Steven Gerrard

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Steven Gerrard

Steven George Gerrard (alizaliwa tarehe 30 Mei 1980) ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu kutoka Uingereza, timu ya Liverpool ambaye sasa ni mfanyakazi wa akademi hiyo. Kwa sasa ni mtangazaji wa mpira wa miguu kwenye kituo cha BT Sport's.

Alikuwa akicheza kwenye nafasi ya kiungo wa kati kwenye klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Uingereza na akiwa nahodha wa timu hizo. Akitambulika kuwa kiungo bora kwa kipindi alichokuwa akicheza, Gerrard alipewa tuzo ya mchezaji bora wa UEFA ngazi ya klabu, 2005 akiwa mshindi wa tatu kwenye kinyang'anyiro cha mchezaji bora wa dunia. Mwaka 2009 Zinedine Zidane na Pelè walimchagua kuwa mchezaji bora wa dunia. Gerrard alikuwa na sifa ya kuwa na kiwango kizuri uwanjani hata kwenye uongozi, Gerrard ni mchezaji wa kwanza kushinda goli kwenye fainali za FA Cup, fainali za kombe la ligi na fainali za UEFA na kushinda kwenye kila fainali.

Alhaj Diof aliwahi kumtuhumu nahodha huyo wa Liverpool na Uingereza kwa kuonesha ubaguzi waziwazi kwa kusema Ligi ya Uingereza ni kwa ajili ya Wazungu sio ya Waafrika.

Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Steven Gerrard kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.