Patrice Evra
Patrice Evra | ||
Maelezo binafsi | ||
---|---|---|
Tarehe ya kuzaliwa | {{{tareheyakuzaliwa}}} | |
Mahala pa kuzaliwa | {{{nchialiozaliwa}}} | |
* Magoli alioshinda |
Patrice Latyr Evra (amezaliwa 15 Mei 1981) ni mchezaji wa mpira kutoka nchi ya Ufaransa, ambaye anaisakatia kabumbu timu ya Uingereza ya Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa. Yeye ni mlinzi wa kushoto ambaye anaweza pia kucheza upande wa kushoto wa uwanja.
Mwana wa mwanadiplomasia, Evra alizaliwa mjini Dakar, Senegal, na aliwasili Ulaya kupitia Brussels kutoka Senegal wakati alikuwa na umri wa miaka sita. Yeye alilelewa Les Ulis, Essonne, Ufaransa, ambako aliishi na familia yake kuanzia mwaka wa 1984 hadi 1998 kabla ya kuchukua nafasi yake ya kwanza ya kucheza kandanda ambayo ilimpelek Marsala, Sicily, Italia.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Wasifu wa Klabu
[hariri | hariri chanzo]Wasifu wa Mapema
[hariri | hariri chanzo]Katika miaka ya yake ya ujana, Evra alianza kazi yake kama winga wa timu ya vijana ya Paris Saint-Germain. Ingawa hakupokea kamwe mkataba wa kitaalima, alichunguzwa na skauti wa timu ndogo ya Italia iitwayo Marsala,ambayo hatimaye walimpa mkataba. Baada ya kucheza mechi 27 msimu wake wa kwanza kama wing'a wa kushambulia, Evra alifunga mabao sita. Msimu ulifuatao, aliichezea timu ya Monza katika Serie B (ligi ya daraja ya pili, Italia), lakini alicheza mechi tatu pekee yake.
Nice
[hariri | hariri chanzo]Evra alirudi Ufaransa kuichezea Nice ya Ligue 2, yaani daraja ya pili. Katika mechi zake kadhaa za kwanza, yeye alicheza kama mshambulizi wa mbele. Kutokana na majeraha ya wachezaji wenzake katika klabu hiyo, alifanywa kucheza kama mlinzi wa kushoto wakati wa mchezo wao dhidi ya Stade Lavallois. Katika mechi kadhaa zilizofuata, meneja Sandro Salvioni alimtumia Evra katika safu ya ulinzi. Wakati uliosalia katika msimu huo, Salvioni aliendelea kumbadilisha kati ya nafasi hizo mbili. Evra aling'ara ulinzini baada ya kutajwa kama mlinzi bora wa kushoto katika Ligue 2.
AS Monaco
[hariri | hariri chanzo]AS Monaco, ambao walifurahishwa sana na juhudi za Evra ulinzini, walimsaini kutoka Nice kwa ada ambayo haikufumbuliwa kupitia meneja Didier Deschamps. Kwa haraka akawa mchezaji wa kawaida wa ulinzi pamoja na Sebastien Squillaci, Gael Givet, na Julien Rodriguez. Katika msimu wake wa kwanza na klabu hiyo, Monaco ilifika fainali ya Kombe la Mabingwa barani Ulaya (UEFA Champions League) mwaka wa 2004 lakini walishindwa 3-0 na Porto, mchezo ambao Evra alicheza dakika 90.[1] Mchezo wake ulimsababisha kuitwa katika timu ya kitaifa ya Ufaransa.
Mwaka wa 2005, Evra alitajwa nahodha mara kadha. Monaco walipambana msimu huo kwani walichujwa katika raundi za kuhitimu za Kombe la Mabingwa barani Ulaya ya mwaka wa 2005-2006 na mara nyingi msimu huo walikuwa nusu ya meza ya ligi hiyo.
Manchester United
[hariri | hariri chanzo]Evra alisaini mkataba wa Manchester United tarehe 10 Januari 2006, ada ya uhamisho ikizungukia paundi milioni 5.5 kutoka AS Monaco. Muda wa mkataba huu ulikuwa wa miaka tatu unusu.[2] Kuwasili kwa Evra kuliashiria azma au nia ya Alex Ferguson kutatua shida ya safu la ulinzi ambalo lilikuwa limehangaika tangu Gabriel Heinze alipojeruhiwa. Katika mkutano wake wa kwanza na klabu baada ya kusainiwa, alimuliza nahodha Gary Neville pahali ambapo kanisa karibu ipo.[3]
Aliichezea Manchester United kwa mara ya kwanza siku nne baada ya kusainiwa.Manchester United walishindwa mechi hii ya ligi kuu la Uingereza 3-1 na Manchester City. Mechi yake ya kwanza haikuwa bora kwani alitolewa wakati wa mapumziko ya kwanza yaani hafutaimu. Alicheza mechi yake ya kwanza nyumbani baina ya Liverpool, mechi ambayo Manchester United ilishinda 1-0 jumatano iliyofuata. Awali Evra alikuwa na baadhi ya matatizo ya kujirakibisha na mchezo wa Uingereza, lakini katikati ya msimu wa 2006-07 fomu yake iliboreka sana na alijiimarisha kama mchezaji wa kawaida wa timu ya kwanza. Tarehe 29 Novemba, alifunga bao lake la kwanza la klabu katika mechi ya ligi dhidi ya Everton katika uwanja wa Old Trafford. Baada ya kukaa nje ya kikosi, Evra alirejea tarehe 10 Aprili 2007 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Roma katika uwanja wa Old Trafford. Alichangia Red Devils kuinyuka wageni hao 7-1 bao lake likiwa la mwisho, la kwanza katika ligi hili la Mabingwa. Kutokana na juhudi zake, Evra alichuma mahala katika timu ya mwaka ya PFA.
Katika msimu wa 07-08, Evra akawa mlinzi muhimu katika safu ya ulinzi. Ingawa alicheza mechi 47 katika mashindano yote kwa ujumla, idadi iliyojuu zaidi katika wasifu wake, hakuweza kufunga bao. United ilishinda ligi hiyo kwa mara ya pili mfululizo siku ya mwisho ya ligi. Waliushinda ubingwa huo wakiwa na alama mbili zaidi ya Chelsea. Alicheza mechi kumi katika ligi ya Mabingwa barani Ulaya ya UEFA, pamoja na fainali ambayo United iliichapa Chelsea kwa njia ya penalti mabao 6-5, kufuatia sare ya 1-1 baada ya muda wa ziada. Tarehe 12 Juni, Evra alisaini mkataba wa urefusho wa miaka minne na United, sunobari ambao utamweka Old Trafford hadi mwaka wa 2012.[4]
Evra alicheza mechi 14 za Manchester United za kwanza za msimu wa 2008-09. Hata hivyo, tarehe 5 Desemba 2008, alipigwa marufuku kutocheza mechi nne - iliyofaa kuanza tarehe 22 Desemba 2008 - na alifainiwa paundi 15000 baada ya kupatikana na hatia ya kuwa na tabia isiyo halali na FA. Shtaka hili lilihusishwa na tukio lilotokea baada ya mechi kati ya Chelsea na Manchester United tarehe 26 Aprili 2008. Dafrao lilizuka baina ya wachezaji wa Manchester United wafanyikazi wa Chelsea.
Wasifu wa Kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Wakati wa Euro 2008, Evra hakujumuishwa kwenya kikosi cha kwanza dhidi ya Romania ndiposa Eric Abidal wa Barcelona apate kucheza. Aliitwa mechi iliyofuata dhidi ya Uholanzi baada ya sare tasa dhidi ya Romania. Ufaransa ilipoteza mechi hiyo 4-1. Mechi ya mwisho katika kundi hicho ilikuwa ni lazima Ufaransa ishinde baina ya Italia. Ufaransa waliopoteza mechi hiyo 2-0 na walibanbuliwa katika mashindano hayo. Baada ya mechi hiyo, kamera ziliwapata Evra na Patrick Vieira wakikaripiana kwenye handaki.
Maisha ya Kibinafsi
[hariri | hariri chanzo]Evra amemwoa Sandra ambaye wana mwana mvulana, Lenny.[5][6] Ana jumla ya ndugu 25, ingawa wawili sasa ni marehemu.[3]
Takwimu ya Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Klabu | Msimu | Ligi | Kikombe | Kikombe cha Carling | Europa | Zingine [7] | Jumla | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Matokeo | Mabao | Matokeo | Mabao | Matokeo | Mabao | Matokeo | Mabao | Matokeo | Mabao | Matokeo | Mabao | ||
Marsala | 1998-99 | [43] | 3 | -- | -- | -- | -- | -- | -- | -- | [43] | 3 | |
Monza | 1999-2000 | 3 | 0 | -- | -- | -- | -- | -- | -- | -- | 3 | 0 | |
Nice | 2000-01 | 5 | 0 | -- | -- | -- | -- | -- | -- | -- | -- | 5 | 0 |
2001-02 | 34 | 1 | -- | -- | -- | -- | -- | -- | -- | -- | 34 | 1 | |
Jumla | 39 | 1 | -- | -- | -- | -- | -- | -- | -- | -- | 39 | 1 | |
AS Monaco | 2002-03 | 36 | 2 | -- | -- | -- | -- | 0 | 0 | -- | -- | 36 | 2 |
2003-04 | [46] | 0 | -- | -- | -- | -- | 13 | 0 | -- | -- | 46 | 0 | |
2004-05 | 36 | 0 | -- | -- | -- | -- | 9. | 0 | -- | -- | 45 | 0 | |
2005-06 | 15 | 0 | -- | -- | -- | -- | 7 | 0 | -- | -- | 22 | 0 | |
Jumla | 120 | 2 | -- | -- | -- | -- | 29 | 0 | -- | -- | 149 | 2 | |
Manchester United | 2005-06 | 11 | 0 | 1 | 0 | 2 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 14 | 0 |
2006-07 | [43] | 1 | 4 | 0 | 1 | 0 | 7 | 1 | 0 | 0 | 36 | 2 | |
2007-08 | [46] | 0 | 4 | 0 | 0 | 0 | 10 | 0 | 1 | 0 | 48 | 0 | |
2008-09 | 28 | 0 | 3 | 0 | 2 | 0 | 11 | 0 | 4 | 0 | 48 | 0 | |
2009-10 | 14 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 4 | 0 | 1 | 0 | 19 | 0 | |
Jumla | [87] | 1 | 12 | 0 | 5 | 0 | 32 | 1 | 6. | 0 | 165 | 2 | |
Jumla wa wasifu | 296 | 7 | 12 | 0 | 5 | 0 | [60] | 1 | 6. | 0 | 380 | 8 |
Takwimu ni sahihi kutokana na mechi iliyochezwa tarehe 28 Novemba 2009 [8][9]
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Klabu
[hariri | hariri chanzo]AS Monako
[hariri | hariri chanzo]- Coupe de la Ligue (1): 2003
Manchester United
[hariri | hariri chanzo]- Ligi kuu la Uingereza (3): 2006-07, 2007-08, 2008-09
- Kikombe cha Carling (2): 2006, 2009
- FA Community Shield (2): 2007, 2008
- Ligi kuu ya Mabingwa barani Ulaya (UEFA) (1): 2008
- FIFA Club World Cup (1): 2008
Kibinafsi
[hariri | hariri chanzo]Marejeleo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Porto 3-0 Monaco", BBC Sport, 2004-05-26. Retrieved on 2009-02-09.
- ↑ "Evra completes Man Utd transfer". BBC Sport. 2006-01-10. Iliwekwa mnamo 2008-05-16.
- ↑ 3.0 3.1 "Evra: Thank God I'm at United". The Times. 2007-07-22. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-25. Iliwekwa mnamo 2007-08-26.
- ↑ "Evra puts pen to paper", Manchester United, 2008-06-12. Retrieved on 2008-06-12.
- ↑ "The War of the WAGSKIS", Daily Mail, 2008-05-21. Retrieved on 2008-11-03.
- ↑ "Best of the left", The Guardian, 2008-10-19. Retrieved on 2008-11-03.
- ↑ [18] ^ Yajumuisha ushindani wa mashindano mengine, zikiwemo FA Community Shield, Uefa Super Cup, kombo la intercontinental , FIFA Club World Cup
- ↑ "Patrice Evra". StretfordEnd.co.uk. Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2009.
- ↑ (Kifaransa) Patrice Evra at L'Équipe Football
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- = (FE60904B-C2A8-4E60-9B05-700DBBC29BBC) & sehemu = playerProfile & teamid = 458 & bioid = 91915 Profile at ManUtd.com
- Profile saa StretfordEnd.co.uk
- Patrice Evra career stats kwenye Soccerbase