Nenda kwa yaliyomo

Uwanja wa michezo wa Santiago Bernabéu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa Santiago Bernabéu
Mwonekano wa ndani wa uwanja
Jina maarufuEl Bernabéu
EneoMadrid, Hispania
Ufunguzi14 Desemba 1947
Uwezo83,186
Aina ya nyasiNyasi Mseto (Hybrid Grass)

Uwanja wa michezo wa Santiago Bernabéu (Kihispania: Estadio Santiago Bernabéu) ni uwanja wa michezo uliopo Madrid, Hispania.

Umekuwa uwanja wa nyumbani wa Real Madrid tangu kukamilika kwake mnamo 1947[1].

Kwa sasa uwanja una uwezo wa kuchukua watazamaji 83,186. Ni uwanja wa 3 kwa ukubwa ulaya na unashika nafasi ya 2 nchini uhispania[2].

Santiago Bernabéu ni kimoja kati ya viwanja maarufu duniani. Imeshuhudia fainali za Ligi la Mabingwa Ulaya mara nne: mnamo mwaka 1957, 1969, 1980 na 2010 na ilisimamia mzunguko wa pili wa fainali za Copa Libertadores.

Mechi za fainaliza UEFA UERO za mwaka 1964 na Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 1982 pia zilifanyika Santiago Bernabéu, ikaufanya uwanja huu kuwa uwanja wa kwanza Ulaya kusimamia Ligi la Mabingwa Ulaya, Fainali za Kombe la Dunia la FIFA na Fainali za Copa Libertadores.

Mwaka 2018 baada ya vurugu kuibuka kwenye fainali ya Copa Libertadores kati ya Rivar Plate na Boca Juniors mechi ya marudiano iliandaliwa Santiago Bernabeu

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Santiago Bernabéu kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.