Zlatan Ibrahimovic

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Zlatan Ibrahimovic (2013)

Zlatan Ibrahimovic (alizaliwa 3 Oktoba 1981) ni mchezaji wa mpira wa miguu aliye maarufu duniani.

Ni mzaliwa wa Sweden na ni mshambulizi mkali sana. Anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira ufikapo miguuni pake, pia ana uwezo mkubwa sana wa kupiga mashuti makali mno kana kwamba akiwa yeye na kipa, kipa hana ujasiri wa kudaka mpira wake.

Baadhi ya timu alizochezea ni: AFC Ajax, Barcelona F.C., Inter Milan, AC Milan, Manchester United na PSG ambapo alipata mafanikio makubwa sana, na hata kujinyakulia baadhi ya makombe makubwa likiwemo kombe la UEFA, kombe la ligi kuu Ufaransa, Ligue 1 mara 15 na mengine makubwa.

Kwa sasa Ibrahimovic anachezea tena timu ya A.C. Milan inayopatikana Italia.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zlatan Ibrahimovic kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.