Alassane Ouattara
Mandhari
Alassane Dramane Ouattara (amezaliwa 1 Januari 1942) ni mwanasiasa wa Ivory Coast ambaye amekuwa Rais wa Ivory Coast (Côte d'Ivoire) tangu mwaka 2010.
Mtaalamu wa uchumi na taaluma, Ouattara alifanya kazi kwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki Kuu ya Nchi za Afrika Magharibi (kwa Kifaransa: Banque Centrale des Etats de l'Afrique de l'Ouest, BCEAO).
Alikuwa Waziri Mkuu wa Côte d'Ivoire kutoka Novemba 1990 hadi Desemba 1993, aliyeteuliwa wadhifa huo na Rais Félix Houphouët-Boigny.
Ouattara alipata kuwa Rais wa Rally of the Republicans (RDR), chama cha siasa cha Ivory Coast, mnamo 1999.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Alassane Ouattara kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |