Rupert Murdoch

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'

Rupert Murdoch
Keith Rupert Murdoch mnamo 2012
Amezaliwa11 Machi 1931
Kazi yakemjasiriamali wa vyombo vya habari kutoka nchini Australia


Rupert Keith Murdoch (alizaliwa 11 Machi 1931) ni mjasiriamali wa vyombo vya habari kutoka nchini Australia.

Anamiliki kampuni ya News Corporation yenye mamia ya magazeti, vituo vya redio na televisheni kote duniani, hasa kwa lugha ya Kiingereza. Media zake ni pamoja na magazeti ya The Sun na The Times (Uingereza), The Daily Telegraph, Sky News Australia, Herald Sun na The Australian (Australia), Fox News, The Wall Street Journal na New York Post (Marekani). Aliwahi kumiliki pia Runinga ya Sky (hadi 2018) na kampuni ya filamu 21st Century Fox (hadi 2019). [1]

Tangu mwaka 1985 amekuwa raia wa Marekani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "PowerPoint Presentation" (PDF). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 September 2010. Iliwekwa mnamo 11 July 2011.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rupert Murdoch kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.