Lionel Messi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Messi mnamo Agosti 2015.

Lionel Andrés Messi (amezaliwa Rosario, Argentina, 24 Juni 1987) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchi ya Argentina.

Tangu mwaka 2003 amekichezea klabu cha Fc Barcelona (Hispania).

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa akiwa njiti (yaani kabla ya miezi 9), akachukuliwa na Barcelona akiwa na umri wa miaka nane (8). Akalelewa ndani klabu ya kukuzia vipaji ya Barcelona inayofahamika kama Katalunya (Catalan), akichezea timu ya watoto akiwa ndiye mwenye umri mdogo zaidi.

Alianza kuchezea timu ya wakubwa mwaka 2003, akiwa anavaa namba 19 mgongoni,wakati namba 10 ilikuwa inavaliwa na Mbrazili Ronaldinho.

Messi kipindi cha mazoezi mwaka 2006

Aliaanza kuingia kwenye historia ya soka duniani mwaka 2009 baada ya kuiwezesha Barcelona kutwaa ubingwa wa klabu bingwa Ulaya (UEFA), na FIFA kumpa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia.

Messi alikulia katika kituo cha kukuzia vipaji cha barca, La Masia, akiwa na miaka 13.

Aliendeleza historia na kuweka historia ya pekee duniani kwa kuchukua tuzo hiyo mara 4 mfululizo.

Messi dhidi ya mchezaji wa brazili Marcelo nusu fainali ya mashindano ya olimpiki ya mwaka2008 .
People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lionel Messi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.