Karim Benzema

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Karim Benzema akiwa na Real Madrid
Karim abenzema akiichezea timu yake ya taifa ya Ufaransa

Karim Mostafa Benzema (alizaliwa Lyon, 19 Desemba 1987) ni mchezaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa. Anajulikana kama straika mwenye kipaji na mwenye nguvu.

Benzema alianza uchezaji kwenye klabu ya Terraillon. Mwaka 1996 alijiunga na klabu ya akademi. Kwenye msimu wa 2004-05 aliiwezesha timu yake kushinda makombe matatu,na msimu wa 2007-08 alibeba kombe la ligi na kuwa kombe la saba kwa Olympique Lyonnais, na kuwa mchezaji bora wa mwaka,na kuwa timu bora ya mwaka.Benzema alikuwa mfungaji bora na kushinda tuzo kutoka gazeti la Italia laGuerin Sportivo. Msimu uliofuata Olympique Lyonnais ilimuuza kwenda Real Madrid kwa ada ya £35 milioni ($50 milioni)na kusaini miaka sita. Baada ya kuhangaika ili aweke heshima,kwa misimu miwili alishinda magoli 32 na kui wezesha Real Madrid kushinda Copa Del rey mwaka 2011,na msimu wa 2011-12 alikuwa mchezaji bora mfaransa mara tatu mwaka 2011,2012,2014.

Benzema alikuwa mchezaji wa timu ya taifa na kuiwakilisha nchi yake chini ya miaka 17. Aliiwezesha timu yake ya taifa kushinda 2004 UEFA European Under-17 Championship.. Benzema kwenye timu ya wakubwa alishinda goli lake la kwanza dhidi ya Austria 1-0.

Mnamo Oktoba 2021, katika kesi ya ngono ya Mathieu Valbuena, ofisi ya mwendesha mashtaka wa Versailles iliomba korti ya jinai kumpa adhabu ya kifungo cha miezi kumi kilichosimamishwa na faini ya euro 75,000.

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Karim Benzema kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.