Nenda kwa yaliyomo

Deco

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Deco

Deco (jina halisi: Anderson Luís de Souza; alizaliwa 27 Agosti 1979) alikuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno na klabu mbalimbali za Ulaya ambazo ni Porto, Barcelona F.C. na Chelsea F.C..

Deco alianza kufahamika katika tasnia ya mpira wa miguu alipoanza kuichezea klabu ya Benfica ya nchini Ureno mwaka 1997.

Mwaka 1999 alihamia Porto ya nchini Ureno na kufanikiwa kushinda kombe la ligi kuu la nchini humo.Mwaka 2004 alihamia klabu ya FC Barcelona ya nchini Hispania ambapo aliiwezesha kuchukua kombe la La Liga.

Mwaka 2008 Deco alihamia timu ya klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza ambapo alicheza mpaka mwaka 2010.

Deco alistaafu kucheza mpira wa miguu 26 Agosti 2013 baada ya kupata majeraha.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Deco kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.