Taekwondo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wapiganaji wa taekwondo.

Taekwondo ni mchezo wa upiganaji ulioanzishwa nchini Korea.

Sifa za upiganaji huo ni kuruka mateke yenye urefu wa kichwa cha mtu anayepigana naye, mateke ya kuruka na kuzunguka hewani, na kupigana harakaharaka.

Taekwondo ilianzishwa wakati wa miaka ya 1940 na 1950 na wanajeshi wa Kikorea wenye ujuzi katika martial arts kama taekkwon karate, na wapiganaji wa Kikorea kama vile Taekkyeon, Subak, na Gwonbeop.

Taasisi ya zamani ya taekwondo ni Korean Taekwondo association (KTA), iliyoanzishwa mwaka wa 1959 kupitia jitihada za ushirikiano na wawakilishi kutoka shule za taekwondo na shule za karate huko Korea.

Tangu mwaka 2000 ni kati ya michezo ya Olimpiki.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Taekwondo kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.