Sergio Ramos

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sergio Ramos akiwa na Real Madrid
Sergio Ramos akimiliki mpira

Sergio Ramos Garcia (kwa Kihispania hutamkwa [ˈserxjo ˈramos ɣarˈθi.a]; alizaliwa tarehe 30 Machi 1986) ni mchezaji na nahodha wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania anacheza kama beki wa kati na pia ana uwezo wa kucheza kama beki wa kulia.

Alitokea katika akademi ya Sevilla na mwaka 2005 alihamia Real Madrid na akawa mchezaji muhimu na mpaka sasa ameshinda mataji ya UEFA mara tatu na La Liga mara nne na akawa mfungaji bora anayecheza nafasi ya ulinzi.

Na kwa timu ya taifa Ramos ameisaidia timu yake kwenye kombe la dunia mara tatu wakawa washindi mwaka 2010 na UEFA Euro kushinda miaka ya 2008 na 2012.Ramos alianza kuonesha uwezo wake akiwa na miaka 18,na akawa mchezaji bora wa timu ya taifa mwenye umri mdogo mwenye mafanikio makubwa.

Ramos anajulikana kama beki bora kwa wakati wake,alikuwa beki bora wa La Liga na alishinda kikosi bora cha UEFA.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sergio Ramos kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.