Chelsea F.C.
Chelsea FC.svg | ||||
Jina kamili | Chelsea Football Club | |||
---|---|---|---|---|
Jina la utani | The Blues The Pensioners (zamani)[1] | |||
Imeanzishwa | 10 Machi 1905[2] | |||
Uwanja | Stamford Bridge (Uwezo: 40,341[3][4]) | |||
Mmiliki | Todd Boehly Clearlake Capital Hansjörg Wyss Mark Walter | |||
Mwenyekiti | Bruce Buck | |||
Kocha | Thomas Tuchel | |||
Ligi | Ligi Kuu Uingereza (EPL) | |||
2021-22 | Premier League, 3th | |||
Tovuti | tovuti ya klabu | |||
|
Chelsea Football Club[5][6] [7][8]ni klabu ya mpira wa miguu ya nchini Uingereza iliyo na maskani yake Fulham, London. Klabu hii ilianzishwa mwaka 1905, na kwa miaka mingi sana imekuwa ikishiriki ligi kuu ya Uingereza. Uwanja wao wa nyumbani ni Stamford Bridge ambao una uwezo wa kuingiza watazamaji 41,837, wameutumia uwanja huu tangu klabu ilivyoanzishwa.
Chelsea, kwa mara ya kwanza ilipata mafanikio makubwa mwaka 1955, ambapo walipata ubingwa wa ligi, na walishinda mataji kadhaa katika miaka ya 1960, 1970, 1990 na 2000. Klabu hii imefurahia zaidi mafanikio katika miongo miwili ilopita, kwa kushinda mataji makubwa 15 tangu mwaka 1997.
Nyumbani, Chelsea imeshinda ubingwa wa ligi mara nne, kombe la FA mara saba, kombe la ligi mara nne, pamoja na ngao za jamii mara nne. Na kimataifa Chelsea imeshashinda UEFA Cup Winners' Cups mara mbili, UEFA Super Cup moja, UEFA Europa League moja na UEFA Champions League moja. Chelsea ndio klabu pekee kutoka London kushinda UEFA Champions League, na ni moja kati ya klabu nne kutoka Uingereza, kuchukua makombe yote makubwa matatu ya Ulaya.
Kwa kawaida Chelsea huvaa jezi ya bluu, kaptula ya bluu na soksi nyeupe. Nembo ya klabu imebadilishwa mara nyingi kulingana na wakati na kuboresha muonekano wa klabu. Nembo ya sasa inaonesha picha ya simba akiwa amebeba mkuki. Tangu Julai 2003, Chelsea imekuwa ikimilikiwa na bilionea wa Kirusi, Roman Abramovich. Tarehe 7 Mei 2022, Chelsea ilithibitisha kwamba masharti yametimiza na kikundi kipya cha umiliki, kinachoongozwa na Todd Boehly, Clearlake Capital, Mark Walter na Hansjörg Wyss, kununua klabu hiyo.[9] Mnamo tarehe 25 Mei 2022, serikali iliidhinisha kuuzwa kwa Chelsea kwa £4.25bn. Mnamo tarehe 30 Mei 2022, mauzo yalikamilika, na hivyo kumaliza umiliki wa miaka 19 wa Abramovich.[10]
Wachezaji[hariri | hariri chanzo]
Kikosi cha timu ya kwanza[hariri | hariri chanzo]
Kama ilivyokuwa tarehe 10 Agosti 2022, kulingana na vyanzo mseto katika tovuti rasmi.[11]
Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.
|
|
Nje kwa mkopo[hariri | hariri chanzo]
Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.
|
|
Wa ziada na walio chuoni[hariri | hariri chanzo]
Orodha ya wachezaji wa kikosi cha ziada na walio chuoni ambao wamewahi kucheza kikosi cha kwanza.
Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.
|
|
Mchezaji Bora wa Mwaka[hariri | hariri chanzo]
Chanzo: Chelsea F.C.
Tuzo[hariri | hariri chanzo]
- Ligi Kuu (6) 1954-1955, 2004-2005, 2005-2006, 2009-2010, 2011-2012, 2016-2017
- FA Cup (7) 1970, 1997, 2000, 2007, 2009, 2010, 2018
- Kombe la Ligi (4) 1965, 1998, 2005, 2007;
- Ngao ya Jamii (4) 1955, 2000,2005, 2009
- UEFA Cup Winners' Cup (2) 1971, 1998
- UEFA Super Cup (1) 1998, 1999, 2003
- Full Members Cup (2) 1986, 1990
- FA Youth-cup (3) 1960, 1961, 2010
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
- ↑ "Chelsea's first cup final – a century ago". Chelsea FC. 23 April 2015. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 August 2016. Iliwekwa mnamo 25 July 2016. Unknown parameter
|url-status=
ignored (help); Check date values in:|date=, |archivedate=, |accessdate=
(help) - ↑ "Team History – Introduction". chelseafc.com. Chelsea FC. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 May 2011. Iliwekwa mnamo 11 May 2011. Unknown parameter
|url-status=
ignored (help); Check date values in:|archivedate=, |accessdate=
(help) - ↑ "General Club Information" (kwa Kiingereza). | site=chelseafc.com.
- ↑ "Premier League Handbook 2020/21". Premier League. uk. 12. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 April 2021. Iliwekwa mnamo 12 April 2021. Unknown parameter
|url-status=
ignored (help); Check date values in:|archivedate=, |accessdate=
(help) - ↑ Danyal Khan, Jake Stokes (2022-05-03). "Chelsea news and transfers LIVE: Todd Boehly takeover hint, Abramovich fear". Football.London (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-03.
- ↑ Bobby Vincent (2022-05-03). "Chelsea could look to reunite Lautaro Martinez and Romelu Lukaku in the summer". Football.London (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-03.
- ↑ Luke Thrower (2022-05-04). "Glen Johnson urges Chelsea to offer Jorginho a new contract amid transfer links". Football.London (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-04.
- ↑ Luke Thrower (2022-05-04). "Chelsea bidder Lord Coe warns club to find quick takeover solution". Football.London (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-04.
- ↑ "Club statement". www.chelseafc.com (kwa en-gb). Iliwekwa mnamo 2022-08-13.
- ↑ "https://twitter.com/fabrizioromano/status/1531290432327634944". Twitter (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-08-13.
- ↑ "Men: Senior". Chelsea F.C. Iliwekwa mnamo 6 August 2022. Check date values in:
|accessdate=
(help)
"Men: On Loan". Chelsea F.C. Iliwekwa mnamo 6 August 2022. Check date values in:|accessdate=
(help)