007-08, baada ya mechi kukamilika kwa sare tasa ya 0-0 ndani ya dakika 90. Mnamo tarehe 21 Desemba 2008, United waliongezea nishani zaidi kwenye hazina yao ya tuzo kwa kushinda katika fainali ya Kombe la Ulimwengu la Vilabu vya FIFA kwa kuishinda LDU Quito kutoka Ecuador kwa bao 1-0 kule Japan, Wayne Rooney ndiye aliyefunga bao la ushindi. Miezi miwili baadaye, waliliongezea kombe la Ligi ya 2009 katika hazina yao ya tuzo kwa kuishinda Tottenham Hotspur mabao 4-1 kwenye mikwaju ya penalti.[30] Mnamo tarehe 16 Mei, United waliweza kuwahi taji la 11 katika Ligi ya Primia - na taji la ujumla la 18 katika Ligi – baada ya kuenda sare tasa ya 0-0 nyumbani kwao wakicheza na Arsenal huku wakishinda mataji matatu mtawalia ya Ligi ya Premier kwa mara ya pili.[31] Mnamo tarehe 27 Mei 2009, Barcelona waliweza kuishinda Manchester United mabao 2-0 katika fainali ya Ligi Mabingwa kule Rome, yaliyofungwa na Samuel Eto'o na Lionel Messi.[32] Fainali ya Ligi ya Mabingwa ilitokea kuwa mechi ya mwisho kwa Carlos Tévez – ambaye mkataba wake ulikamilika mnamo tarehe 30 Juni – na Christiano Ronaldo – aliyeuzwa kwa Real Madrid kwa gharama ya milioni £80, kuvunja rekodi ya dunia ya kuhamisha na kusajiliwa kwa Kaka na Real Madrid kutoka Milan kwa gharama ya milioni £56. Hata hivyo, United waliitikia hasara hizo kwa kumhamisha na kumsajili Michael Owen bila gharama yoyote, Antonio Valencia kwa milioni £17 na Gabriel Obertan kwa gharama ya milioni £3.

Msimu wa 2009-10 ulianza vizuri kwa timu ya Manchester United, licha ya kushindwa 1-0 na timu ya Burnley kule Turf Moor iliyokuwa pigo kubwa kwao. Wingi wa ushindi ukafuata hatimaye, pamoja na ushindi wa kusisimua dhidi ya Manchester City kwa mabao 4-3, uliopatikana mnamo dakika ya 96 kutokana na bao lake Michael Owen. Hata hivyo, mchezo isioridhisha uliwafanya kushindwa mabao 2-0 na Liverpool uwanjani Antfield. Kufikia 1 Novemba, Manchester United ni ya pili katika ligi, alama 2 nyuma ya Chelsea. Katika Ligi ya Mabingwa, United kwa sasa ndio washindi wa kwanza kwenye kundi lao, pamoja na ushindi dhidi ya Beşiktaş na CSKA Moscow na ushindi dhidi ya Wolfsburg huko nyumbani kwao. Mnamo tarehe 3 Novemba, Manchester United waliweza kuhifadhi na kuhitimu kutoka katika kikundi kwa kupata mabao sare 3-3 dhidi ya CKSA Moscow.

Nembo na rangi za klabu[hariri | hariri chanzo]

Katika enzi zake kama Newton Heath, klabu kilitumia mavazi ya rangi tofauti, inayotambuliwa zaidi ni shati la rangi ya manjano na kijani lililovaliwa kuanzia 1878 hadi 1892, na tena 1894-1896; vazi hili la milia lilitumika tena katika michuano ya ugenini mapema miaka ya 1990. Mavazi mengine yaliyovaliwa na Newton Heath ni pamoja na shati jekundu lililokuwa na weupe robo yake (1892-1894) na shati jeupe lisilo kuwa na milia (1896-1902), zote hizi zilivaliwa na kaptura ya rangi ya samawati.[33] Katika mwaka wa 1902, pamoja na klabu kubadili jina na kuwa Manchester United, klabu pia kilibadili rangi zake kuwa jezi nyekundu, kaptura nyeupe na soksi nyeusi, ambayo imesalia kuwa sare wastani ya Man Utd katika michuano ya nyumbani tangu wakati huo. Kilicho tofauti na haya ni jezi ambazo timu ilivaa ikicheza fainali ya kombe la FA 1909 na Briston City ambayo ilikuwa nyeupe na mshipi mwekundu wa muundo wa “V”.[34] Mtindo huu ulifufuliwa katika miaka ya 1920 kabla United kurudia mashati yenye rangi nyekundu pekee, pia ilitumika kwa ajili ya michuano ya nyumbani na ugenini katika msimu wa 2009-10 kama njia ya kusherehekea miaka 100 katika Old Trafford.[35][36]

Jezi za kuchezea ugenini kawaida huwa nyeupe na kaptura nyeusi na soksi nyeupe, lakini rangi nyingine zimetumika, ikiwa ni pamoja na shati iliyokuwa na milia ya samawati na nyeupe iliyotumika kati ya 1903-1916, sare nyeusi kila kitu kilichotumika mwaka 1994, 2003 na 2007 na shati la blue iliyokuwa na mistari myembamba mwaka 2000. Mojawapo ya sare iliyokuwa maarufu kwa wengi, japo haikudumu, ni sare ya United iliyokuwa ya michuano ya ugenini ya rangi ya kijivu pekee iliyotumika kati ya 1995-96, iliacha kutumiwa baada ya timu kushindwa mchezo mmoja wakati walikuwa wameivaa. Katika muda wa mapumziko wakicheza dhidi ya Southampton, wakati united ilikuwa imetingwa 3-0, walibadilisha mavazi na kuvaa sare ya samawati na nyeupe lakini bado wakashindwa 3-1. Kulingana na wachezaji, mavazi ya kijivu hayakuwa yakionekana vyema jambo lililosababisha matokeo duni.[37] Sare nyingine maarufu ya kucheza ugenini ya Man Utd ilikuwa uweza wa kuvalika pande zote, ilikuwa na milia ya nyeupe na mikono mieusi na mstari wa kidhahabu upande mmoja na milia ya kidhahabu na mstari mweusi upande mwingine. Shati hii ilitolewa kama sare ya mwisho iliyoshonwa na Umbro kwa klabu kabla ya kuanza kuhudumiwa na Nike, na iliadhimisha miaka 100 tangu klabu kilipobadili jina lake kutoka Newton Heath kuwa Manchester United.

Sare ya tatu ambayo huvaliwa katika michuano ya nyumbani ni samawati tangu shati hadi sokisi kwa heshima ya sare iliyovaliwa 1968 timu iliposhinda Kombe la Ulaya, ukumbusho wa moja kwa moja ulifanywa na klabu 2008-09 kukumbuka miaka 40 ya jezi la tatu la 1968. Kinyume na desturi hii ni kuwa ni pamoja na sare ya rangi ya manjano iliyovaliwa katika miaka ya 1970, sare iliyotajwa hapo awali ya mistari ya samawati na nyeupe kuanzia 1996, ambayo ilionekana kuwapendeza sana mashabiki, na shati jeupe iliyokuwa na mikato ya mlazo wa rangi nyeusi na nyekundu kuanzia 2004. United pia imetumia shati zilizo wahi kutumika kama ya mazoezi kuwa sare zao za tatu, iliwahi kutumia sare nyeusi toka juu hadi chini katika msimu 1998-99 na shati samawati iliyokuwa na rangi ya damu ya mzee ubavuni mwaka 2001 kwa michuano dhidi ya Southampton na PSV Eindhoven.

Hivi sasa, jezi ya nyumbani ya Manchester United ni nyekundu na iliyo na tepe nyeusi isiyokolea kifuani. Nembo ya klabu huwa juu ya ngao nyeusi yenye ukubwa sawa upande wa kushoto wa V, ilihali alama ya Nike ni nyeupe na huwa upande wa kulia; nembo ya AIG pia ni nyeupe. Katika kukumbuka miaka 100 tangu kufunguliwa kwa uwanja wa klabu hicho cha Old Trafford kuna kitambulisho kinachosoma “Uwanja wa ndoto tangu 1910” (The Theatre of Dreams Since 1910) kilichoshikishwa upande wa mshono. Shati la nyumbani huvaliwa na kaptura nyeupe iliyo na mistari myekundu inayoteremka pande zote mbili za miguu, na soksi nyeusi iliyo na mkato mwekundu.[35] Hivi karibuni sare ya kucheza ugenini imekaribiana katika muundo na sare ya nyumbani, lakini shati ni jeusi lililo na utepe wa samawati kifuani na nembo ya klabu huwa juu ya ngao ya samawati. Sawa na sare ya nyumbani, nembo ya wadhamini iko katikati na kwa rangi nyeupe. Kaptura pia ni nyeusi na milia ya samawati ikielekea chini, huku soksi nazo zikiwa nyeusi na tepe ya samawati.[36] Sare ya ugenini ya klabu ya msimu wa 2008-09, inayojumuisha shati jeupe lililo na mstari wa samawati kwenda chini ubavuni na ukosi wa samawati ilio na mkato mwekundu, unaotumiwa kama sare ya tatu ya msimu wa 2009-10. Ikivaliwa pamoja na kaptura za samawati na soksi nyeupe, jezi la tatu lina nembo za wafadhili kwa rangi ya samawati pamoja na herufi "MUFC" nyuma ya ukosi.Beji ya klabu inakalia nguo nyeupe kushoto mwa kifua.[38][39]

Nembo ya Manchester United imebadilishwa mara chache, lakini umbo la kimsingi limebakia sawa. Beji hiyo imechukuliwa kutoka kwa nembo ya jiji la Manchester. Picha ya Shetani kwenye beji ya klabu ilitokana na lakabu ya klabu “Red Devils” (Shetani Wekundu); lililoanza kutumika mapema miaka ya 1960 baada ya Matt Busby kusikia likirejelea timu ya raga ya Salford kutokana na jezi zao nyekundu.[40] Kufikia mwisho wa miaka ya 1960 nembo hiyo ya shetani ilianza kujumuishwa katika utaratibu na shali za klabu kabla ya kujumuishwa kwenye beji ya klabu mnamo 1970 ikishikilia mkuki wenye ncha tatu. Katika mwaka wa 1998, beji iliundwa upya tena, wakati huu maneno "Footbal Club" yakiondolewa.[41]

Wachezaji[hariri | hariri chanzo]

Kikosi cha timu ya kwanza[hariri | hariri chanzo]

Kama ilivyokuwa 29 Oktoba 2009,kulingana na vyanzo mseto katika tovuti rasmi.[42][43]

Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.

Na. Nafasi Mchezaji
1 Uholanzi GK Edwin van der Sar
2 Uingereza DF Gary Neville (captain)
3 Ufaransa DF Patrice Evra
4 Uingereza MF Owen Hargreaves
5 Uingereza DF Rio Ferdinand
6 Uingereza DF Wes Brown
7 Uingereza FW Michael Owen
8 Brazil MF Anderson
9 Bulgaria FW Dimitar Berbatov
10 Uingereza FW Wayne Rooney
11 Welisi MF Ryan Giggs (vice-captain)
12 Uingereza GK Ben Foster
13 South Korea MF Park Ji-Sung
14 Serbia MF Zoran Tošić
15 Serbia DF Nemanja Vidić
16 Uingereza MF Michael Carrick
17 Ureno MF Nani
18 Uingereza MF Paul Scholes
Na. Nafasi Mchezaji
19 Uingereza FW Danny Welbeck
20 Brazil DF Fábio
21 Brazil DF Rafael
22 Eire DF John O'Shea
23 Eire ya Kaskazini DF Jonny Evans
24 Uskoti MF Darren Fletcher
25 Ekuador MF Antonio Valencia
26 Ufaransa FW Gabriel Obertan
27 Italia FW Federico Macheda
28 Eire MF Darron Gibson
29 Poland GK Tomasz Kuszczak
30 Ubelgiji DF Ritchie De Laet
31 Eire ya Kaskazini MF Corry Evans
38 Ujerumani GK Ron-Robert Zieler
41 Norwei FW Joshua King
42 Norwei MF Magnus Wolff Eikrem
43 Uingereza MF Matthew James

Wa mkopo[hariri | hariri chanzo]

Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.

Na. Nafasi Mchezaji
35 Uingereza MF Tom Cleverley (at Watford until 3 Januari 2010)[44]
36 Uskoti MF David Gray (at Plymouth Argyle until 18 Desemba 2009)[45]
37 Eire ya Kaskazini DF Craig Cathcart (at Watford until 4 Januari 2010)[46]
Na. Nafasi Mchezaji
40 Uingereza GK Ben Amos (at Peterborough United until 29 Novemba 2009)[47]
Senegal FW Mame Biram Diouf (at Molde until 31 Desemba 2009)[48]

Wa ziada na walio chuoni[hariri | hariri chanzo]

Kwa kikosi cha wachezaji wa ziada na walio chuoni, tazama Manchester United F.C. Reserves and Academy.

Waliokuwa wachezaji hapo awali[hariri | hariri chanzo]

Kwa maelezo juu ya wachezaji wa zamani, tazama Orodha ya wachezaji wa klabu ya Soka ya Manchester United na Category:Manchester United F.C. players

Manahodha wa klabu[hariri | hariri chanzo]

Tarehe [49] Jina Maelezo
1878-1882 Haijulikani
1882 Earth E. Thomas Nahodha wa kwanza wa klabu anayejulikana
1882-1883 Haijulikani
c.1883-1887 Uingereza Sam Black
c.1887-1890 Welisi Jack Powell
1890-1892 Haijulikani
1892-1893 Uskoti Joe Cassidy
1893-1894 Haijulikani
c.1894 Uskoti James McNaught
1894-1896 Haijulikani
c.1896-1903 Uingereza Harry Stafford Nahodha wa kwanza wa Manchester United
1903-1904 Haijulikani
c.1904-1905 Uskoti Jack Peddie
c.1905-1912 Uingereza Charlie Roberts
1912-1913 Uingereza George Stacey
1913 Uingereza Dick Duckworth
1914 Uingereza George Hunter
1914-1915 Uingereza Patrick O'Connell
1915-1919 Hamna Hakuna kandanda iliyochezwa wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia
1919-1922 Haijulikani
c.1922-1928 Uingereza Frank Barson
c.1928-1931 Uingereza Jack Wilson
1931-1932 Uskoti George McLachlan
1932 Uingereza Louis Page
1932-1935 Haijulikani
c.1935-1939 Uskoti Jimmy Brown
1939-1945 Hamna Hakuna kandanda iliyochezwa wakati wa Vita vya Pili vya Dunia
1945-1953 Eire Johnny Carey Nahodha wa Kwanza wa baada ya Vita, na wa kwanza kutoka nje ya Uingereza
1953-1954 Uingereza Stan Pearson
1954-1955 Uingereza Allenby Chilton
1955-1958 Uingereza Roger Byrne Alikufa mwaka wa 1958 katika ajali ya ndege ya Munich
1958-1959 Uingereza Bill Foulkes
1959-1960 Uingereza Dennis Viollet
1960-1962 Uingereza Maurice Setters
1962-1964 Eire Noel Cantwell
1964-1967 Uskoti Denis Law
1967-1973 Uingereza Bobby Charlton
1973 Uskoti George Graham
1973-1975 Uskoti Willie Morgan
1975-1982 Uskoti Martin Buchan
1982 Uingereza Ray Wilkins
1982-1994 Uingereza Bryan Robson Nahodha aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya United
1994-1996 Uingereza Steve Bruce
1996-1997 Ufaransa Eric Cantona Nahodha wa kwanza wa United kutoka nje ya Uingereza na pia Jamhuri ya Ireland
1997-2005 Eire Roy Keane Tuzo nyingi zaidi zilishindwa akiwa nahodha
2005-hadi leo Uingereza Gary Neville Nahodha wa kwanza wa kilabu wa kuzaliwa katika eneo la Greater Manchester tangu enzi za Dennis Viollet

Rekodi za wachezaji[hariri | hariri chanzo]

Kwa mujibu wa mechi iliyochezwa tarehe 8 Novemba 2009 na kulingana na takwimu ya tovuti rasmi.[50] Wachezaji walioandikwa kwa maandishi kolezo ndiyo bado wanaichezea timu ya Manchester United.

Walioshiriki michuano mingi[hariri | hariri chanzo]

# Jina Muda klabuni Kushiriki Mabao
1 Welisi Ryan Giggs 1991-hadi sasa 817 150
2 Uingereza Bobby Charlton 1956-1973 758 249
3 Uingereza Bill Foulkes 1952-1970 688 9
4 Uingereza Paul Scholes 1994-hadi leo 616 144
5 Uingereza Gary Neville 1992-hadi leo 578 7
6. Uingereza Alex Stepney 1966-1978 539 2
7 Eire Tony Dunne 1960-1973 535 2
8 Eire Denis Irwin 1990-2002 529 33
9. Uingereza Joe Spence 1919-1933 510 168
10 Uskoti Arthur Albiston 1974-1988 485 7

Waliofunga zaidi[hariri | hariri chanzo]

# Jina Muda klabuni Mabao Kushiriki Uuwiano wa Mabao/Michezo
1 Uingereza Bobby Charlton 1956-1973 249 758 0.328
2 Uskoti Denis Law 1962-1973 237 404 0.587
3 Uingereza Jack Rowley 1937-1955 211 424 0.498
4 = Uingereza Dennis Viollet 1953-1962 179 293 0.611
4 = Eire ya Kaskazini George Best 1963-1974 179 470 0.381
6. Uingereza Joe Spence 1919-1933 168 510 0.329
7 Welisi Mark Hughes 1983-1986
1988-1995
163 467 0.349
8 = Uholanzi Ruud van Nistelrooy 2001-2006 150 219 0.685
8 = Welisi Ryan Giggs 1991-hadi leo 150 817 0.184
10 Uingereza Stan Pearson 1937-1954 148 343 0.431

Washindi wa matuzo[hariri | hariri chanzo]

Ballon d'Or

Wachezaji wafuatao walikuwa washindi wa Ballon d'Or wakati wakiichezea Manchester United:

European Golden Shoe ( taji la kiatu cha dhahabu cha Ulaya)

Wachezaji wafuatao walikuwa washindi wa European Golden Shoe wakati wakiichezea Manchester United:

Tuzo la UEFA kwa mwanakandanda wa klabu bora wa mwaka

Wachezaji wafuatao walikuwa washindi wa tuzo la UEFA kwa mwanakandanda wa klabu bora wa mwaka wakati wakiichezea Manchester United:

Mchezaji wa mwaka wa FIFA

Wachezaji wafuatao walikuwa washindi wa tuzo laMchezaji wa mwaka wa FIFA wakati wakiichezea Manchester United:

Timu ya akina dada[hariri | hariri chanzo]

Timu ya soka ya akina dada ya Manchester United yaani Manchester United Ladies FC ilianzishwa mwaka 1977 kama klabu ya mashabiki akina dada yaani Manchester United Supporters Club Ladies. Walijiunga na ligi ya Three Counties League mwaka 1979, na wakawa wanachama waanzilishi wa ligi ya wanawake wa eneo la kaskazini (North West Women's Regional Footbal League) mwaka 1989, walipogeuza jina lao rasmi na kuwa Manchester United Ladies FC. Ingawa walishushwa kutoka katika ligi msimu wao wa kwanza, walipandishwa ngazi tena baada ya msimu huo na kushinda taji ya ligi ya 1995-96. Msimu wa 1998-99, timu hiyo ilijiunga na Northern Combination, hatua mbili chini ya Ligi Kuu ya wanawake ya FA. Waliletwa rasmi chini ya mwavuli wa Manchester United FC mwanzo wa msimu wa 2001-02, lakini walivunjiliwa mbali kiutata mwanzo wa msimu wa 2004-05 kwa sababu za kifedha. Uamuzi huo ulikumbwa na upinzani ikizingatiwa faida inayopatikana na Manchester United na pia kutokana na ukweli kuwa timu ziliondolewa ligi zao zote kabla hata wachezaji kuarifiwa kuhusu uamuzi huo. Hata hivyo, klabu bado kilishiriki katika kandanda ya wasichana kwa kutoa mafundisho kwa wasichana chini ya umri wa miaka 16.[51]

Maafisa wa klabu[hariri | hariri chanzo]

Manchester United Limited

 • Wenyekiti wenz: Joel Glazer & Avram Glazer
 • Afisa mkuu mtendaji: David Gill
 • Afisa mkuu wa utekelezaji: Michael Bolingbroke
 • Mkurugenzi wa Kibiashara: Richard Arnold
 • Mkurugenzi mtendaji: Ed Woodward
 • Wakurugenzi wasio watendaji: Bryan Glazer, Kevin Glazer, Edward Glazer & Darcie Glazer

Manchester United Football Club

Maafisa wa ukufunzi na wa kimatibabu

Historia ya usimamizi[hariri | hariri chanzo]

Tarehe Jina Maelezo
1878-1892 Hajulikani
1892-1900 Uingereza AH Albut
1900-1903 Uingereza James West
1903-1912 Uingereza Ernest Mangnall
1912-1914 Uingereza John Bentley
1914-1922 Uingereza Jack Robson
1922-1926 Uskoti John Chapman Meneja wa kwanza kutoka nje ya Uingereza
1926-1927 Uingereza Lal Hilditch
1927-1931 Uingereza Herbert Bamlett
1931-1932 Uingereza Walter Crickmer
1932-1937 Uskoti Scott Duncan
1937-1945 Uingereza Walter Crickmer
1945-1969 Uskoti Mtt Busby Meneja wa kwanza wa baada ya Vita ya Pili ya Dunia na meneja aliyehudumu muda mrefu katika historia ya United
1969-1970 Uingereza Wilf McGuiness
1970-1971 Uskoti Mtt Busby
1971-1972 Eire Frank O'Farrell Meneja wa kwanza kutoka nje ya Uingereza
1972-1977 Uskoti Tommy Docherty
1977-1981 Uingereza Dave Sexton
1981-1986 Uingereza Ron Atkinson
1986-hadi leo Uskoti Alex Ferguson Meneja aliyefaulu sana kwa mujibu wa vikombe

Ufuasi[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya Vita ya Pili vya Dunia, mashabiki wachache wa kandanda wa Uingereza walisafiri mbali kutazama michezo kwa sababu ya muda, gharama, na vikwazo vya kivifaa kama vile uhaba wa magari miongoni mwa wakaazi.[onesha uthibitisho] Jinsi City na United walivyocheza michuano ya nyumbani kwa kubadilishana siku za Jumamosi, Wanamanchester wengi wangetazama United juma moja na juma lifuatalo City, lakini baada ya vita, ushindani mkali ukaibuka na ikawa kawaida zaidi kwa shabiki kuchagua kufuata timu moja pekee.[onesha uthibitisho]

United iliposhinda ligi mwaka 1956, walikuwa na ufuasi wastani wa juu zaidi wa mahudhurio ya ligi nyumbani, rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Newcastle United kwa miaka michache iliyotangulia. Kufuatia ajali yao ya ndege Munich mwaka wa 1958, watu zaidi walianza kushabikia United na wengi wakaanza kuhudhuria michuano. Hii illisababisha ushabiki kwa United kupanuka sababu moja inayofanya United kuwa mahudhurio ya juu katika ligi ya kandanda ya Uingereza kwa takribani kila msimu tangu wakati huo, hata wakati waliposhushwa ngazi na kuwa katika Divisheni ya Pili 1974-75.[1] Kwa kweli, kwa misimu miwili ambayo United haikuwa na mahudhurio ya ligi, Old Trafford ilikuwa ikifanyiwa kazi kubwa ya ujenzi (1971-72 na 1992-93).

Ripoti ya mwaka 2002, kwa anwani Do You come From Manchester?, Ilionyesha kuwa asilimia kubwa ya wanunuzi wa tiketi za msimu za Manchester City huishi katika wilaya za posta za Manchester, wakati United ilikuwa na idadi kamili juu ya wanunuzu wa tiketi za msimu wanaoishi katika eneo moja.[53]

Katika miaka ya 1990 na mapema miaka ya 2000, chanzo cha wasiwasi kwa mashabiki wengi wa United kilikuwa uwezekano wa klabu kununuliwa. Kundi la wafuasi IMUSA (Independent Manchester United Supporters' Association) lilijihusisha sana katika kupinga ununuzi uliotarajiwa wa Rupert Murdoch mwaka 1998. Kundi lingine lililotoa shinikizo klabu kisiuzwe, Shareholders United against Murdoch (ambalo baadaye lilikuwa Shareholders United na sasa ni Manchester United Supporters' Trust) liliundwa wakati huu kuhamasisha wafuasi kununua hisa za klabu, ili kwa kiasi kuwawezesha wafuasi kuwa na usemi zaidi katika masuala yaliyowatia wasiwasi kama vile bei na mgao wa tiketi, na kwa kiasi kupunguza hatari ya watu wasiohitajika kununua hisa za kutosha kumiliki klabu. Hata hivyo, mpango huu ulishindwa kumzuia Malcolm Glazer kuwa mmiliki mwenye hisa nyingi. Wafuasi wengi walikasirishwa, na baadhi walibuni klabu asi kwa jina F.C. United of Manchester. Licha ya hasira ya baadhi ya wafuasi kwa wamiliki wapya, mahudhurio yameendelea kuongezeka.

Hisia zilizotolewa na mashabiki hao, wakati mwingine umeshutumiwa. Mwaka 2000, maoni yaliyotolewa kuhusu baadhi ya mashabiki katika Old Trafford na nahodha wa wakati huo Roy Keane, kwamba baadhi ya mashabiki hawawezi hata " kuendeleza neno kandanda, acha kuielewa" yalipelekea wao kutajwa kama "mashabiki wanaohudhuria mchuano kufurahia ukarimu wa klabu na wala si kuishabikia".[54] Alex Ferguson pia ametoa maoni kadhaa kuhusu mashabiki kiasi kwamba alidai kuwa hali iliyoshuhudiwa tarehe 1 Januari 2008 ilikuwa kama "matanga".[55] Baadaye aliongeza, "Nadhani kumekuwa na siku kama hizi hapo nyuma. Ilitokea miaka michache iliyopita, wakati tulipotawala".[55] Baada ya ushindi maarufu wa 1-0 dhidi ya Barcelona ugani Old Trafford, ambao uliiwezesha United kushiriki katika fainali ya Ligi ya Mabingwa ( Champions League) Moscow, Ferguson alisema kwamba mashabiki wa United "walikuwa wapevu sana" na kwamba wao "walituwezesha kufanikiwa".[56][57]

Uwanja[hariri | hariri chanzo]

Old Trafford
Theatre of Dreams
Old Trafford after its most recent expansion
LocationSir Matt Busby Way,
Old Trafford,
Greater Manchester,
England
Broke ground1909
Opened19 Februari 1910
OwnerManchester United
OperatorManchester United
Construction cost£90,000 (1909)
ArchitectArchibald Leitch (1909)
Capacity76,212 seated[58]
Tenants
Manchester United (Premier League) (1910–present)

Klabu kilipoanzishwa mara ya kwanza, Newton Heath alicheza michuano yao ya nyumbani kwenye uwanja mdogo ulio North Road, Newton Heath. Hata hivyo, timu geni zilizokuja kucheza uwanjani humo zililalamikia hali yake, ambayo ilikuwa "bwawa upande mmoja na uliojaa miamba kama ya timbo upande mwingine".[8] vyumba vya kubadilishia nguo pia havikuwa vya kujivunia, vilikuwa umbali wa kutembea dakika kumi katika baa ya Three Crowns iliyokuwa Oldham Road. Baadaye walihamishiwa Shears Hotel, mkahawa mwingine uliokuwa Oldham Road, hata hivyo mabadiliko yalihitajika kama klabu ilitaka kuendelea katika Ligi ya Kandanda.

Heath walibaki katika uwanja wao wa North Road kwa miaka kumi na mitano 1878-1893, mwaka mmoja baada ya kuingia Football League na baadaye kuhamia makao mapya Bank Street hapo Clayton. Uwanja mpya haukuwa mzuri sana, vipande vichache vya nyasi vilijipenyeza usoni mwa changarawe na mawingu ya moshi yalifuka kutoka katika kiwanda kilichokuwa karibu. Wakati mmoja, Walsall Town Swifts ilikataa kucheza kutokana na hali mbaya ya uwanja. Changarawe ilimwagwa uwanjani na walinda uga, hatimaye wageni wakawashawishi kucheza na kupoteza 14-0. walipinga matokeo hayo, wakitaja hali mbaya ya uwanja kama sababu ya wao kushindwa, mchuano ukarudiwa. Hali haikuwa nzuri sana wakati wa marudiano, timu ya Walsall ilishindwa tena, ingawa wakati huu walibugia 9-0 tu.[8]

Mwaka wa 1902, klabu karibu kifilisike na uwanja wa Bank Street ulifungwa na mdai kutokana na klabu kushindwa kulipa deni lake. Klabu kiliokolewa katika dakika za mwisho na nahodha Harry Stafford ambaye aliweza kuchangisha fedha za kutosha kulipia mchuano wa ugenini Bristol City na kupata uwanja wa muda karibu na Harpurhey kwa kuchezea duru nyingine dhidi ya Blackpool.[59]

Kufuatia uwekezaji kuimarisha klabu tena, jina lilibadilishwa na kuwa Manchester United, ingawa kulikuwa na hamu ya kupata uwanja uliokubalika. Wiki sita kabla ya mchuano wa kwanza wa United kuwania Kombe la FA Aprili 1909, Old Trafford ilitajwa kuwa nyumbani kwa Manchester United kufuatia ununuzi wa ardhi muhimu kwa takribani £ 60,000. Msanifumijengo Archibald Leitch aliajiriwa na mwenyekiti wa United John Henry Davies na kupewa bajeti ya £ 30.000 kwa ajili ya ujenzi. Mipango asilia ilionyesha kuwa uwanja ungefaa kujengwa kuhimili watu 100.000, ingawa idadi hiyo ilipunguzwa hadi 77,000. Licha ya hilo, rekodi ya mahudhurio ya 76,962 ilirekodiwa, ambayo hata sasa ni zaidi ya idadi rasmi inayokubalika katika uwanja huo. Ujenzi ulifanywa na Messrs Brameld na Smith wa Manchester. Katika ufunguzi wa uwanja, tiketi za kusimama ziligharimu peni sita, wakati viti ghali zaidi katika jukwaa kuu zililipiwa shilingi tano. Mchezo wa ufunguzi ulikuwa tarehe 19 Februari 1910 dhidi ya Liverpool FC, na wageni wakashinda kwa 4-3. Kama ilivyotokea, mabadiliko ya uwanja yalitokea wakati mwafaka zaidi - siku chache tu baada ya klabu kucheza mchuano wao wa mwisho ugani Bank Street, mojawapo ya jukwaa liliangushwa chini na dhoruba.[60]

Kupigwa kwa bomu wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, tarehe 11 Machi 1941, kuliharibu sehemu kubwa ya uwanja, hasa jukwaa kuu. Handaki la kati katika South Stand ndilo la pekee lililobakia katika robo hiyo ya uwanja. Baada ya vita, United iliwasilisha ripoti kwa Tume ya Madhara ya Vita na kupokea fidia ya £ 22.278 kwa ajili ya ukarabati wa uwanja huo. Ingawa uwanja ulijengwa upya tena 1949, hakuna mchuano uliosakatwa Old Trafford kwa takribani miaka 10 michuano ya "nyumbani" katika kipindi hicho ilichezwa katika uwanja wa Manchester City, Maine Road. Manchester City iliilipisha United £ 5,000 kwa mwaka kwa matumizi ya uwanja wao, pamoja na asilimia fulani ya ada ya kiingilio.[61]

Marekebisho mengine yalitokea baadaye, yakianza na kuwekwa paa upande wa Stretford End kisha ikawekwa pande za North Stand na East Stand. Hata hivyo, mtindo wa zamani wa paa uliwazuia mashabiki wengi kutazama na hivyo, kupelekea kuboreshwa kwa paa hizo kuwa zilizoinuka na ambazo bado zipo katika uwanja huo leo. Stretford End lilikuwa jukwaa la mwisho kufanyiwa ukarabati wa kuinuliwa paa, kazi iliyokamilika kwa muda ufaao kuruhusu michuano ya msimu wa 1993-94.[62]

Taa za uwanjani ziliwekwa kwa mara ya kwanza uwanjani katikati ya miaka ya 1950. Viunzi-foot180 (m 55) vinne vikuu vilijengwa, kila kimoja kikiwa na taa 54. Mfumo mzima wa taa uliigharima klabu £ 40,000, na kutumika mara ya kwanza katika mechi ya tarehe 25 Machi 1957. Hata hivyo, taa mtindo zamani zilibomolewa mwaka wa 1987, na kubadilishwa na taa za kisasa zilizowekwa katika paa la kila jukwaa, zinadumu hadi leo.

Mwaka 1990, kufuatia janga la Hillsborough Disaster, ripoti ilitolewa iliyotaka viwanja vyote kukarabatiwa ili kuruhusu mashabiki wanaoketi pekee, hilo lilipelekea ukarabati ulioshusha idadi ya mashabiki wanaoruhusiwa hadi takribani 44,000. Hata hivyo, umaarufu wa klabu ulimaanisha kuwa maendeleo zaidi yangetokea. Mwaka 1995, North Stand ilijengwa kuwa na daraka tatu na kuongeza idadi inayoruhusiwa hadi takribani 55,000. Hii ilifuatiwa na upanuzi kwanza wa jukwaa la East na kisha West kufikisha jumla ya idadi ya 68,000. Upanuzi wa hivi karibuni zaidi ulikamilika mwaka 2006, ambapo robo iliyopo North-East na North West ilifunguliwa, na kufikisha rekodi ya idadi ya sasa ya 76,098, 104 tu chini ya upeo wa idadi inayoruhusiwa.[62]

Imekadiriwa kwamba kwa maendeleo zaidi kufanyiwa uwanja, hasa Southern Stand ambayo ndio hadi sasa ina daraka moja tu, gharama ya uboreshaji inaweza kukaribia £ million 114 ambazo tayari zimetumika kuboresha uwanja huo katika miaka kumi na minne iliyopita. Hii ni kutokana na ukweli kwamba ingebidi takriban nyumba hamsini kununuliwa na klabu, hilo huenda likaongeza usumbufu kwa wakazi wa mtaa huo,na upanuzi wowote ungelazimika kujengwa juu ya laini ya reli inayopita karibu na uwanja huo. Kwa kweli , upanuzi huo utajumuisha kuifanya South Stand kuwa na angalau daraka mbili na kujaza jukwaa za South-West na South-East kuhifadhi umbo la "bakuli" la uwanja huo. Makadirio ya sasa yanaashiria kuwa uwanja huo ukijengwa hivyo utakuwa na uwezo wa kuhimili takriban mashabiki 96,000, zaidi wa uwanja mpya wa Wembley.[62]

Udhamini[hariri | hariri chanzo]

AIG ndio wadhamini wakuu wa Manchester United, na kama sehemu ya mpango huo wa udhamini nembo yao imebandikwa mbele ya mashati ya klabu na bidhaa nyingi nyinginezo za klabu. Udhamini wa AIG ulitangazwa na afisa mtendaji wa Manchester United David Gill tarehe 6 Aprili 2006, ina thamani ya £ milioni 56.5 rekodi ya aina yake nchini Uingereza na ya kulipwa kwa takribani miaka minne (£ milioni 14.1 kila mwaka).[63] Udhamini huo ulikuwa wenye thamani zaidi dunia mwezi Septemba 2006 baada ya kubatilishwa kwa udhamini wa £ milioni 15 kila mwaka kati ya Juventus na kampuni ya mafuta ya Tamoil.[64] Tarehe 21 Januari 2009, ilitangaza kuwa AIG haitafanya upya udhamini wao wa klabu ifikapo mwisho wa udhamini wa sasa Mei 2010. Hata hivyo, si wazi ikiwa mkataba wa AIG kusimamia MU Finance utaendelea.[65] Kampuni ya bima ya marekani Aon ilitajwa kama mdhamini mkuu wa klabu tarehe 3 Juni 2009, huku udhamini wao kwa klabu ukianza kutekelezwa mwanzo wa msimu wa 2010-11.[66] Masharti ya mpango huo hawakufichuliwa, lakini imeripotiwa kuwa una thamani ya takriban £ million 80 kwa takriban miaka minne, ambayo itaifanya kuwa mdhamini mkuu zaidi katika historia ya kandanda.[67]

Klabu kimekuwa na wadhamini wakuu watatu tu wa shati. Wa kwanza na waliohudumu kwa muda mrefu zaidi walikuwa Sharp Electronics, ambao walifadhili klabu kuanzia 1982 hadi 2000, ilikuwa moja ya udhamini wa faida kubwa na wa muda mrefu katika Soka ya Uingereza.[68][69] Nembo ya Sharp ilikuwa mbele ya shati za United katika miaka hiyo 17, wakati ambao timu ilishinda mataji saba ya Ligi Kuu, tano za Kombe la FA, moja la Football League, moja la Washindi wa makombe ya Ulaya na moja la Kombe la Ulaya. Vodafone ilichukua udhamini kwa mkataba wa awali wa miaka minne wa £ million 30 tarehe 11 Februari 2000, udhamini ulianza mwanzo wa msimu wa 2000-01.[68][69] Mnamo Desemba 2003, udhamini ulirefushwa kwa miaka minne na Vodafone ikakubaliana kulipa £ million 36 zaidi kwa miaka minne ya 2004-2008.[70] Hata hivyo, tarehe 23 Novemba 2005, Vodafone ilitangaza kuwa itakomesha udhamini wake Mei 2006 ili kuangazia zaidi udhamini wao wa UEFA Champions League.[71]

Vivyo hivyo, klabu imekuwa na washonaji huru nne tu wa sare yake, wa kwanza walikuwa kampuni ya Uingereza UMBRO. Admiral ilichukua usukani mwaka 1975, na kuwa kampuni ya kwanza ya kuweka nembo yao kwenye shati la Manchester United mwaka wa 1976.[72] Adidas ilifuatiwa mwaka 1980,[73] kabla Umbro kuanzaa kipindi chao cha pili kama watengenezaji wa sare za klabu hiyo mwaka wa 1992.[74] Udhamini wa Umbro ulidumu kwa miaka kumi zaidi kabla ya klabu kupata udhamini wa kuvunja rekodi - £ million 302.9 kutoka kwa Nike. Makubaliano na Nike yatadumu kwa miaka 13 ya awali, na kuendelea hadi angalau mwaka wa 2015.[75]

Washindani[hariri | hariri chanzo]

Kihistoria, washindani wa karibu wa Manchester United wamekuwa Liverpool, Manchester City na Leeds United.[76][77] Hivi sasa, mashabiki wengi huona Liverpool kama washindani wao wakubwa kutokana na mafanikio ya klabu zote mbili,[78] ingawa bado wengine huiorodhesha Manchester City kama wapinzani wao wakuu.

Ushindani na Liverpool ulianza katika miaka ya 1960 wakati klabu hizo mbili zilikuwa kati ya klabu imara zaidi Uingereza, na zimekuwa zikishindana kwa karibu sana kila msimu tangu zamani. Ushindani wa Manchester City ulianza wakati wa enzi ya Newton Heath ya miaka ya 1890 na imebakia kali kutokana na klabu hizi mbili kuwa katika divisheni sawa kwa muda mrefu wa historia yao. Huku ushindani ukiwa na msingi wa ukinzani wa jadi kati yaYorkshire-Lancashire, ushindani kati yao na Leeds United ulianza mwishoni mwa miaka ya 1960 wakati Leeds ilitawazwa mshindi, na kuendelea katika miaka ya 1970 na 1980 kabla kufikia kilele wakati Leeds ilipoiadhibu United katika taji la ligi 1992.

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Nchini Uingereza[hariri | hariri chanzo]

Ligi[hariri | hariri chanzo]

Vikombe[hariri | hariri chanzo]

Ya Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Duniani[hariri | hariri chanzo]

na ni moja wapo ya bora ulimwenguni ambayo ina makombemengi

Ushindi wa mataji mawili au matatu[hariri | hariri chanzo]

Hasa mashindano mafupi kama vile Charity / Community Shield, Kombe la mabara, Kombe la FIFA la klabu za Dunia au Super Cup hazifikiriwi kwa jumla kuchangia Ushindi mara mbili au tatu.

Taji kuu la peke ambalo Manchester United haijashinda kamwe ni Kombe la UEFA,[80] ingawa walifika robo-fainali mwaka 1984-85 na nusu fainali ya mashindano tangulizi ya michuano hiyo Inter-Cities Fairs Cup, mwaka wa 1964-65.[81][82]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. 1.0 1.1 "European Football Statistics". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-06-13. Iliwekwa mnamo 24 Juni 2006.
 2. "Manchester United win 11th FA Cup", CBC Sports, Canadian Broadcasting Corporation, 22 Mei 2004. Retrieved on 12 Agosti 2007. Archived from the original on 2013-05-21. 
 3. "United tops global rich list", premierleague.com, Premier League, 11 Januari 2008. Retrieved on 11 Januari 2008. Archived from the original on 2011-11-09. 
 4. "Soccer Team Valuations (Special Report)", Forbes.com, Forbes, 4 Aprili 2009. Retrieved on 12 Agosti 2009. 
 5. "Agreement heralds new era in football", uefa.com, Union of European Football Associations, 21 Januari 2008. Retrieved on 21 Januari 2009. 
 6. Northcroft, Jonathan. "20 glorious years, 20 key decisions", The Sunday Times, Times Newspapers, 5 Novemba 2006. Retrieved on 26 Januari 2009. 
 7. "Neville appointed Man Utd skipper", BBC Sport, British Broadcasting Corporation, 2 Desemba 2005. Retrieved on 21 Januari 2009. 
 8. 8.0 8.1 8.2 Murphy, Alex (2006). "1878-1915: From Newton Heath to Old Trafford". The Official Illustrated History of Manchester United. London: Orion Books. uk. 14. ISBN 0-7528-7603-1.
 9. "Manchester United FC". Talk Football. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-08-19. Iliwekwa mnamo 2008-03-09.
 10. Bill Wilson. "Man Utd's turbulent business history", BBC News, 29 Juni 2005. Retrieved on 8 Juni 2007. 
 11. Murphy, Alex (2006). "1878-1915: From Newton Heath to Old Trafford". The Official Illustrated History of Manchester United. London: Orion Books. uk. 16. ISBN 0-7528-7603-1.
 12. "1908 Charity Shield". footballsite.co.uk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-08-19. Iliwekwa mnamo 12 Agosti 2007.
 13. "Munich Air Disaster", BBC News. Retrieved on 12 Agosti 2007. 
 14. "August 19 - "You'll Never Win Anything With Kids"". On This Football Day. 19 Agosti 2007. Iliwekwa mnamo 5 Januari 2009.
 15. "Cantona crowns United's season of Double delight", Daily Telegraph, Telegraph Media Group, 12 Mei 1996. Retrieved on 11 Desemba 2006. Archived from the original on 2006-12-31. 
 16. 16.0 16.1 "United crowned kings of Europe", BBC News, 26 Mei 1999. Retrieved on 11 Agosti 2008. 
 17. 17.0 17.1 "Man United stands alone". Sports Illustrated. 16 Mei 1999. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-01-06. Iliwekwa mnamo 11 Agosti 2008.
 18. "Two down, one to go". Sports Illustrated. 22 Mei 1999. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-06. Iliwekwa mnamo 11 Agosti 2008.
 19. "Ferguson and Magnier: a truce in the internal warfare at United". International Herald Tribune. 8 Machi 2004. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-11-28. Iliwekwa mnamo 11 Agosti 2008.
 20. "Other News in Soccer in 1999". Sports Info Japan. Iliwekwa mnamo 11 Agosti 2008.
 21. "G-14's members". G14.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-09-02. Iliwekwa mnamo 12 Septemba 2006.
 22. "Glazer Man Utd stake exceeds 75%", BBC News, 16 Mei 2005. Retrieved on 11 Agosti 2007. 
 23. 23.0 23.1 "Manchester United's new owner", CBS Sports Online, 22 Juni 2005. Retrieved on 11 Agosti 2007. Archived from the original on 2005-09-10. 
 24. "Glazer's sons join Man U board". ABC News. 8 Juni 2005. Iliwekwa mnamo 2008-08-11.
 25. "Ruud accuses Ferguson of betrayal", BBC Sport, 7 Septemba 2006. Retrieved on 11 Desemba 2006. 
 26. "Glazers Tighten Grip On United With Debt Refinancing". The Political Economy of Football. 8 Julai 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-08-19. Iliwekwa mnamo 11 Agosti 2008.
 27. "Manchester United reveal refinancing plans". RTÉ Sport. 18 Julai 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-08. Iliwekwa mnamo 11 Agosti 2008.
 28. "Seven wonders of sublime United dazzle and destroy helpless Roma", The Guardian, 4 Januari 2009. 
 29. Caroline Cheese. "AC Milan 3-0 Man Utd (Agg: 5-3)", BBC Sport, 2 Mei 2007. Retrieved on 28 Mei 2007. 
 30. McNulty, Phil. "Man Utd 0-0 Tottenham (aet)", BBC Sport, British Broadcasting Corporation, 1 Machi 2009. Retrieved on 1 Machi 2009. 
 31. McNulty, Phil. "Man Utd 0-0 Arsenal", BBC Sport, British Broadcasting Corporation, 16 Mei 2009. Retrieved on 16 Mei 2009. 
 32. Bell, Jack (27 Mei 2009). "Champions League Final: Barcelona 2, Manchester United 0 - Goal Blog - NYTimes.com". Goal.blogs.nytimes.com. Iliwekwa mnamo 27 Mei 2009.
 33. "Manchester United Historical Kits". historicalkits.co.uk. Iliwekwa mnamo 11 Agosti 2008.
 34. "English FA Cup Finalists 1900 - 1909". historicalkits.co.uk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-09-25. Iliwekwa mnamo 11 Agosti 2008.
 35. 35.0 35.1 Thompson, Gemma. "Gallery: New home kit", ManUtd.com, Manchester United, 26 Juni 2009. Retrieved on 26 Juni 2009. 
 36. 36.0 36.1 Thompson, Gemma. "Black and blue suits Reds", ManUtd.com, Manchester United, 29 Julai 2009. Retrieved on 29 Julai 2009. 
 37. "Grey day for Manchester United", BBC.co.uk. Retrieved on 28 Mei 2007. 
 38. Thompson, Gemma. "Free trophy pic with new kit", ManUtd.com, Manchester United, 18 Julai 2008. Retrieved on 26 Juni 2009. 
 39. "Third Kit 2009/10". United Direct. Manchester United. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-08-05. Iliwekwa mnamo 7 Agosti 2009.
 40. "A to Z of Manchester United — R". ManUtdZone.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-22. Iliwekwa mnamo 3 Agosti 2007. In the early 1960's Salford Rugby club toured France wearing red shirts and became known as "The Red Devils". Manager Matt Busby liked the sound of it, thinking that a nasty devil is more intimidating to opponents than angelic babes.
 41. "Manchester United kits". prideofmanchester.com. Iliwekwa mnamo 28 Mei 2007.
 42. "First Team". ManUtd.com. Manchester United. Iliwekwa mnamo 22 Septemba 2009.
 43. "Reds register European squad", ManUtd.com, Manchester United, 2 Septemba 2009. Retrieved on 3 Septemba 2009. 
 44. Coppack, Nick. "Young Reds on loan", ManUtd.com, Manchester United, 18 Agosti 2009. Retrieved on 18 Agosti 2009. 
 45. "Graychester", pafc.co.uk, Plymouth Argyle FC, 18 Septemba 2009. Retrieved on 18 Septemba 2009. Archived from the original on 2009-09-22. 
 46. Bartram, Steve. "Cathcart joins Hornets", ManUtd.com, Manchester United, 15 Septemba 2009. Retrieved on 15 Septemba 2009. 
 47. "Posh sign Man Utd keeper on loan", BBC Sport, British Broadcasting Corporation, 29 Oktoba 2009. Retrieved on 29 Oktoba 2009. 
 48. Bostock, Adam. "United agree terms for striker", ManUtd.com, Manchester United, 17 Julai 2009. Retrieved on 17 Julai 2009. 
 49. Crick, Michael (1999) [1996]. Manchester United: The Complete Fact Book (toleo la 2nd). London: Profile Books. ku. 46–47. ISBN 1-86197-206-7.
 50. Endlar, Andrew. "The Website of Dreams". StretfordEnd.co.uk. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2009.
 51. Towle, Theresa (2005). "United abandons women's football" (PDF). United Shareholder (26). Shareholders United: 10. Iliwekwa mnamo 21 Januari 2009. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
 52. "Anatomy of the United Bench". Inside United (195): 18–19. 2008. Richard Hawkins has the fascinating title of 'head of human performance'. He works with the sports science team at Carrington, helping the players reach peak physical performance. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
 53. Dr. Adam Brown (2002). "Do You Come From Manchester?" (PDF). Manchester Metropolitan University. uk. 3. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2008-02-27. Iliwekwa mnamo 28 Mei 2007.
 54. "Home 10 classic Roy Keane rants", Guardian, 24 Agosti 2006. Retrieved on 18 Mei 2008. 
 55. 55.0 55.1 "Home support disappoints Ferguson", BBC Sport, 2 Januari 2008. Retrieved on 2 Januari 2008. 
 56. "Boss: Fans forced us to play", ManUtd.com, Manchester United, 29 Aprili 2008. Retrieved on 4 Januari 2009. 
 57. "FERGUSON HAILS SCHOLES GOAL", Football365, 28 Aprili 2008. Retrieved on 28 Aprili 2008. Archived from the original on 2009-05-05. 
 58. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named sky_sports
 59. Murphy, Alex (2006). "1878-1915: From Newton Heath to Old Trafford". The Official Illustrated History of Manchester United. London: Orion Books. uk. 15. ISBN 0-7528-7603-1.
 60. Murphy, Alex (2006). "1878-1915: From Newton Heath to Old Trafford". The Official Illustrated History of Manchester United. London: Orion Books. uk. 27. ISBN 0-7528-7603-1.
 61. White, John (2007) [2005]. The United Miscellany (toleo la 2nd). London: Carlton Books. uk. 11. ISBN 978-1-84442-745-1.
 62. 62.0 62.1 62.2 "Old Trafford 1909-2006". ManUtdZone.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-02-17. Iliwekwa mnamo 21 Mei 2007.
 63. "Man Utd sign £56m AIG shirt deal", BBC News, British Broadcasting Corporation, 6 Aprili 2006. Retrieved on 28 Mei 2007. 
 64. "Oilinvest to renegotiate Juventus sponsorship". SportBusiness.com. 7 Septemba 2006. Iliwekwa mnamo 28 Mei 2007.
 65. "AIG ends Man Utd sponsorship deal", BBC News, British Broadcasting Corporation, 21 Januari 2009. Retrieved on 21 Januari 2009. 
 66. Communications Dept. "Future shirt sponsor unveiled", ManUtd.com, Manchester United, 3 Juni 2009. Retrieved on 3 Juni 2009. 
 67. "Man Utd in new shirt sponsor deal", BBC News, British Broadcasting Corporation, 3 Juni 2009. Retrieved on 3 Juni 2009. 
 68. 68.0 68.1 "Vodafone in £30m Man Utd tie-up", BBC News, British Broadcasting Corporation, 11 Februari 2000. Retrieved on 8 Aprili 2008. 
 69. 69.0 69.1 "United must find new shirt sponsor", CNN.com International, 24 Novemba 2005. Retrieved on 8 Aprili 2008. 
 70. "Man Utd rings up £36m shirt deal", BBC News, British Broadcasting Corporation, 1 Desemba 2003. Retrieved on 21 Januari 2009. 
 71. "Vodafone ends Man Utd shirt deal", BBC News, British Broadcasting Corporation, 23 Novemba 2005. Retrieved on 21 Januari 2009. 
 72. "Manchester United Shirts 1970-79". Pride Of Manchester. Iliwekwa mnamo 13 Agosti 2008.
 73. "Manchester United Shirts 1980-89". Pride Of Manchester. Iliwekwa mnamo 13 Agosti 2008.
 74. "Manchester United Shirts 1990-99". Pride Of Manchester. Iliwekwa mnamo 13 Agosti 2008.
 75. "A to Z of Manchester United — N". ManUtdZone.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2001-04-22. Iliwekwa mnamo 22 Mei 2007.
 76. "Bitter rivals do battle". Daily Telegraph. 15 Aprili 2008. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-08-19. Iliwekwa mnamo 6 Mei 2008.
 77. "United's rivalries". Manchester Evening News. 16 Septemba 2005. Iliwekwa mnamo 23 Desemba 2007.
 78. "Liverpool v Manchester United preview". Sky Sports. Iliwekwa mnamo 23 Desemba 2007.
 79. 79.0 79.1 79.2 [342] ^ Baada ya kubuniwa kwake mwaka wa 1992, Ligi Kuu imekuwa daraja ya juu katika kandanda ya Uingereza; Divisheni ya Kwanza na ya Pili zilifanywa kuwa daraja za pili na tatu katika usanjari huo. Divisheni ya kwanza sasa inajulikana kama Football League Championship na Divisheni ya Pili sasa inajulikana kama Football League One.
 80. "Trophy Room". ManUtd.com. Manchester United. 2009. Iliwekwa mnamo 4 Januari 2009.
 81. "UEFA Cup — Season 1984-1985 - Quarter-finals". uefa.com. Union of European Football Associations. Iliwekwa mnamo 15 Februari 2009.
 82. Zea, Antonio (9 Januari 2008). "Fairs' Cup 1964-65". rsssf.com. Rec.Sport.Soccer Statistics Foundation. Iliwekwa mnamo 15 Februari 2009. {{cite web}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons