Tasnia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tasnia


Tasnia (kutoka Kiarabu: تصنيع, kwa Kiingereza: industry, manufacturing) ni neno la kutaja matawi mbalimbali ya uchumi wa nchi ambako bidhaa zinatengenezwa au huduma kutolewa.

Kiasili tasnia ilimaanisha hasa shughuli ambako watu wanashirikiana kuzalisha bidhaa wakibadilisha malighafi kuwa vitu vinavyotumika na binadamu, kwa hiyo shughuli za sekta ya pili ya uchumi pamoja na sekta ya viwanda.

Matumizi ya istilahi imepanuka kufuatana na Kiingereza "industry"[1] kumaanisha pia utoaji wa malighafi (sekta ya msingi) na huduma (sekta ya tatu ya uchumi).

Tasnia ya kisasa hutegemea mgawanyo wa kazi na usanifishaji wa kazi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. [https://www.dictionary.com/browse/industry Industry], tovuti ya dictionary.com
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tasnia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.