Beki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Beki Philipp Lahm (kulia) akijaribu kumzuia winga Nani.

Beki (kutoka neno la Kiingereza "back"; pia mlinzi kutoka kitenzi "kulinda") ni mchezaji wa nafasi ya ulinzi karibu na goli katika michezo mbalimbali kama vile: mpira wa miguu, ragbi, hoki ya ugani n.k.

Katika soka, beki ni mchezaji wa ndani ambae jukumu lake la msingi ni kuzuia wachezaji wa timu pinzani kufunga katika lango lao, wachezaji hawa hucheza mbele ya Golikipa.

Kuna aina nne ya mabeki: Beki wa kati, Mfagiaji, Beki wakabaji na Beki wasaidizi. Beki wa Katina Beki wakabaji ni nafasi ambazo ni za muhimu katikia mifumo mingi. Beki wasaidizi na wafagiaji hutegemea na aina ya mfumo unaotumika.

Beki wa kati[hariri | hariri chanzo]

Beki wa kati John Terry (26 jezi ya bluu) akimdhibiti mshambuliaji Didier Drogba

Beki wa kati (kwa jina lingine mlinzi/walinzi wa kati) hulinda eneo lililopo mbele ya lango moja kwa moja, wakiwa uwanjani hujaribu kuwazuia wachezaji wa timu pinzani hasa hasa Washambuliaji wasifunge. Wanaweza kufanya hivi kwa kuzuia mashuti yapigwayo, kuzuia mipira ya juu kwa kupiga vichwa na kuwa karibu na mchezaji wa timu pinzani ili kupunguza urahisi wa mchezaji kupigiwa pasi.

Mfumo maarufu wa 4-4-2, beki wa kati wawili hutumika.

Wakiwa na mpira, beki wa kati wanategemewa kutoa pasi ndefu na yenye uhakika kwa wachezaji wenzake au kuupiga mbele bila kumlenga mchezaji mwenzake, lengo likiwa ni kuuondoa mpira karibu na lango lake kwa kadri awezavyo. Kutokana na mbinu nyingi katika soka la kisasa, beki wa kati hutegemewa kumiliki mpira zaidi, katika beki wawili wa kati, timu nyingi zimekua zikiambatanisha beki mmoja mwenye nguvu na mmoja mwenye wepesi sana, hii inasaidia kuimarisha ulinzi na kumiliki mipira na kuisogeza mbele kwa urahisi zaidi, mfano wa pea hizo ni pamoja na Kelvin Yondan,John Terry na Ricardo Carvalho walipokua klabu ya Chelsea, Sergio Ramos, Raphaël Varane au Pepe wakiwa Real Madrid, Nemanja Vidić na Rio Ferdinand wakiwa Manchester United, au Giorgio Chiellini, Leonardo Bonucci, Andrea Barzagli na Medhi Benatia wakichezea Juventus.[1][2]

Katika mchezo wa kawaida, Beki wa kati wanakua na nafasi ndogo sana ya kufunga. Hata na hivyo, wakati wa upigaji wa mipira iliyokufa aidha kona na faulu, beki hupanda katika eneo la Penalti la timu pinzani kwani huwa na uwezo mkubwa wa kuicheza mipira ya juu kwa kichwa. Wakati huu, beki wasaidizi au viungo wa kati huziba nafasi ya beki wa kati kwa muda.

Baadhi ya beki wa kati wanajulikana sana kwa uwezo wao wa kupiga mipira iliyokufa kwa ufasaha zaidi hasa ikiwa katika umbali mrefu kutoka lango la timu pinzani. Beki wa kati wa Brazili David Luiz, Alex, na Naldo wanajulikana zaidi kwa upigaji wa mipira ya aina hii, upigaji wao ni wa kutumia nguvu zaidi.

Katika mpira wa kisasa, timu nyingi hutumia beki wawili au watatu wa kati wakicheza mbele ya golikipa. Mfumo wa 4–2–3–1, 4–3–3 na 4–4–2 hutumia beki wawili wa kati.

Kuna aina mbili za ukabaji zinzotumiwa na mabekiwa kati, kukaba kwa nafasi, ambapo kila beki huwa na nafasi yake maalumu uwanjani, na kukaba mtu kwa mtu ambapo kila beki humkaba nmshambuliaji maalumu wa timu pinzani.

Mfagiaji (libero)[hariri | hariri chanzo]

<centre>mfumo wa 5–3–2 ukiwa na mfagiaji

Mfagiaji (kwa jina lingine libero) ni aina ya beki wa kati mnyumbulifu anayeondoa mipira mshambuliajia akifanikiwa kupita ukuta wa mabeki.[3][4] Nafasi hii ni nyumbulifu zaidi tofauti na aina nyingine ya mabeki ambao hukaba wapinzani kwa karibu zaidi, kwa sababu hioyo, aina hii ya mabeki imepewa jina la libero.[5][6]

Japo wafagiaji hutegemewa kujenga mashambulizi ya kushtukiza, jukumu linalohitaji ujuzi mkubwa wa kukokota mipira na kuopiga pasi za ufasaha mkubwa, vipaji vyao mara nyingi havitegemei ujuzi mkubwa wa kukaba. Mfano mfumo wa uchezaji ujulikanao kwa lugha ya kiingereza catenaccio uliotumika zaidi nchini Italia miaka ya 60, ulitumia aina hii ya beki ambaye muda mwingi alikua akizurura nyuma ya ukuta wa mabeki.[7][8]

Inaaminika kuwa nafasi hii ilishughulikiwa zaidi na Franz Beckenbauer, Gaetano Scirea, na Elías Figueroa, japo sio wa kwanza kucheza katika nafasi hii, wachezaji wa mwanzo wa nafasi hii inawajumuisha wachezaji kama Alexandru Apolzan, Ivano Blason, Velibor Vasović, na Ján Popluhár.[9][10][11][12][13][14][15] Beki wengine wanaoelezewa kama wafagiaji na pamoja na Bobby Moore, Franco Baresi, Ronald Koeman, Fernando Hierro, Matthias Sammer, na Aldair, kutokana na ufundi wao kwenye kuchezea mpira, uwezo wa kuona na kupiga pasi za umbali mrefu.[9][10][11][16] Japo nafasi hii haitumiki katika mpira wa kisasa, nafasi hii inabaki kuwa ya muhimu sana na yenye kuheshimika.

Beki wasaidizi[hariri | hariri chanzo]

Beki wa pembeni Caitlin Foord wa timu ya taifa ya wanawake ya Australia katika moja ya michezo ya kombe la alva (2017 Algarve Cup)

Kwa kiingereza (wing-backs) ni aina ya walinzi au beki wanaotumika zaidi kushambulia timu pinzani. Aina hii ya mabeki wanaweka nguvu kubwa zaidi kwenye kushambulia zaidi ya kukaba, lazima wawe na uwezo wa kurudi nyuma kuzuia mashambulizi au kupunguza athari za ushambuliaji za timu pinzani. Kazi za mabeki hawa hutofautiana kulingana na aina ya mfumo ya timu, kuna mifumo inayowalazimu kukaba zaidi na mingine inawapa uhuru wa kushambulia zaidi. Mabeki hawa mara nyingi hutumika katika mifumu yenye mabeki watatu wa kati, na mara nyingine huitwa viungo.

Katika mabadiliko ya soka la kisasa, mabeki wasaidizi ni mjumuisho wa viungo wa pembeni na mabeki wakabaji. Hivyo basi, ni eneo linalohitaji matumizi mengi ya nguvu. Mabeki wasaidizi ni nafasi ya kiujumla sana, na mara nyingi hutegemewa kucheza upana kwa timu zisizotumia winga.[17]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Judges have a blindspot when destroyers like Vidic play a blinder. The Guardian (19 January 2011). Iliwekwa mnamo 2 February 2017.
  2. Giorgio Chiellini: ‘I have a strong temperament but off the pitch I am more serene’. The Guardian (13 June 2016). Iliwekwa mnamo 2 February 2017.
  3. BBC Sports Academy
  4. Evolution of the Sweeper. Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-08-24. Iliwekwa mnamo 2019-10-15.
  5. DIZIONARIO DI ITALIANO DALLA A ALLA Z: Battitore (Italian). La Repubblica. Iliwekwa mnamo 21 April 2016.
  6. Damele, Fulvio (1998). Calcio da manuale. Demetra. p. 104. 
  7. La leggenda della Grande Inter (Italian). Inter.it. Jalada kutoka ya awali juu ya 19 October 2012. Iliwekwa mnamo 10 September 2014.
  8. Il volo di Bonucci e la classifica degli 8 migliori difensori italiani di sempre (Italian). Il Corriere della Sera (23 November 2016). Iliwekwa mnamo 27 December 2016.
  9. 9.0 9.1 BBC Football - Positions guide: Sweeper. BBC Sport (1 September 2005). Iliwekwa mnamo 5 January 2008.
  10. 10.0 10.1 Remembering Scirea, Juve's sweeper supreme. FIFA.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-07-11. Iliwekwa mnamo 5 January 2015.
  11. 11.0 11.1 Franz Beckenbauer Biography. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-01-21. Iliwekwa mnamo 5 January 2015.
  12. Rotting fruit, dying flowers The Guardian
  13. Czechoslovakia World Cup Hero Jan Popluhar Dies Aged 75 Goal.com
  14. VELIBOR VASOVIC Archived 29 Desemba 2019 at the Wayback Machine. The Independent
  15. Evolution of the Sweeper. Outsideoftheboot.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-08-24. Iliwekwa mnamo 2019-10-15.
  16. Franchino (detto Franco) BARESI (II). Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-05-12. Iliwekwa mnamo 5 January 2015.
  17. Positions guide: Wingback. BBC Sport (1 September 2005). Iliwekwa mnamo 21 June 2008.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Beki kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.