Nenda kwa yaliyomo

Robert Pires

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Robert Pires ni mchezaji wa zamani wa timu ya Ufaransa

Robert Pires (jina kamili: Robert Emmanuel Pires; amezaliwa Ufaransa, 29 Oktoba 1973) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa nchi ya Ufaransa.

Pires alizaliwa na baba wa Ureno na mama wa Hispania. Alichezea vilabu viwili vya Ufaransa kabla ya kwenda Arsenal. Alivyokuwa timu hiyo ya Arsenal alishinda kombe mbili za FA na mataji mawili ya ligi kuu. Mchezaji huyu alishawahi kupata mataji 79 kati ya 1996 na 2004 kwa nchi yake, pamoja na kushinda Kombe la Dunia la FIFA la 1998 na UEFA Euro 2000.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Robert Pires kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.