Montevideo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Montevideo
Nchi Uruguay
Mji wa Montevideo.
Montevideo

Montevideo ni mji mkuu wa Uruguay na mji mkubwa nchini. Uko kwenye mdomo mpana wa mto Rio de la Plata. Karibu nusu ya watu wote wa Uruguay hukaa jijini; milioni 1.35 mjini wenyewe na milioni 1.9 katika rundiko la jiji.

Jina "Montevideo" linamaanisha "Naona mlima".

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wareno walijenga boma katika eneo la mji wa baadaye mnamo mwaka 1724. Walifukuzwa na Wahispania na tarehe 24 Desemba 1726 gavana Mhispania wa Buenos Aires Bruno Mauricio de Zabala aliunda mji wa Montevideo.

Tangu mwaka 1828 mji umekuwa mji mkuu wa nchi ya Uruguay.

Mji ulikua kutokana na uhamiaji mkubwa kutoka Ulaya hasa Italia. Wakazi wengi wa Montevideo wana asili ya nchi hiyo.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Uruguay bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Montevideo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.