Cote d'Ivoire

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Côte d'Ivoire)
Cote d'Ivoire


Abidjan ni mji mkubwa na muhimu zaidi kiuchumi wa Ivory Coast .

Côte d'Ivoire (tamka: kot divwar; kwa Kifaransa jina lina maana ya Pwani ya pembe za ndovu; kwa Kiingereza: Ivory Coast; kwa Kiswahili pia: Kodivaa) ni nchi ya Afrika ya Magharibi.

Imepakana na Liberia na Guinea upande wa magharibi, Mali na Burkina Faso kaskazini, Ghana mashariki na Ghuba ya Guinea ya Atlantiki upande wa kusini.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Baada ya uhuru (7 Agosti 1960) iliwahi kuwa kati ya nchi tajiri zaidi za Afrika lakini tangu mwaka 2002 uchumi na hali ya maisha kwa jumla vimeharibika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe (2002-2011).

Ramani ya Côte d'Ivoire

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wakazi walikadiriwa kuwa 29,344,847 mwaka 2023, lakini sensa ya mwaka huo ilihesabu idadi ndogo zaidi: 29,389,150.

Kabila kubwa ni lile la Waakan (38%). Asilimia 22% ni wahamiaji, hasa kutoka nchi jirani (Liberia, Burkina Faso na Guinea). Asilimia 4 wana asili tofauti, hasa Ufaransa, Lebanoni, Vietnam na Hispania.

Lugha zinazotumika kawaida ni 68, lakini lugha rasmi ni Kifaransa.

Upande wa dini, Uislamu una 42.5%, Ukristo 39.8% (Kanisa Katoliki peke yake 24.9%), dini asilia za Kiafrika 2.2% na dini nyingine 0.5%. Wasio na dini ni 12.6%

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons

Serikali

Habari

Overviews

Biashara

Orodha

Utalii

Mengineyo


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Cote d'Ivoire kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.