Liverpool F.C.

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wachezaji wa Liverpool kabla ya mechi kuanza dhidi ya Wigan Athletic mnamo machi 9 2010

Liverpool Football Club (/ˈlɪvərpuːl/) ni klabu kubwa ya mpira wa miguu mjini Liverpool, Uingereza, inayoshiriki Ligi Kuu Uingereza (EPL). Imeshinda mataji sita ya European Cups, 3 ya UEFA Cups, 4 UEFA Super Cups, 18 ya Ligi kuu, 7 ya FA Cups, 8 Kombe la ligi,and 15 Ngao ya jamii ya FA.

Imeanzishwa mwaka 1892, ikajiunga na ligi mwaka mmoja baadaye ikiutumia uwanja wa Anfield tangu kuanzishwa. Liverpool ilileta ushindani mkubwa kwenye ligi ya Uingereza na Ulaya kwa ujumla kwenye miaka ya 1970 na 80 ambapo Bill Shankly na Bob Paisley wakiisaidia kushinda mataji 11 ya ligi na mataji 7 ya ulaya. Ikifundishwa na Rafa Benitez na nahodha Steven Gerrard, Liverpool ikawa mshindi wa ulaya kwa mara ya tano 2005.[1]

Liverpool ilikuwa ya tisa kwa usajili mkubwa duniani 2016-17 ikitumia €424.2 milioni na ikawa klabu ya nane kwa thamani duniani mwaka 2017 kwa thamani ya $1.492 bilioni.Imedumu kwa muda mrefu ligi kuu pamoja na Manchester United na Everton F.C..[2]

Mashabiki wa timu hiyo wamehusishwa kwenye maafa mara mbili;Uwanja wa Heysel,ambapo mashabiki waliokuwa wakijaribu kukimbia walibanwa na ukuta uliokuwa unaanguka kwenye fainali za kombe la Ulaya 1985 mjini Brussels, ambapo watu 39 - wengi Waitalia na mashabiki wa Juventus - walikufa. Baadaye timu za Uingereza zilipewa adhabu ya kutoshiriki michuano ya Ulaya na Hillsborough ilitokea ajali mwaka 1989,ambapo mashabiki wa Liverpool 96 walifariki walipoangukiwa na ukuta.

Toka mwaka 1964 timu ilibadili mavazi ya fulana nyekundu na bukta nyeupe na zote kuwa nyekundu ikiwa nyumbani na mavazi hayo kutumika mpaka sasa. Na kauli mbiu ya timu ni "You'll Never Walk Alone".

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Liverpool F.C. kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.